Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.
MKRISTO WA UWONGO AMEGUNDULIWA!

THE FALSE CHRISTIAN DISCOVERED!
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Asubuhi ya, Julai 7, 2019
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Morning, July 7, 2019

“Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu” (Mathayo 7:21-23).


Nitachukua andiko langu kutoka mstari wa 21,

“Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21).

Mahubiri haya sijayatoa kwa mawazo yangu. Chanzo chake ni maneno ya Kristo Mwenyewe, na maelezo ya Mtawa Mathayo Mead (1629-1699). Mfafanusi wa Biblia Yohana MacArthur barabara alikubaliana na kitabu cha Mead, Aliyekaribia kuwa Mkristo amegunduliwa. Pia mimi nakubaliana nacho.

“Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21).

Mtu anaweza kuwa na ufahamu mwingi, ufahamu mwingi kumhusu Kristo, na bado awe amepotea. Mafarisayo walikuwa na ufahamu mwingi, na bado walikuwa kizazi cha wanafiki. Lo! wengi wameenda Jehanamu na ufahamu mwingi! Kufahamu ili upate tu kufahamu zaidi ni jambo linalotokana na upekuzi. Kufahamu ili ujivunie unayoyafahamu ni ubatili. Kufahamu na kutenda unayoyafahamu ndio Ukristo wa kweli!

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

Mtu anaweza kuwa na karama kuu za kiroho na bado awe amepotea. Kipawa cha maombi ni cha kiroho. Mtu anaweza kuomba kwa njia ya kupendeza na bado awe amepotea. Mtu anaweza kuwa na kipawa cha kuhubiri na awe hajaokoka. Yuda alikuwa mhubiri mashuhuri. Yuda alisema, “Bwana, Bwana, tumehubiri kwa Jina lako, na kwa Jina lako tumetoa pepo.” Anaweza kuomba zaidi, na kuhubiri zaidi kumliko Mkristo wa kweli na bado awe si Mkristo wa kweli. Mtu anaweza kuwasaidia wengine kupitia maombi yake na mahubiri yake, na bado asisaidike yeye mwenyewe.

Uweza wa kuhubiri na kuomba hautegemei mamlaka ya mhubiri, lakini unategemea mamlaka ya Mungu anaye bariki maombi na mahubiri. Mtu anaweza kuongoka kupitia mahubiri yake, na bado mhubiri mwenyewe atupwe Jehanamu! Pendleton alimhubiria Sanders siku ya Malkia Maria ili asimame kwa sababu ya injili aliyoihubiri, na bado baadaye akawa mwasi aliyeenda Jehanamu! Nimewajua vijana wengi waliokuwa wahubiri hodari, lakini baadaye waligunduliwa walikuwa wanafiki! Mtu anaweza kuhubiri kama mmoja wa Mitume na kuomba kama malaika, na bado awe na moyo wa pepo! Mtu anaweza kuwa na vipawa vikuu na bado yeye mwenyewe awe mtu aliyepotea. Askofu mmoja mashuhuru alisema, “Maskini, watu wasio na elimu uenda mbinguni, mbali sisi, pamoja na masomo yetu yote huanguka Jehanamu.” Mtu anaweza kuwa na vipawa vikuu, na bado awe mtu tu aliyepotea. Wakia moja ya neema ya kweli ni bora zaidi kuliko pauni kumi za vipawa. Yuda alimfuata Kristo! alihubiri injili ya Kristo, alitoa pepo, katika jina la Kristo, alikula na akanywa katika ile meza moja pamoja na Kristo; bado Yuda alikuwa mnafiki “aliyeenda mahali pake” katika Jehanamu! Anayejifanya kuwa mtakatifu na hatendi utauwa “wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake.”

Mtu anaweza tangaza kwamba yeye ni Mkristo, na bado moyo wake haujawahi kubadilika. Ni mnafiki anayeonekana kuwa Mkristo mzuri, lakini amejawa na kiburi na uasi. Watu wengi wanaonekana kuwa wenye haki, lakini wanavaa haki yao kama barakoa, ili kuficha kiburi na maasi ya mioyo yao. Hilo linamuelezea mtu aliyesomea seminari na kuwekwa wakfu. Lakini moyo wake haukubadilika. Hivyo aliliacha kanisa letu ili kumfuata kidosho aliyepotea. “Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa” (II Timotheo 4:10). Hilo linamuelezea Dkt. Kreighton L. Chan, aliyebainika kuwa mnafiki wakati ambapo kiburi chake na uasi wake ulipoonekana, wakati ambapo barakoa yake ilipopasuka na tukamwona kuwa mnafiki.

“Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukuhubiri kwa Jina lako? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”

Panya na buku wanaweza kuishi katika nyumba moja. Lakini nyumba inapoonekana inaanza kuanguka, wanakimbia kutafuta mahali pengine pa usalama. Siku za furaha katika kanisa huleta wanafiki wengi katika kanisa. Lakini kanisa linapotingika, wanatoroka – kubainisha ya kwamba wao sio Wakristo wa kweli na haijalishi waliyoyasema hapo awali. Hapa kuna baadhi yao.

Mtu mmoja alisema, “Popote atakaponiongoza nitamfuata. Nijapokumbana na taabu au shida Yesu...amenipa uhai. Lisifu jina la thamani la Yesu.” Bado huyu mtu ndiye aliyekuwa wa kwanza kukimbia kutoka kanisani kwetu mgawanyiko ulipoanza.

Msishana Mchina alisema, “Nataka wengine wajue mambo makuu ambayo Mungu amenitendea. Mungu ayatumie maisha yangu kuwa ushuhuda wake.” Lakini alitoroka kanisani hata kabla ya mgawanyiko!

Kijana mwingine Mchina alisema, “Siwezi eleza jinsi ilivyo adhimu kuokolewa na Yesu...nataka wengine wajue mambo makuu ambayo Kristo amenitendea.” Na bado muda mfupi baadaye aliliacha kanisa na akamfuata Chan, na hili likaonyesha kwamba maneno yake hayakumaanisha chochote. Alikuwa mnafiki aliyepotea anayeenda Jehanamu!

Kijana kutoka Vietinamu alisema, “Upendo huu wote Yesu alionao kwa anjili yangu, siwezi kumpendwa vyakutosha. Natoa maisha yangu kwa Yesu aliye Mwokosi wangu.” Mwaka mmoja baadaye alimsaliti Mwokosi, akaliacha kanisa pamoja na muasi Chan.

Kijana mwingine mwanafunzi wa chuo alisema, “Ninamshukuru Mungu kwa kunitakasa kupitia Damu ya thamani ya Yesu Kristo. Bwana Asifiwe!” Maneno hayo yanaonekana mazuri, sivyo? Lakini muda mfupi baada ya kusema hivyo, alirejelea katika dhambi za ulimwengu na akaliacha kanisa letu.

Msishana Mjapani/Mmarekani alisema, “Ushuhuda wangu ni rahisi. Nilimwamini Yesu na aliniokoa” – na alimlipa Yesu kwa kuliacha kanisa na kumfuata muasi Chan!

Mwanamme Mmeksiko alisema, “Nilionyeshwa huruma na Mwokosi aliyenipenda, na hili sitawahi kulisahau” – Lakini muda mfupi baadaye alisahau aliyoyasema na kumkimbilia muasi Chan. Nina picha yake akiwa amesimama pamoja na muasi mnafiki, karibu na muasi Chan.

Mwanamke mchanga kutoka China alisema, “Yesu ananipenda! Sasa nataka kumwimbia Mwokosi wangu, Yesu Kristo!” Yanaonekana maneno mazuri, sivyo? Lakini baada ya muda mfupi alilisaliti kanisa letu na akakimbia pamoja na muasi Chan!

Mtu mmoja aliniambia, “Dkt. Hymers, usiwalete Wachina wengine. Ni wanafiki walio na sura mara-mbili!” Ni ukweli kabisa, isipokuwa waongoke kikamilifu wamepotea kama hawa niliowataja hapa. Yesu alisema, “Hamna budi kuzaliwa mara ya pili” (Yohana 3:7).

“Neema rahisi” na “imani rahisi” ni misemo mipya, lakini “Upingaji wa sheria adilifu katika Biblia” si jambo geni. Martin Luther (1483-1546) ndiye aliyetumia huo msemo. Msemo huu unawazungumzia wote wanaotaka faida za wokovu lakini hawataki kanuni za wokovu (Chapisho la Soli Deo Gloria, jalada la kitabu cha Mathayo Mead Aliyekaribia kuwa Mkristo amegunduliwa, dibaji ya Yohana MacArthur).

Mmoja wa watu wa muasi Chan anasema, “Dkt. Hymers ufikiria hakuna mtu anayeweza kuokoka isipokuwa tu wahudhurie kanisa lake.” Muasi kama huyo ataweza kudanganya kwa njia yoyote ili kufunika upotevu na uovu wa dhambi zake. Sistaajabu kwamba alidanganya namna hiyo, kwa sababu anajua vyema kwamba sikusema hivyo – wala siamini hivyo.

Lakini ninaamini ya kwamba kanisa ni “mwili wa Kristo” (Waefeso 4:12). Wanaoliacha kanisa Lake wanaudhoofisha mwili Wake. Wanaolivamia kanisa Lake, wanauvamia mwili Wake. Wanaolipasua kanisa Lake, wanaupasua mwili Wake. Wale ambao sio washirika wa kanisa Lake, sio washirika wa mwili Wake. Madhehebu mengi mapya ya Kiinjilisti hawatilii maanani Maandiko. Hio ndio sababu wanauasi mwili wa Kristo!

Watu wengine husema huo ni mtazamo wa “kihistoria”. Sijali wanavyouita, huu ndio mwelekeo wa Biblia. Kanisa ni “mwili wa Kristo!”

Ninakuuliza asubuhi ya leo huje kwa Yesu. Amefufuka kutoka kwa wafu. Ameketi katika mkono wa kuume wa Mungu juu Mbinguni. Kuja kwa Yesu. Ondokea ulimwengu na dhambi. Mwamini Yesu na atakutakasa dhambi zote na Damu yake ya thamani! Mwamini Yesu na utakuwa sehemu ya Mwili wake, ambao ni kanisa. Amina.

Ikiwa ungependa kuzungumza nasi kuhusu kumwamini Yesu tafadhali njoo na usimame hapa mbele sasa hivi. Tunapoendelea kuimba wimba nambari 5, “Jinsi Nilivyo,” wewe njoo.

Jinsi nilivyo, bila hoja yoyote, Lakini Damu yako ilimwagika kwa ajili yangu,
Na unanialika nije Kwako, Ee Mwana-Kondoo wa Mungu, Naja! Naja!

Jinsi nilivyo, bila kungojea, Kuiponya nafsi yangu waa la dhambi nyeusi,
Kwako ambaye Damu yako inaweza takasa kila doa, Ee Mwana-Kondoo wa Mungu, Naja! Naja!

Jinsi nilivyo, ingawa mapambano yanipepeta, na mashaka mengi,
Vita na woga ndani, na nje, Ee Mwana-Kondoo wa Mungu, Naja! Naja!
   (“Jinsi Nilivyo” na Charlotte Elliott, 1789-1871, umebadilishwa na Mchungaji).


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.