Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




YONA – NABII WA UAMSHO!

JONAH – THE PROPHET OF REVIVAL!
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.,
Mchungaji Mstaafu

Mahubiri yaliyo hubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku Ya Bwana Alasiri, Juni 14, 2020
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Afternoon, June 14, 2020

“Basi neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu” (Yona 1:1, 2).


Kitabu cha Yona kiliandikwa na nabii Yona mwenyewe. Ninasema hivyo kwa sababu kinafunua mawazo ya Yona na maombi yake ambayo hakuna mwingine angeyajua isipokuwa yeye mwenyewe. Ukweli kwamba Yona alikuwa mtu anayejulikana katika historia unapatikana katika II Wafalme 14:24-25 wakati ambapo marabi wa zamani walimwita, “Yona mwana wa Amitai, nabii, kutoka Gath-heferi” (II Wafalme 14:25). Bwana Yesu Kristo Mwenyewe alimtaja Yona kuwa nabii halisi anayepatikana katika historia. Tafadhali fungua Mathayo 12:39-41. Simama ninaposoma mambo ambayo Yesu aliyasema kumhusu Yona,

“Lakini yeye akawajibu, “Kizazi kiovu na cha uzinzi kinaomba ishara! Lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya nabii Yona. Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la nyangumi kwa siku tatu, usiku na mchana, vivyo hivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika moyo wa nchi siku tatu, usiku na mchana. Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu waliposikia mahubiri ya Yona. Na tazama, hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona.” (Mathayo 12:39-41).

Salia umesimama na ufungue pamoja nami Luka 11:29-30.

“Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu akawaambia, “Kizazi hiki ni kizazi kiovu. Kinataka ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya Yona. Jinsi Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninewi, ndivyo pia Mwana wa Mtu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki.” (Luka 11:29-30).

Unaweza Kuketi.

Hivyo II Wafalme 14:25 inasimulia habari ya kihistoria kumhusu Yona. Katika Luka 11:29-30 kuna habari kwamba Yesu Christo alimtaja Yona kama ishara. Na katika Mathayo 12:39-41 inasimulia kuhusu kufufuka kwa Yona kama ishara ya kuzikwa na kufufuka kwa Yesu Kristo baada ya siku tatu baada ya kuzikwa kwake. Hivyo, Agano la Kale linayo habari kwamba Yona alikuwa mtu halisi, na Kristo Mwenyewe anatuambia kwamba kifo cha Yona na kufufuka kwake ulikuwa unabii wa kufa na kufufuka Kwake.

Sir Winston Churchill alisema vyema, “Hatujashawishika na vitabu vikubwa vya kiliberali vya Profesa Gradgrind na Dkt. Dryasdust. Tuna hakika kwamba mambo haya yote yalitendeka kama yanavyosimuliwa na maandiko matakatifu [Biblia].” (Ilinukuliwa na Dkt. J. Vernon McGee, Kupitia katika Biblia, juzuu III, dokezo kuhusu Yona, Utangulizi, uk. 738).

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +
MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

I. Kwanza, Kuitwa kwa Yona.

“Basi neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake …” (Yona 1:1, 2).

Mstari wa 3,

“Basi, Yona akaanza safari… ili kumkwepa Mwenyezi-Mungu.” (Yona 1:3).

Ninamuelewa huyu mtu anayeitwa Yona. Hiyo ndiyo sababu kitabu hiki kidogo cha Yona ni kimoja cha vitabu ninavyo penda katika Agano la Kale. Yona alitoroka kutoka kwa uwepo wa Bwana. Mimi sikufanya hivyo. Niliitwa kuwa mmisionari na nilijua hivyo vyema. Lakini nilikuwa mwanafunzi maskini kiasi cha kwamba nilijua singeweza kuhitimu kutoka kwa Chuo nilikosomea. Nilihitajika nihitimu kutoka chuoni na pia katika Seminari ili niwe mmisionari wa Southern Baptist. Lakini hata hivyo nilijihisi kama Yona. Nilijua nimeitwa, lakini nilijaribu kutoroka kutokan kwa uwepo wa Mungu kwa sababu nilikuwa na woga kwamba sitaweza kuhitimu chuoni. Mungu alikuwa ananiambia nifanye jambo ambalo haliwezekani.

Kijana mmoja mchanga mwanafunzi wa seminari aliniambia, “Siwezi kujihuzisha na huduma kwa sababu ninajua nitalemewa.” Alikuwa anaogopa kutofaulu katika huduma. Nilifikiria kuhusu hili jambo. Halafu nikasema, “Nimekuwa katika hali ya kukosa kufaulu mara nyingi kiasi cha kwamba siogopi hali hii tena.”

Woga usababisha mtu ambaye ameitwa na Mungu asifanye kazi ya huduma. Kila wakati huwa woga kwa njia moja ama nyingine. Kijana huyu alifaulu katika mambo yote aliyoyafanya – lakini aliogopa kufanya kazi ya huduma. Kakake mdogo alisema haya kumhusu, “Kakangu anaweza kufanya chochote.” Lakini angeweza kuwa huru kwa woga wa “kutofaulu.” Alikuwa na kimo cha futi sita, alikuwa mwanafunzi aliyehitimu kwa alama ya‘A’ chanya, na aliyekuwa na kipawa cha kuhubiri. Lakini alitoroka kutoka kwa uwepo wa Bwana kwa sababu ya woga!

Sasa, vijana nataka niwaambie jambo nililojifunza katika maisha, “Unaweza kufanya jambo lolote ambalo Mungu alikuita ulifanye – lolote!” Biblia inasema, “Naweza kufanya mambo yote katika yeye anipaye nguvu.” (Wafilipi 4:13). Kwa sababu nimethibitisha aya hiyo, najua ni kweli. Niko katika mwaka wangu wa 80 katika maisha, mtu aliyenusurika kutoka kwa saratani, na ugonjwa wa baridi yabisi katika magoti yangu, lakini siogopi, hata ingawa watu wawili waovu walichukua robo tatu za watu kutoka kwa kanisa letu katika mpasuko wa kanisa uliokuwa mbaya. Na bado mimi nimtulivu kama mtoto mdogo mikononi mwa mamake. Nina woga? Kwa kweli, sina woga hata kidogo! Nyanyangu kutoka upande wa mama kila mara alikuwa ananiambia, “Hauna chochote cha kuogopa isipokuwa woga wenyewe,” jambo ambalo alilisikia kutoka kwa Rais Franklin D. Roosevelt wakati wa Mshuko Mkubwa wa Uchumi. Na nikagundua ya kwamba nyanyangu aliyekuwa mzee alikuwa amesema ukweli!

Pia niligundua ya kwamba hauwezi ukatoroka “kutoka kwa uwepo wa Bwana.” Kwa nini? Kwa sababu Mungu yu pamoja nawe popote uendapo – hiyo ndiyo sababu! Unaweza kwenda, kama alivyoenda Yona, kule Tarshishi. Lakini Mungu yuko huko kama alivyokuwa kule nyumbani! Na Mungu atamwacha muhubiri aende bila mapambano makali.

Wakati mmoja nilimjua mtu aliyekuwa mlevi. nilipata kujua baadaye alikuwa anakunywa pombe ili ajisahaulishe katika mawazo yake kwamba Mungu alikuwa amemuita, lakini alikuwa mwoga sana kutii mwito wa Mungu. Kwa hivyo alikunywa pombe kila usiku kuuondoa ule woga. Jina lake lilikuwa Yohana Birch (bila mchezo.) na alikuwa pamoja nami kule seminari, alikuwa anatoroka kutoka kwa bweni mara kwa mara kwa sababu alikuwa mlevi!

Nilimjua mtu mwingine aliyeitwa Alan. Nilimwongoza Alan kwa Kristo, lakini ilikuwa vigumu sana. Kwa nini? Alan aliogopa kuokoka kwa sababu hilo lingemfanya aende Mbinguni! Kwanini aliogopa kwenda Mbinguni? Aliniambia siku moja, “Hilo litanifanya nimwone babangu tena na amekasirika nami sana kwa kutohudhuria seminari na kuwa mhubiri wa Kipresbiteri kama alivyokuwa.” alikuwa na umri wa zaidi ya miaka sitini. Aliketi katika kanisa la Kipresbiteri kila Juma Pili, akiogopa kuokoka kwa sababu marehemu babake angemkasirikia sana kule Mbinguni! Aliteswa na wazo hilo kwa zaidi ya miaka arobaini. Lakini niliweza kumshawishi kwamba babake [Kasisi Black] angetabasamu na kumkumbatia, kama alivyo fanya baba wa yule kijana mpotevu, kijana aliporudi nyumbani. alikuwa mtu wa kwanza niliyeongoza kwa Kristo!

Nilipokuwa seminari, msichana wa umri wa chuo aliokoka katika mojawapo ya mikutano yetu. Alikuwa msichana mwenye haya, lakini niliweza kugundua kwamba alikuwa anasumbuka, hivyo nikaenda kuzungumza naye. Alisema, “Ninaogopa kumwambia mamangu kwamba nimeokoka.” Nilimwambia, “Nenda umwambie. Hatakukasirikia.” Lakini nilikuwa nimekosea. Mamake alipojua kwamba ameokoka, alimfukuza nyumbani. Nilimuona huyo msichna akilia na nilisema, “Acha niende nikazungumze na mama yako.” Nilivaa suti na tai na nikaenda kumuona huyo mwanamke. Alipojua mimi ni nani, alianza kunipigia kelele. Mwishowe nikaingia katika chumba chake. Na nikasema, “Utamruhusu msichana wako kuja nyumbani?” Alisema, “Ningemvumilia alipokuwa akijiuzisha na ngono na madawa ya kulevya. Lakini sasa yeye ni Mkristo! Na sitawahi kumruhusu kuishi katika nyumba yangu.”

Maskini msichana huyu alikaribishwa katika nyumba ya mmoja wa washirika kanisani na akapata kazi, na akamaliza masomo katika chuo. Mwishowe aliolewa na kijana mmoja ambaye alikuwa Mkristo mzuri. Nilifahamu ya kwamba mama yake hakuhudhuria harusi ya binti yake. Jamii hiyo changa walienda kama wamisionari katika nchi iliyo katika Bara Ulaya. Huwa tunawatumia pesa kila mwezi kuwasaidia.

Halafu siku moja nilisikia kwamba watu wa magazeti walijazana katika mlango wa nyumba ya mama yake. Polisi walivunja mlango na wakampata mama yake – akiwa amekufa na amelala sakafuni – mkono wake ukiwa umeshikilia chupa iliyokuwa nusu ya vodka!

Lo, machozi na uchungu uliokuwaje msichana huyu aliopitia kuwa Mkristo na mmisionari! Lakini alimpenda Yesu vya kutosha ili kushinda woga na kumfuata Bwana katika viwanja vya misheni! Na alikuwa katika hali nzuri ya kiroho kuyasikia aliyoyasema Yesu, na kutii aliyoyasema.

Simama na ufungue katika Biblia yako Mathayo 10:34-39.

“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga. Maana nimekuja kuleta mafarakano kati ya mtu na baba yake, kati ya binti na mama yake, kati ya mkwe na mkwe wake. Na maadui wa mtu ni watu wa nyumbani mwake. Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi, hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. Mtu asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hanistahili. Anayeyashikilia maisha yake, atayapoteza; lakini anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata.” (Mathayo 10:34-39).

Unaweza kuketi.

Ninajua wengi wenu mnao wazazi ambao watajaribu kuwachawishi kuhama kanisa letu. Tafadhali kumbuka ujasiri wa msichana huyu na ufuate mfano wake. Ukifanya hivyo, watakukasirikia kwa muda. Lakini watakapoona tabia nzuri katika maisha yako, mwishowe – katika siku za usoni – wataandamana pamoja nawe kuja kanisani. Lakini ni lazima uwe na imani ya kumfuata Kristo, hata ikiwa hawatakukubali tena! Usiwe kama Yona na ujaribu kutoroka kutoka kwa uwepo wa Bwana!!!

Katika kanisa la Kichina, nilikuwa na marafiki wawili wa karibu – walioitwa Ben na Jack. Ben alikuwa mkaidi kwa Dkt. Lin. Mwishowe alimtorosha msichana aliyekuwa rafiki yake. Sikuwahi kumwona tena. Lakini Jack alihitimu kuwa mfamasi. Bado hakuipenda taaluma hiyo, hivyo alijiunga na chuo cha seminari cha Talbot na akawa mhubiri. Alikuwa rafiki wangu wa karibu. Nilisimamia harusi yake. Alimwamini Yesu katika mojawapo ya mikutano yetu. Halafu aliandika hivi, “Miaka mingi baadaye hili lilizaa matunda ya wokovu wa babangu na mamangu…nilishuhudia babangu akipokea elimu na kutumika kama mwalimu wa kufundisha watoto kanisani, aliboresha maisha ya wanafunzi wake jambo lililochangia ukuaji wa kanisa.”

II. Pili, Taabu ya Yona.

“Basi, Yona akaanza safari, lakini akashika njia ya kwenda Tarshishi ili kumkwepa Mwenyezi-Mungu. Akaenda hadi mjini Yopa ambapo alikuta meli moja iko tayari kwenda Tarshishi. Alilipa nauli, akapanda meli, akasafiri na mabaharia hao kwenda Tarshishi ili kumkwepa Mwenyezi-Mungu. Lakini Mwenyezi-Mungu akavumisha upepo mkali baharini, ikatokea dhoruba kali, meli ikawa karibu kabisa kuvunjika.” (Yona 1:3-4).

Tazama. Yona alijua ya kwamba dhoruba ile ilitoka kwa Mungu.

“Yona akawajibu, “Nichukueni mkanitupe baharini, nayo bahari itatulia, maana naona wazi kwamba dhoruba hii imewapata kwa sababu yangu mimi” (Yona 1:12).

Mwishowe wale mabaharia wakamchukua Yona wakamtupa baharini, na bahari ikatulia.

“Kisha, Mwenyezi-Mungu akaamuru samaki mkubwa ammeze Yona, naye akawa tumboni mwa samaki huyo kwa muda wa siku tatu, usiku na mchana. Basi, Yona, akiwa tumboni mwa samaki huyo, akawa akimwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wake” (Yona 1:17-2:1).

Nilikuwa na tatizo kuamini hili hapo mbeleni. Lakini baadaye niliona tukio hili lilikuwa kielelezo cha Yesu, aliyekufa Msalabani, akazikwa, na halafu akafufuka kutoka kwa wafu.

Baadaye nikasoma aliyoyasema Dkt. M. R. DeHaan kuhusu Yona na samaki aliyekuwa mkubwa. Dkt. DeHaan alisema Yona alikuwa amekufa ndani ya samaki mkubwa. Dkt. J. Vernon McGee alisema,

Kitabu hiki kwa kweli ni unabii wa ufufuo. Bwana Yesu Mwenyewe alisema kwamba kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa ninawi, atakuwa ishara katika kizazi chake kupitia kufufuka kwake…Kitabu hiki kidogo cha Yona kinaeleza na kufundisha ufufuo wa Bwana Yesu (Kupitia Biblia (Thru the Bible), Dokezo kuhusu ufufuo wa Yona kutoka kwa wafu, juzuu ya III, uk. 739).

Angalia Yona 1:17.

“Kisha, Mwenyezi-Mungu akaamuru samaki mkubwa ammeze Yona, naye akawa tumboni mwa samaki huyo kwa muda wa siku tatu, usiku na mchana” (Yona 1:17).

Sasa tazama maneno yaliyo na umuhimu zaidi katika kitabu cha Yona, maneno manne ya mwisho wa Yona 2:9,

“Wokovu hutoka kwa Bwana” (Yona 2:9b).

Acha nisimamie hapa na nikupe mawazo yangu kuhusu taabu ya Yona ndani ya samaki kubwa.

Nilipokuwa nikisoma kitabu cha Yona usiku mwingine, niliweza kuliona jambo sijawahi fikiria hapo awali. Ni jambo la kawaida kufikiria kwamba uamsho “unasababishwa” na hali za nje. Wahubiri wengi mashuhuri wanasema kwamba Virusi vya Korona vitasababisha ufufuo. Siamini hilo hata kidogo!!! Hilo ni wazo kutoka kwa mtu mbinafsi na mwenye kupuuza.

Lakini hapa kuna ukweli wa uamsho – uamsho “una sababishwa” (Ninachukua majina yanayotumiwa na madhehebu mapya ya Kiinjilsti) – uamsho “unasababishwa” na Mungu Mwenyewe, “Wokovu hutoka kwa Bwana” (Yona 2:9b).

Lakini kuna jambo nilisema wazi usiku mwingine – Tunaposoma kuhusu uamsho mkubwa katika historia, tunapata kwamba uamsho mkubwa unaanza viongozi wanapopitia mateso. Nitataja chache ambazo nitakumbuka.

Yohana Wesley – Ninataja tu kwa uchache mateso aliyopitia kabla ya Uamsho Mkuu wa Kwanza. Alikuwa ameshindwa kama mmisonari kule Georgia. Alipambana na mapepo. Mfano wake ulichomwa kwa kuchukiwa. Rafikiye George Whitefield alivunja ushirika naye. Alisingiziwa na dhehebu lake mwenyewe. Alisingiziwa katika kanisa la babake na akakatazwa meza ya Bwana na Mchungaji. Alioa mke ambaye alivuta nywele zake na kumwacha. Halafu Westly akapitia Pentekoste yake mwenyewe. Ni wakati huo tu ndipo alipoweza kupitia Pentecoste yake mwenyewe! Maelfu ya watu walihimili baridi kali ili wamsikilize akihubiri. Maisha yake na kazi yake zilizungumziwa na washauri wa Mfalme: “Hakuna mtu mmoja aliyeweza kushawishi watu wengi jinsi hivyo. Hakuna sauti iliyoguza watu wengi jinsi hivyo. Hakuna mtu mwingine aliyeweza kufanya kazi nyingine kama hiyo katika Uingereza.” Nyumba moja ya ushapishaji ilisema hivi majuzi, kwamba Yohana Westly alikuwa “mmoja wa wahubiri mashuhuri tangu wakati wa Mitume wa Yesu.”

Marie Monsen – Alianza kufunga na kuomba kwa sababu ya ufufuo kule China. Shetani alimfinyilia chini na kuupinda mwili wake kama nyoka mkubwa. Aliendelea bila msaada, mtu aliyekuwa na upweke, mwanamke mmisionari aliyeishi peke yake na aliyeombea uamsho mkuu unao endelea kupitia makanisa yanayoendele katika manyumba ya watu hata sasa nchini China.

Yonathani Goforth – Yeye na mkewe walienda China na huko waliteseka sana. Watoto wao wane walifariki. Bw. Goforth alikuwa karibu kufa mara mbili. Alisafirisha maiti za watoto wake kwa kutumia mkokoteni masaa 12 ili kuizika hiyo miili kwa njia ya Kikristo. Natamani kama ningekuwa na wakati ningekusimulia alivyo teseka mke wa Goforth pamoja na watoto wake. Mtoto wao Constance alipofariki, “mwili wa Costance mchanga ulizikwa kado ya kaburi la dadake siku ya kuzaliwa kwake, Octoba 13, 1902.”
     Ni wakati huo tu ndio moto wa Mungu ulishuka katika mikutano ya Goforth. Nafasi ya maombi ikapatikana. Bi. Goforth alisema, “Ilikuja kwa ghafla na kwa haraka kama radi…Kwa hiyo uamsho uliletwa na maombi. Haungezuilika na hakukuwa na juhudi zozote za kuuzuia…Wanaume kwa wanawake wakizama katika nguvu za Mungu… Wengine ambao walikuwa wamemwacha Bwana, walimrudia Bwana hadharani na kuungama dhambi zao…Hakukuwa na mkanganyiko. Kutaniko lote likaunganika kwa maombi…Zote tunahitaji kwenda katika mikutano kwa maombi, na, lo, kuna furaha na utukufu katika maombi!...Jambo la pekee tulilolifanya ni kupiga magoti na kuinamisha vichwa vyetu kuisikiliza sauti ya Mungu ikisema, ‘Nyamazeni na kujua kuwa mimi ni Mungu.’ Sasa tumejifunza kwamba ‘Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.’
     Makutano makubwa, zaidi ya watu 700, walisongea na kujazana mbele kuungama dhambi zao…Ilikuwa vingumu kuitamatiza mikutano. Kila mkutano ulidumu saa tatu. Kwa kweli, kila mkutano ulidumu siku nzima …Ujumbe mfupi ulitolewa na Goforth kuanzia hapo na kuendelea kuwa bora kwa kila aliyesikia. Hawa walikuwa Wapresbiteri madhubuti, waliothibitiwa kwa kawaida, wakimlilia Mungu awahurumie… Mhubiri mmoja hodari Mpresbiteri alionekana baadaye akiwa peke yake katika chumba chake, akilia akiwa na maumivu mazito katika nafsi yake.” Bi. Goforth alisema, “Maombi hayo – yalikuwa ya uwazi na unyenyekevu, na uhakika! Lilikuwa jambo la kuvutia kuwa katika mazingira kama hayo!”
      “Wamisionari weupe waliudhuria pamoja na ndugu zao wa Kichina wakiziungama dhambi zao na makosa. Ulikuwa wakati wa watu wote kuja pamoja – Wachina kwa Wachina, Wamisionari kwa Wachina, na haya yalitendeka kwa sababu walikuwa na umoja katika Kristo. Na Kristo alisema kwetu sisi zote, ‘Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.’

Tulikuwa na mikutano katika kanisa letu la awali iliyoonekana kwa nje kuwa kama mikutano ya Goforth nchini China. Nimesema “kwa nje” makusudi. Lakini wengi wa “viongozi” katika kanisa letu walisema uwongo kwa Mungu walipoungama dhambi zao. Hivyo, kama alivyosema Dkt. Tozer, walitenda dhambi aina mbili – dhambi ya kusema uwongo, na dhambi ya kusema uwongo kwa jina la Mungu! Kreighton alimwambia uwongo Dkt. Cagan aliposema hakuhitaji “kuhubiri” ili “aridhike.” Hivyo mtu huyu mdogo mwenye huzuni akawa kama Yuda, aliyemsaliti Kristo, na si kama Petro aliyetubu kwa dhati.

Uamsho halisi chini ya Yonathani Goforth ulikuwa kama uamsho halisi niliouona mimi mwenyewe chini ya Dkt. Timotheo Lin, katika Kanisa la Kibaptisti la Wachina mwisho wa miaka ya 1960, “mahali ambapo hakukutiliwa mkazo wa karama za Roho” –ila tu toba ya dhati na maombi. La kusikitisha ni kwamba, ninavyoona mimi, ni kwamba wakati huo “masadikisho na toba” ilikuwa mihemuko tu – lakini hazikuwa za dhati. Bado inanishangaza kuwa watu kama Kreighton na Griffith walionekana kuwa walidhani wanaweza kumdanganya Mungu!!! Ni upovu kiasi gani huu!!!

Nilipokuwa nikiandika mahubiri haya katika bafu yetu siku chache zilizopita, nilikuwa nimeketi mwisho wa beseni ya kuogea. Nilipokuwa naendelea kukaa mahali pale nilianguka katika beseni ya kuogea, kichwa changu kikagonga sehemu ya chini. Nikawa nimelala pale miguu yangu ikiwa imeelekea juu. Nilijaribu kujisaidia nigeuke nikae vizuri, lakini singeweza. Nilipokuwa nimelala pale, nikiwa nimekwama katika ile beseni, nilifikiria shingo yangu imefunjika. Lakini niliweza kuchezesha vidole vyangu, hivyo nikajua sijavunjika uti wa mgongo.

Nilipokuwa pale katika hali hiyo ya kutisha, Shetani aliniambia kwamba hatutawahi kuwa na uamsho wa kweli. Ndipo wakati huo Mungu akanionyesha uamsho mkuu katika historia ulikuja baada ya watu kama Wesley, Marie Monsen, na Yonathani Goforth, na wengine kama Yohana Sung, walipopitia hali ya majaribia makubwa, kama Yona katika tumbo la samaki mkubwa, kabla ya Mungu kuwaamini na uamsho wa namna hiyo. Tunaweza kuwa na uamsho wa kweli? Pengine. Lakini lazima tuwe watu wa kweli hakika, au Mungu hataachilia uamsho wa kweli ambao wengine wetu tumekuwa tukiuombea miaka hii yote!

Kama Yona, Mchungaji Richard Wurmbrand alikuwa ndani ya tumbo la samaki kwa miaka 14 katika gereza la Wakomunisti. Miaka mitatu kati ya hiyo miaka 14 alikuwa amefungiwa mahali akiwa peke yake, hakuwa anamuona mtu yeyote ila tu Wakomunisti waliokuwa wakimtesa. Kwa nini Mungu alikubali Wurmbrand apitie mambo haya yote? Ukikisoma kitabu chake utaona kwamba Mungu alitumia seli kumfundisha kuwa mtu aliye na upendo wa kweli. Sijawahi kutana na mtu aliye wa kweli kama Richard Wurmbrand. Alijifunza hakiwa katika chumba alipofungiwa peke yake kuyaongea maneno ya kweli kwa ulimwengu wote baada ya kuachiliwa kutoka gerezani. Watu wadogo kama Kreighton na Griffith hawakuwa watu waaminifu. Hata walimdanganya Mungu. Hata “waliungama” dhambi jambo ambalo alikuwa na maana yeyote kwao.

Ni rahisi vyakutosha kuona kwamba Yohona Wesley, Marie Monsen, na Yonathani Goforth walikuwa watu makinifu, na hawakuwa wandanganyifu. Hivyo divyo alivyokuwa Yona!

Dkt. A. W. Tozer alisema, “Ikiwa tunaweza kuwa wajinga vyakutosha kufanya hivyo, tunaweza kaa mwaka mzima kwa ubatili tukimwomba Mungu kuleta uamsho, wakati ambapo tunapuuza matakwa yake kwa upofu na kuendelea kuvunja sharia zake. Au tunaweza sasa anza kutii na kujifunza baraka za utiifu. Neno la Mungu liko mbele zetu. Tunahitaji tu kulisoma na kutenda sawasawa na maandiko na uamsho…utakuja tu kawaida kama mavuno yanavyokuja baada ya kupanda na kupalilia” (“Ni vipi kuhusu uamsho? – Sehemu ya Kwanza”). Mungu anatafuta uaminifu!


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.


MWONGOZO WA

YONA – NABII WA UAMSHO!

JONAH – THE PROPHET OF REVIVAL!

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

“Basi neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu” (Yona 1:1, 2).

(II Wafalme 14:25; Mathayo 12:39-41; Luka 11:29-30)

I.   Kwanza, Kuitwa kwa Yona, Yona 1:1, 2, 3; Wafilipi 4:13; Mathayo 10:34-39.

II.  Pili, Taabu ya Yona, Yona 1:3-4, 12; 1:17-2:1; 1:17; 2:9b.