Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.Wimbo Ulioimbwa Kabla ya Mahubiri: “Mimi ni Askari wa Msalaba?”
(na Dkt. Isaka Watts, 1674-1748).


NIMESULUBIWA PAMOJA NA KRISTO!

CRUCIFIED WITH CHRIST!
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.,
Mchungaji Mstaafu

Mahubiri yaliyohubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Alasiri, Mai 17, 2020
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Afternoon, May 17, 2020

“Nimesulubiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi, bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu” (Wagalatia 2:20).


Inamaanisha nini unaposema “nimesulubiwa pamoja na Kristo”? Nina amini inamaanisha kwamba lazima nafsi zetu zipitie usiku wa giza. lazima tuhisi dhambi zetu, tuhisi mjeledi wa sheria, tuhisi msumari, tufe pamoja na Kristo – tuunganishwe na Kristo katika kifo, pamoja na kukufuka kwake.

Mchungaji Wurmbrand alipitia katika hali ya kusulubiwa pamoja na Kristo alipokuwa jela, amefungwa peke yake. Katika kitabu chake, Katika chumba cha chini cha Mungu, alieleza jinsi alivyosulubiwa pamoja na Kristo. Wurmbrand alisema,

     Nilifungiwa katika seli peke yangu kwa miaka miwili. Sikuwa na chochote cha kusoma wala mahali pa kuandikia; Mawazo yangu tu ndio yalikuwa pamoja nami, na sikuwa mtu wa kutafakari, mbali nafsi iliyojua kutulia.
     Nilimwamini Mungu? Basi jaribu lilikuja. Nilikuwa peke yangu. Hakukuwa na mshahara ambao ningepokea, hakukua na wazo muhimu la kuzingatia. Mungu unipa mateso tu – ningeendelea kumpenda?
     Polepole nikajifunza kwamba katika mti wa utulivu kunalo tunda la amani…nilipata kwamba hata hapa [mahali nilipo peke yangu] mawazo yangu yalimwelekea Mungu, na kwamba ningeweza kuendelea katika maombi, mozoezi ya kiroho na sifa usiku baada ya mwingine. Nilijua sasa sikuwa najifanya. NILIAMINI! (Katika Chumba cha Chini cha Mungu, uk. 120).

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

Inamaanisha nini unaposema “nimesulubiwa pamoja na Kristo”? Inamaanisha kwamba lazima nafsi zetu zipitie usiku wa giza. lazima tuhisi dhambi zetu, tuhisi mjeledi wa sheria, tuhisi msumari, tufe pamoja na Kristo – tuunganishwe na Kristo katika kifo, pamoja na kukufuka kwake.

Mara nyingi mtu aliye mkaidi kama mimi ni lazima apitie hali hii mara nyingi kabla ya kujisalimisha na “kusulubiwa pamoja na Kristo.” kikamilifu Bado niko katika mchakato wa kujifunza huu ukweli, ingawa sasa niko katika mwaka wa themanini wa maisha yangu.

Mara ya kwanza nilianza kujifunza huu ukweli nilipokuwa katika kanisa la Kichina, mahali ambapo “sikuwa mwenyeji” kwa miongo mingi. Nilitaka kuliacha, lakini Mungu hakutaka niliache. Aliniambia wazi wazi nisiliache kupitia Waebrania 10:25 na mahali kwingineko katika Biblia. Hivyo nikaanza “kusulubiwa pamoja na Kristo.”

Wakati mwingine nilipojaribiwa ilikuwa katika seminari ya dhehebu la Southern Baptist katika Kaunti ya Marin. Nilichukia mahali hapo kwa sababu kulikuwa na maprofesa huria ambao karibu wote hawakuwa wameongoka na waliirarua Biblia vipande vipande karibu kila darasa. Nilichukia kuwa pale,lakini mara nyingine, Mungu akaniambia nikae, haijalishi nilivyohisi. Baada ya usiku wa manane, katika chumba changu kule seminari, Mungu akaniita wakati huo wa usiku. Kwa “sauti ndogo na nyororo” Mungu akaniambia, “Miaka mingi kutoka sasa utafikiria kuhusu usiku huu wa leo na utakumbuka ya kwamba nilikwambia kazi yako kuu itaanza utakapokuwa mzee…Sasa utajifunza kutoogopa. Nitakuwa pamoja nawe…Usiposema haya maneno hakuna atakayeyasema, na maneno haya yanahitaji kunenwa sana – na wengine wanaogopa kuyasema, hivyo usipoyasema hakuna atakayeyasema, au hawatayasema vyema.”

Kulikuwa na profesa wangu wa somo la kujifundisha kuhubiri Dkt. Gordon Green, aliyeniambia, “Hymers, wewe ni mhubiri mzuri sana, mmoja wa walio bora. Lakini…hautawahi kupata kanisa la kuchunga la Southern Baptist ikiwa hautakomo kuleta shinda.” Nilimtazama machoni, “Ikiwa hiyo ndiyo inavyogharamu sitaki hiyo nafasi.” Sikuwa na chochote cha kupoteza (Dhidi ya woga wote, uk. 86).

Ndipo nikaja huku Los Angeles nikalianzisha hili kanisa. Baadaye Kreighton alilipasua hili kanisa kwa sababu “hakukubaliana” nami. Ni nini hakukubaliana nacho? Hakukubaliana na msimamo wangu mkali katika maswala mbali mbali, hicho ndicho hakukubaliana nacho! Mtu mpole na mwenya hofu, aliyeogopa kusimama na ukweli wa Mungu! Kwaheri, mwenye hofu!

Sasa, katika mwaka wangu wa themanini, nimekuja kujua ya kwamba Mungu amekuwa akiniandaa muda huo wote kuwa sauti ya kinabii katika ukengeufu wa nyakati za mwisho(II Wathesalonike 2:3).

Wakati ambapo wengine wanasema utanyakuliwa, nasema ya kwamba utapitia sehemu kubwa ya kipindi cha dhiki kuu, kama anavyosema Marvin J. Rosenthal katika Unyakuzi wa Kanisa kabla ya dhiki. Wakati wengine, kama Kreighton, wanataka kuwavuta kuingia madhehebu Mapya ya Kiinjilsti, ninasema, “Simama na Kristo – haijalishi kitakachotendeka.”

Simchukii Yohana Samweli. Nilikuja kufahamu kwamba si mkakamafu kiasi kwamba anaweza kuwa sauti ya unabii nyakati hizi za mwisho. Aliogopa kwamba “angeshindwa na kusimia”. Hii ni kwa sababu Yohana Samweli bado “hajasulubiwa pamoja na Kristo.” “Nimeshindwa na nimesimia” mara nyingi kwamba hainistui tena!

Dkt Cagan kila mara uniambia anapenda ninayoyahubiri kuhusu kuwa na nguvu nyakati hizi za mwisho. Hilo ni himizo linalonitia nguvu! Ukiwa “umesulubiwa pamoja na Kristo” utaweza kukaa nami pamoja na Dkt Cagan katika siku hizi za ukengeufu (II Wathesalonike 2:3), na utakuwa mashahidi aliyeheshimika – au angalau muungamaji aliyeheshimika, kama Mchungajir Wurmbrand!

“Nimesulubiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi, bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu” (Wagalatia 2:20).

Dkt. Timotheo Lin, katika kitabu chake Ufalme wa Munggu, alisema, “Leo washirika wengi kanisani hawawezi kusikia sauti ya Mungu kwa sababu wanapenda ubinafsi…Mioyo yao imekuwa miguma, na hivyo wanavyo endelea kujifundisha ndivyo wanavyoendelea kusikia kwa uchache. Wengi wanafikiri wanajua kila kitu, wakati ambapo kwa kweli hawajui ukweli mwingi wa kimsingi. Wengi wao hawawezi hata kusema kusundi lao katika maisha ni nini!” Dkt. A. W. Tozer alitoa mfano huu.

     Muulize mwanafunzi mchanga wa chuo kikuu, “Bob, kwa nini uko hapa?”
      “Nataka kuoa; ningependa kupata pesa; na ningependa kusafiri.”
      “Lakini Bob, haya ni mabo ya muda mfupi. Utayafanya alafu utazeeka na utakufa. Sababu kuu ya maisha yako ni ipi?”
     Basi Bob anaweza kusema, “Sijui kama nina kusudi lolote katika maisha.”
     Watu wengi hawajui kusudi lao katika maisha (“Kusudi la Mwanadamu,” uk. 27).

Mkristo anaweza kusema kusudi lake katika maisha ni kwenda Mbinguni. Lakini Dkt. Lin alisema mara nyingi kwamba hakuna aya katika Maandiko inayosema kwenda Mbinguni ndilo kusudi katika maisha yako!

Kukuonyesha kusudi la maisha yako linavyostahili kuwa, angalia II Timotheo 2:12. Soma sehemu ya kwanza ya aya ya 12,

“Kama tukivumilia, tutatawala pamoja naye pia.…”

“Kuvumilia” inamaanisha “kustahimili.” Ufunuo 20:6 inasema, “Watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, na watatawala pamoja naye kwa miaka 1,000.” Neno “Kuvumilia” inamaanisha “kustahimili.”. Muktadha wa II Timotheo 2:12 unapatikana katika II Timotheo 2:1-11. Dokezo katika Biblia ya Scofield kuhusu aya ya kwanza inasema vyema, “Mapito ya ‘askari mwema’ katika nyakati za ukengeufu.” Huku kutawala pamoja na Kristo kumeonyeshwa wazi katika methali ya fungu la fedha, katika Luka 19:11-27. Wanaojiandaa kutawala pamoja na Kristo watapewa “madaraka juu ya miji kumi” (aya 17) au “zaidi ya miji mitano” (aya 19). Dkt. Lin alisema hili litakuwa jambo halisi. Watakaovumilia katika maisha haya watatawala pamoja na Kristo katika Ufalme Wake unaokuja! Neno “Kuvumilia” inamaanisha “kustahimili.”

Hivyo ni nini tutavumilia? Tutavumilia kwa kutoipenda dunia,

“Msiipende dunia wala mambo yaliyomo duniani. Kama mtu akiipenda dunia, hawezi kumpenda Baba. 16 Maana vitu vyote vilivyomo duniani, yaani, tamaa za mwili, tamaa ya vitu vinavyoonekana kwa macho, na kiburi kiletwacho na mali, vyote hivi havitoki kwa Baba bali hutoka ulimwenguni. Nayo dunia inapita na tamaa zake zote zinapita, lakini mtu anayetimiza mapenzi ya Mungu huishi milele.” (I Yohana 2:15-17).

Tunavumilia kwa kutoungana na mgawanyiko wa kanisa,

“Watu hao walitoka kati yetu, lakini hawakuwa wa kundi letu. Kama wangekuwa wa kundi letu, wangeende lea kuishi pamoja nasi; lakini waliondoka ili iwe wazi kuwa hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kundi letu” (I Yohana 2:19).

Tunavumilia kwa kukataa kuwafuata walimu wa uwongo,

“Wapendwa, msiamini kila roho bali zipimeni roho zote kwa makini muone kama zinatoka kwa Mungu. Kwa maana manabii wengi wa uongo wametokea duniani” (I Yohana 4:1).

Tunavumilia kwa kutenda mambo yampendezaye Mungu,

“Nasi tunapokea kutoka kwake lolote tuombalo kwa kuwa tunatii amri zake na kufanya yampendezayo” (I Yohana 3:22).

Tunavumilia kwa kutii amri ya Mungu,

“Nasi tunapokea kutoka kwake lolote tuombalo kwa kuwa tunatii amri zake na kufanya yampendezayo. Na amri yake ndio hii: tuliamini jina la Mwanae Yesu Kristo na kupendana, kama alivyotu agiza” (I Yohana 3:22, 23).

Tunavumilia kwa kuwatii walimu wetu,

“Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Tafakarini jinsi walivyoishi na matokeo ya mwenendo wao, mkaige imani yao.Watiini viongozi wenu na kufanya wanavyowaagiza. Wao wanachunga roho zenu, kama watu ambao watatoa ripoti ya huduma yao. Watiini kusudi wafanye kazi yao kwa furaha, na wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu” (Waebrania 13:7, 17).

Tunavumilia kwa “kujitoa kwa kuzidi kufanya kazi ya Bwana” – kusimama imara!

“Kwa hiyo ndugu zangu, simameni imara. Msitikisike. Mzidi sana kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, juhudi yenu si bure katika Bwana” (I Wakorintho 15:58).

Kwa kuvumilia mambo haya, Mungu utufundisha kuwa wanafunzi, watakaotawala na Kristo katika Ufalme Wake unaokuja.

“Mshindi nitamjalia kuketi pamoja nami juu ya kiti changu cha enzi, kama vile mimi mwenyewe nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu juu ya kiti chake cha enzi. Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!” (Ufunuo 3:21, 22).

Mchungaji Wang Ming Dao (1900-1991) alifungwa jela miaka 22 katika nchi ya China iliyo ya kikomunisti, kwa sababu ya imani yake Alisema,

“Watu wengine uniuliza ni njia gani kanisa linastahili kwenda. Nami hujibu bila kusita, njia ya Mitume…kuwa waaminifu hadi kifo.” Alihubiri katika ibada ya mazishi ya Dkt. John Sung. Alipoteza meno yake yote, uwezo wake wa kusikia na pia kuona akiwa jela. Baada ya kufunguliwa kutoka jela, yeye na mke wake walifundisha vikundi vya Wakristo katika chumba chao hadi kifo chake mwaka wa 1991.

Tafadhali simama na uimbe wimbo wetu,

Mimi ni askari wa msalaba, Mfuasi wa Mwana Kondoo;
Na nitaogopa kujitambulisha na kusudi Lake, au kuonea haya jina Lake?

Lazima nibebwe angani na vitanda vya maua ya raha,
Wengine wakipiga vita kushinda tuzo, Na kupitia katika bahari ya damu?

Kwani hakuna maadui ninaokumbana nao? Lazima niyakabili mafuriko?
Dunia hii chungu ni rafika ya neema, Kunisaidia kumwendea Mungu?

Hakika lazima nipige vita, ikiwa nitatawala; Niongeze ujasiri, Bwana!
Nitatoa jasho, nivumilie uchungu, Nikisaidiwa na Neno.
   (“Mimi ni Askari wa Msalaba?” na Dkt. Isaka Watts, 1674-1748).


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.