Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




MWITO WETU KUWA WANAMISHENI!

OUR CALL TO BE MISSIONARIES!
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.,
Mchungaji Mstaafu

Mahubiri yaliyo hubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Alasiri, Machi 8, 2020
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Evening, March 8, 2020


Isaya alikuwa, kama ninavyoona, nabii mkubwa kuliko wote. Lakini ni vipi Isaya akawa mtu wa Mungu wa namna hii? Katika sura ya sita ya Isaya, tunalo jibu.

“Mnamo mwaka aliofariki mfalme Uzia, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi kilicho juu na cha fahari. Pindo la vazi lake lilienea hekaluni mote” (Isaya 6:1).

Isaya alisikia maserafi wakipaza sauti, “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Dunia yote imejaa utukufu wake” (Isaya 6:3).

Isaya aliyekuwa mchanga alimpenda Mfalme Uzia, aliyekuwa Mfalme mwema na mwenye heshima. Lakini sasa mfalme huyu aliyekuwa mwema alifariki. Ni jambo gani lingemtendekea Isaya sasa kwamba mfalme huyu mwema alikuwa amefariki? Nafikiri mtu huyu mchanga alihisi kama wengine wenu. Mnahusunika kwamba kanisa letu limeisha. Lakini Mungu hakuwa amemalizana na Isaya.

Maono haya ya Mungu yalikuwa yamezama katika nafsi yake. Isaya hakupatwa na husuni ambayo haikuwa na tumaini. Badala yake, maono ya Mungu yalimpata kwa njia tofauti. Alisema,

“Basi, mimi nikasema, “Ole wangu! Mimi nimeangamia, maana, midomo yangu ni najisi, na watu ninaoishi nao ni najisi kama mimi. Hata hivyo, kwa macho yangu mwenyewe, nimemwona Mfalme, Mwenyezi-Mungu wa majeshi” (Isaya 6:5).

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

Haya yalikuwa mafanikio ya kiroho ya Isaya aliyekuwa mchanga! Haya ni mafanikio ya kiroho ambayo hata wewe unaweza kuyapata. Lakini itakubidi umtafute Mungu kuliko mambo mengine yote! Dkt. A. W. Tozer alisema, “Hawakuondoka kanisani kwa sababu hawakumtaka Mungu – lakini ni kwa sababu walikipata kitu ambacho walikihitaji kuliko Mungu…wakati hali yao ya asili iliwachochea walimwonyesha Mungu mgongo na wakaliacha kanisa. Waliingia katika uhusiano na wanawake wachanga au wanaume wasiomjua Mungu. Waliingia katia mahusiano ya kiulimwengu. Walijihuzisha na kazi ambazo hasiwapi nafasi ya kumpendeza au kumtukuza Mungu. Walirudia mambo ya ulimwenguni. Waliamua kupata walichokipenda zaidi…sitaki kuwandanganya na kuwapoteza kwa kufundisha kwamba unaweza kuwa Mkristo na kuupende ulimwengu huu wa sasa. Ndio, unaweza kuwa mnafiki na uupende ulimwengu. Unaweza kuwa Mchungaji aliyedanganyika na kuupenda ulimwengu. Unaweza kuwa na imani legefu ya kiinjilsti cha siku hizi na kuupenda ulimwengu. Lakini hauwezi kuwa Mkristo halisi wa Biblia na uupende ulimwengu. Linaweza kuwa jambo la kunisikitisha kwamba nitashikilia kanuni hii peke yangu lakini sitakundanganya kuhusu jambo hili” (Mimbari ya Tozer).

Tena, Dkt. Tozer alisema, “Kwa maoni yangu, hitaji lililokuu siku ya leo ni kwamba huyo mwenye moyo mwepesi, mwenye imani ya kiinjilisti dhaifu apatwe na maono ya Mungu aketiye katika kiti cha enzi kilicho juu na cha fahari ambaye pindo la vazi lake limeenea hekaluni mote.” Bila maono ya Mungu ya namna hiyo “tutabaki tu na mipango yetu, na tutalazimika kuleta ndani ya kanisa shughuli zisizo na maana za kushikilia watu kanisani…Tumeogopa sana hali ya kuwa katika uchache hivyo kwamba tumefungua milango ulimwengu ukaingia kanisani. Hili husababish janga la kiroho… Imani ya kiinjilisti ina upungufu katika mtazamo wao kumhusu Mungu na katika mtazamo wao kuhusu ulimwengu na dhambi” (Kuegemea upepo).

Angalia mstari 5,

“Basi, mimi nikasema, “Ole wangu! Mimi nimeangamia, maana, midomo yangu ni najisi, na watu ninaoishi nao ni najisi kama mimi. Hata hivyo, kwa macho yangu mwenyewe, nimemwona Mfalme, Mwenyezi-Mungu wa majeshi” (Isaya 6:5).

Ni wakati ule tu Isaya mchanga alipotakazwa na moto wa Mungu ndipo aliambiwa “na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa.” (Isaya 6:7).

Sasa angalia mstari wa 8. “Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.” (Isaya 6:8).

Wakati kanisa lilipasuka nilihisi kwa hakika nitapoteza bidii yangu ya uinjlisti. Niliamua kuwa na muda kila usiku na vijana watatu waliokata tamaa kumhusu Kristo – Mchungaji Richard Wurmbrand, Yohana Wesley, na mmishonari mwanzilishi wa mwisho kwa China, Yonathani Goforth. Lilikuwa waso lenye busara. Nilifanya bafu iliyokuwa ndogo, karibu na chumba chetu cha kulala, mahali pangu pa kuombea na kuwa na ushirika na hawa watu mashuhuri wa Mungu. Kutoka kwa Wurmbrand nilijifunza kuwa thabiti. Kutoka kwa Yohana Westly nilijifunza kuendelea kutoka kwa jaribio moja hadi jingine. Lakini kutoka kwa Goforth na mke wake Rosalind, Nilijifunza kwamba ni lazima twende mbele katika magoti tukiomba. Hudson Taylor aliandika barua iliomchochea Goforth na mke wake. Hudson Taylor alisema, “Sisi kama wanamisheni tulijaribu kwa miaka miwili kuingia katika mkoa wa China wa Honan, na tulifaulu hivi karibuni. Ndugu, ungeweza kuingia katika ule mkoa, ni lazima uende kwa magoti.” Maneno hayo ya Hudson Taylor yakawa ndio kauli mbiu katika misheni ya Goforth kule kasikasini mwa Honan.

Basi mtoto wao akafariki. Goforth akaandika, “Gertrude amefariki. Tumepata hasara mbaya. Chini ya muda wa majuma mawili yaliopita alikuwa mzima, lakini Julai 24 alifariki, siku sita baada ya kupatwa na ugonjwa wa kuhara. Ilinibidi kusafirisha mwili wake kwa mkokoteni maili hamsini…Na ilipokaribia jioni tulimpumzisha mtoto wetu mpendwa huko.” Wasichana wawili wachanga wa Kichina walikuja kila asubuhi kuweka maua mabichi katika lile kaburi la mtoto wetu mpendwa.

Baada ya kifo cha Gertrude, mvulana mzuri alizaliwa na Bi. Goforth. Walimpa jina “Donald mchanga.” Alianguka akagongwa kichwa chake kidogo. Na polepole alipoteza uwezo wake wa kutumia miguu yake na mikono yake. Katika kilele cha joto katika majira ya joto, mnamo Julai 25, alipokuwa na umri wa miezi kumi na tisa, Donald mchanga akafariki. Kwa mara nyingine Goforth aliupeleka mwili wa mvulana wake mdogo kwa mkokoteni maili hamsini. Donald mchanga alizikwa katika kaburi kado na mwili wa dadake mdogo, Gertrude. Mara moja baada ya kurudi kwake, Goforth na mke wake mpendwa walijiandaa kwenda katika makao yao mapya kule kasikasini mwa Honan. Mtoto wao mchanga wa miezi mitano alienda pamoja nao.

Halafu Yonathani Goforth akawa mgonjwa sana akiugua homa ya matumbo. Maisha yake yakaning’inia kati ya uhai na kifo. Januari 3, mtoto Florence akazaliwa. Kulikuwa na joto sana msimu ule wa joto na mtoto ndogo Paulo alikuwa karibu kufa kutokana na joto jingi, lakini aliweza kuishi joto ilipopungua.

Shinda nyingi za kutisha na majaribu yakafuatia. Mtoto wao wa kwanza akafa msimu wa masika. Watoto wao wengine wakafa kwa malaria na utando wa ubongo. Baadaye Goforth na mkewe walilazimika kukimbia uasi wa kikundi kilichoitwa Boxer. Waliepuka kuuawa kimuujiza.

Bi. Rosalind Goforth akawa kiziwi. Mumewe akawa masikio yake. Goforth alipopotea macho kabisa, mkewe akawa macho yake. Alifariki akiwa usingizini mkewe alipokuwa bafu. Katika masishi yake, kijana wake Paulo alisema haya, “Kwangu mimi babangu alikuwa mtu mashuhuri.” Bintiye Ruth alikuwa mmishonari kule Vietnam. Ruth alimwandikia mamake hivi, “Ninaweza tu kufikiria kuhusu utukufu kama mapito ya Baba...Mungu amempandisha katika kiwango kikubwa cha utumishi.”

Kitabu, Goforth wa China, kiliandikwa na mkewe Rosalind baada ya kifo chake. Rosalid Goforh alikuwa mmishonari wa kweli na waajabu!

Alikutana naye mara ya kwanza alipoiangalia Biblia yake, “Nilipata Biblia yake ilikuwa imechanika kabisa, iliyowekwa alama kutoka jalada hadi jalada.” Rosalind alisema, “Huyo ndiye mwanamume ambaye ningependa anioe.” Msimu huo wa vuli aliniuliza, “Utaungana nami katika maisha yako kwa sababu ya China?” Jibu lake lilikuwa “ndio.” Siku chache baadaye alimwambia, “Utaniahidi kwamba utanikubalia kumpa kipaumbele Bwana na kasi yake, hata mbele yako?” Alimjibu, “Ndio, nitafanya hivyo kila wakati.” Hakujua hiyo ahadi itakavyomgarimu!

“Kisha nikamsikia Mwenyezi-Mungu akisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekuwa mjumbe wetu?” Nami nikajibu, “Niko hapa! Nitume mimi” (Isaya 6:8).

Kanisa letu limepoteza watu ambao hawakuwa tayari kuwa wanamisheni. Ni ombi langu kwamba kila mtu aliye hapa alasiri ya leo atakuwa mmishonari. Tutakuwa na wakati mgumu kukusanya pesa za kutosha kuiwezesha kazi yetu ya umishonari wa mtandao kuendelea. Wewe na mimi tunaweza kuwa wanamishonari ulimwenguni kote kwa (1) Kuwahubiria watu waokoke; (2) Kuombea huduma yetu ya umishonari katika ulimwengu wote; (3) Kutoa pesa za kutosha kusaidia kitengo chetu cha umishonari wa mtandao kutuma mahubiri yetu, pamoja na hii, kusaidia wamishonari katika Ulimwengu wa Tatu kuhubiri Habari Njema. Mchungaji mmoja mmishonari alisema hivi juu ya nafasi zetu leo “Tunastahili kuwa Wakristo wa Ulimwengu wote tukiwa na umishonari wa Ulimwengu wote kwa sababu Mungu wetu ni wa Ulimwengu wote.” Utajibu pamoja na Rosalind Goforth “Ndio, Nitafanya hivyo, kila wakati”?

Jaza maono yangu, Mwokozi, naomba, Naomba nimwone Yesu pekee leo;
   Ingawa nipitapo katika bonde wewe uniongoza, Utukufu wako usiochujukaa hunizunguka.
Jaza maono yangu, Mwokozi Mungu, Hata roho yangu itakapoangaza kwa utukufu wako.
   Jaza maono yangu, kwamba wote waone Mfano wako Mtakatifu ukionyeshwa ndani yangu.

Jaza maono yangu, niyatamaniyo Yaweke kwa utukufu Wako; nipe msukumo katika nafsi yangu,
   Kupitia ukamilifu Wako, Upendo wako mtakatifu, Gharikisha njia yangu na mwanga kutoka juu.
Jaza maono yangu, Mwokozi Mungu, Hata roho yangu itakapoangaza kwa utukufu wako.
   Jaza maono yangu, kwamba wote waone mfano Wako Mtakatifu ukionyeshwa ndani yangu.

Jaza maono yangu, lisipatikane tone la dhambi kufunika mwanga ulio ndani.
   Niuone tu uso Wako wa baraka, Nikijisherehesha nafsi yangu katika neema Yako ya milele.
Jaza maono yangu, Mwokozi Mungu, Hata roho yangu itakapoangaza kwa utukufu wako.
   Jaza maono yangu, kwamba wote waone Mfano Wako Mtakatifu ukionyeshwa ndani yangu.
(“Jaza Maono Yangu” na Avis Burgeson Christiansen, 1895-1985).


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.