Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




MACHOZI KATIKA MAOMBI

TEARS IN PRAYER
(Swahili)

na Dkt. Christopher L. Cagan

Mahubiri yaliyohubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Jioni ya, Juni 2, 2019
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Evening, June 2, 2019

“Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu” (Waebrania 5:7).


Somo letu linazungumzia Yesu alipokuwa akiomba katika Bustani ya Gethsemane, usiku ule kabla ya kusulibiwa kwake. Alikuwa na shinikizo kubwa kwa maana alitwikwa dhambi zetu, ili azibebe katika mwili wake kuelekea Msalabani siku iliyofuatia. Injili ya Luka inatuambia,

“Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini” (Luka 22:44).

Kristo aliomba “katika dhiki” usiku huo. Andiko letu linasema alimtolea Mungu “maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi.” Ombi la Yesu lilijaa hisia na tukutiko, kulia sana na machozi. Usiku huu nataka kuzungumzia hisia na tukutiko katika maombi.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

I. Kwanza, sala ya uwongo ikiwa na hisia.

Wapentekoste wengi na Wakarismatiki ufikiria ya kwamba kupiga kelele na kulia, hisia na msisimko ni sehemu muhimu katika sala. Wao ufikiria kwamba kupiga moyowe na kulia ina maana kwamba Roho Mtakatifu anahusika katika ile sala, na ikiwa hakuna kutetemeka na kupiga kelele Roho Mtakatifu hahusiki katika ile sala. Hawasemi hivi tu kwa sala pekee, lakini pia kwa jinsi watu wanavyofanya wanapoimba, wanaposikiliza mahubiri, na wanapofanya mambo mengine yote yanayotendeka kanisani. Lakini wamekosea. Hisia zenyewe hazimaanishi chochote. Inaweza kuondoa maana ya sala. Inaweza kuwa pia ya kipepo.

Hebu nikupe mfano kutoka kwa Biblia wa hisia za uwongo katika sala. Eliya aliwakabili manabii wa Baali. Aliwaambia wachukue siku wapige mayowe kwa Baali, naye atamwomba Mungu wa Israeli. Na Mungu atakayejibu kwa moto atajidhihirisha kuwa Mungu wa kweli. Manabii wa Baali wakawa na mhemko mkali na hisia katika sala yao. Ingeonekana kuwa nzuri katika makanisa mengi siku ya leo! “Wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya.” (Wafalme 18:26). Wakati wa adhuhuri “Wakapiga kelele, wakajikatakata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika.” (I Wafalme 18:28). Lakini “hapakuwa na sauti wala aliyejibu.” (I Wafalme 18:29). Kisha Eliya akasali sala rahisi tu kwa Mungu na Mungu akatuma moto kutoka Mbinguni. Msisimko wa kipepo, kurukaruka, kupiga mayowe na kulia na mengine mengi, hayakuwafaidi manabii wa uwongo. Msisimko wenyewe haumaanishi chochote.

Nimeona hisia zenyewe mara nyingi. Hazikufaidi chochote. Wakati mmoja nilikuwa namshauri msichana katika chumba cha maojiano, nikijaribu kumwongoza kwa Kristo. Aliendelea kulia na kutetemeka. Hakuacha nilipomuuliza aache. Alisema alikuwa analia kwa sababu ya dhambi zake, lakini hakuondoka kutoka kwa hicho kilio kumwelekea Yesu. Hakuelekeza usikivu wake kwa Kristo. Hakuongoka. Baadaye aliliacha kanisa na akajihuzisha na maisha ya dhambi nzito.

Watu wengine wana hisia nyingi. Wanaangua kilio kwa jambo lolote. Namkumbuka msichana mwingine aliyefanya vivyo hivyo. Haikuwa baada ya mahubiri, au aliposhauriwa kuhusu kumwamini Kristo. Ilikuwa kila wakati. Angeanza kutokwa na machozi na kulia. Hangeweza kuyaelekeza mawazo yeke kwa Kristo, au kanisa au Biblia. Siku moja alihisi huzuni. Alifuata hisia zake na akatoka kanisani. Sikuwahi kumwona tena.

Kulia na kupiga kelele hakufanyi jambo lolote kuwa “halisi.” Haifanyi sala kuwa halisi. Kujaribu kujifanya ulie au kupiga kelele hakufaidi chochote. Unaposali, fikiria kuhusu jambo unaloliombea. Unaweza kusali ukitokwa na machozi au unaweza kuwa hautatokwa na machozi. Yesu alionyesha hisia katika Bustani ya Gethsemane. Aliomba kwa “kulia sana na machozi.” Lakini haikuwa kulia tu kwa sababu ya kulia. Machozi yake hayakufanya maombi yake kuwa mazuri. Machozi yake yalitokana na maombi yake. Yalitokana na sala yake. Alimlilia Mungu katika mashaka, katika shinikizo na maumivu, alipokuwa ametwikwa dhambi za kizazi cha binadamu. Kulia kwake kulitokana na kujitolea kwake, kujishughulisha kwake, hitaji lake, mzigo wake na mateso yake. Na hivyo ndivyo ilivyo hata kwako wewe. Usijaribu kulia. Usipange kulia au ujitayarishe kulia. Sali tu. Mungu anaweza kukuongoza ulie, au anaweza kosa kukuongoza katika kulia, lakini kwa njia yoyote katika hizi itakuwa sala halisi.

II. Pili, sala ya uwongo bila hisia.

Nyingi ya zile zinazoitwa “sala” siku ya leo si sala kabisa. Ni maneno tu mtu anayoyasema, si sala ya kweli kwa Mungu. Ni maneno tu yanayoonekana mazuri, yanayoonekana ni ya dini, lakini ni desturi tu, hayana maana, bila kumgeukia Mungu na kumwomba jambo.

Nimehudhuria sherehe nyingi za mahafali. Mapema katika sherehe kuna kitu kinachoitwa “sala.” Inastahili kuwa sala, lakini si sala. Anayesoma husoma sentensi kadha akiomba sherehe iwe nzuri, na wanafunzi wawe na maisha mazuri. Lakini hakuna yeyote anayetazamia Mungu ajibu na hasa afanye jambo au abandilishe jambo – hata yule anayesoma hiyo “sala.” Hakuna hisia zozote au neno kutoka kwa moyo katika sala kama hiyo.

Kuna wakati nilitembea Washington, D.C., mji mkuu wa nchi yetu. Na pale nikaingia katika kanisa kuu la taifa. Rais Reagan alikuwa amefariki, na walikuwa wanajitayarisha kuwa na ibada ya mazishi. Na pale nikasikia kasisi wa Episkopali akiyasoma maneno ya “sala.” Lakini hakuwa anasali kamwe. Alikuwa anayasoma maneno kutoka kwa kitabu. Hivyo tu na hakufanya lingine. Hakuwa anamuuliza Mungu afanye jambo lolote. Hakutarajia jibu. Alikuwa anayasema maneno tu kwa sababu hivyo ndivyo alihitajika kufanya. Hakuwa na hisia zozote kutoka kwa moyo.

Yesu alizungumzia juu ya Farisayo aliyeenda katika Hekalu kusali. Huyo mtu akasema, “Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma, hutoa zaka katika mapato yangu yote.” (Luka 18:11, 12). Hakuwa anasali kabisa. Hakumuuliza Mungu chochote. Badala ya hiyo alimwambia Mungu jinsi alivyo mzuri. Kristo alisema aliomba “moyoni mwake” (Luka 18:11). Hakuonyesha hisia zozote. Hakuwa anaomba kutoka kwa moyo wake.

Kristo aliwakemea Mafarisayo kwa sababu ya maombi yao ya uwongo. Alisema, “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi” (Mathayo 23:14). Walisali sala ndefu kujionyesha kwamba ni watakatifu. Lakini kile hasa walitaka ni kuchukua manyumba na pesa kutoka kwa mama wazee. Ilikuwa tu rahisi hivyo. Hisia zozote walizozionyesha zilikuwa za nje na za uwongo ili waonekane ni wazuri. Hawakuomba kutoka kwa moyo. Mioyo yao haikuwa sawa.

Unaweza kusema, “mimi si kama wao.” Lakini wewe huomba maombi ya uwongo, yaani kule kupitia maneno? Nimewahi fanya hivyo. Katika wakati wako wa maombi ya kibinafsi, wewe hutaja watu na vitu unavyoviombea, bila kuvifikiria, bila kumuuliza Mungu ajibu? Umewahi kufanya hivyo katika mikutano ya maombi kanisani? Nimewahi fanya hivyo. Uliomba kwa sababu ulihitajika huombe jambo – kwa sababu zamu yako ya kuomba imefika? Na unafurahia mkutano unapoisha kwa sababu hautahitajika kuendelea kuomba. Hiyo haikuwa sala ya kweli. Lilikuwa jambo tu ulilolipitia. Umewahi kujaribu “kuomba vyema” ili umvutia mtu mwingine? Ninamjua mtu aliyepanga maombi yake kabla ya wakati. Hayo hakika hayakuwa maombi, hiyo ilikuwa hotuba, yalikuwa matamshi tu. Ninasema, “Usipange maombi yako, yaombe!” Kabla ya mkutano wa maombi, tumia dakika chache umuulize Mungu akusaidie kuomba. Na unapoomba katika mkutano au wewe binafsi, fikiria kuhusu mambo unayoyaomba. Fikiria kuhusu jinsi hali ingekuwa mbaya ikiwa Mungu hatasaidia. Fikiria jinsi unavyohitaji sana jibu la Mungu. Kufunga kutasaidia maombi yako, kwa kuwa utakuwa makini na humwonyesha Mungu kwamba umejitolea. Geukia Mungu katika sala zako na umwombe akumbe kile unachoomba. Vile vile unaweza kulia kwa hisia. Usijinyamazishe. Ni Mungu amekuelekeza kufanya hivyo. Wakati mwingine unaweza kosa kulia. Usijilazimishe kulia. Sala haiwezi kuwa nzuri kwa sababu kuna kulia – wala haiwezi kuwa nzuri kwa sababu hakuna kulia. Sala ni nzuri wakati Mungu amehusika!

III. Tatu, sala ya kweli ikiwa na hisia na pia bila hisia.

Andiko letu linasema kwamba Kristo alisali kwa “maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi.” Lakini wakati mwingine sala ya kweli inayopata majibu inatendeka kukiwa na hisia ndogo au pasipo hisia. Nimekwambia jinsi ambavyo manabii wa Baali walivyoomba miungu yao ya uwongo. Sasa nataka nikueleze jinsi Eliya alivyoomba. Alisema,

“Ee BWANA, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. Unisikie, Ee BWANA, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, BWANA, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie.” (I Wafalme 18:36, 37).

Haijaandikwa ya kwamba Eliya alilia. Haijaandikwa ya kwamba Eliya aliruka-ruka. Na kwa hakika hakujikatakata! Alioamba tu akiwa amemaanisha. Alimwomba Mungu ajulishe watu ya kuwa yeye ndiye Mungu wa kweli. Na Mungu alijibu ombi hilo na akautuma moto kutoka Mbinguni kuiteketeza dhabihu ya Eliya. Watu walisema, “BWANA ndiye Mungu, BWANA ndiye Mungu” (I Wafalme 18:39). Ombi la Eliya aliloliomba akimaanisha, ambalo haijaandikwa lilikuwa na hisia, liko tofauti kabisa na fujo ya manabii wa Baali. Sala ya kweli hahitaji hisia. Sala ya kweli inahitaji Mungu!

Lakini wakati mwingi hisia, na hata machozi, huandamana na sala ya kweli. Ukitambua hitaji lako, ni kawaida kwako kuwa na hisia. Unaweza kumwita Mungu kwa bidii,kwa haraka, na kwa kulia. Unaweza kunyenyekea na kumwomba kwa machozi. Mara kwa mara Biblia huunganisha machozi na kuomba. Mwandishi wa Zaburi aliomba, “Ee BWANA, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyanyamalie machozi yangu” (Zaburi 39:12).

Mfalme Hezekia alikuwa mgonjwa karibu kufa. Hezekia alimwomba Mungu. Aliomba namna gani? Biblia inasema, “Hezekia akalia sana sana” (II Wafalme 20:3). Kwa kweli alilia. Alikuwa anaelekea kufa. Alilia sana. Alilia alipokuwa akiomba. Alafu neno la Mungu likamjia nabii Isaya kusema, “Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako, tazama, nitakuponya” (II Wafalme 20:5). “Nimeyaona machozi yako.” Mungu aliyaona na kuhisi machozi ya Hezekia katika ombi lake lilionyesha hawezi na anahitaji. Mungu alimjibu na akayaokoa maisha ya mfalme.

Katika Agano Jipya, mtu alimjia Yesu. Mwanawe alipagawa na pepo. Kristo alimuuliza ikiwa anaamini mwanawe anaweza kupona. Na “Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu” (Marko 9:24). Yesu alimfurusha yule pepo kutoka kwa yule kijana. Mara nyingi andiko hili linatumika kuonyesha ya kwamba mtu aliye na imani dhaifu anaweza kupokea majibu. “Nisaidie kutokuamini kwangu.” Lakini andiko hili pia linasema kwamba babake “alipaza sauti” na akazungumza na Kristo “kwa machozi.” Mtu huyu hakuwa mmoja wa Wanafunzi wake. Hakuwa mtu ambaye ameongoka. Alikuwa tu “mtu mmoja katika mkutano,” Mtu tu katika ule umati (Marko 9:17). Lakini alimleta mwanawe kwa Yesu na akapaza sauti kwake kwa machozi.

Kwa nini mtu huyu alipaza sauti kwa Yesu kwa machozi? Hakuwa shujaa wa maombi. Hakuwa ameokoka. Ilikuwa kawaida kwake kupaza sauti kwa Yesu namna hiyo, kwa maana aliliona hitaji lake. Mwanawe alikuwa amepagawa na pepo na hakuwa na njia nyingine ya kumweka huru pasipo Yesu. Huyu mtu akujifanya analia. Kwa sababu ya hitaji lake, kwa kukata tamaa kwake, machozi yake yalimtoka. Hitaji linapokuwa moyoni, kuwa katika hali ya kukata tamaa na kukosa tumaini, kila mara huelekeza katika kulia na machozi. Alipaza sauti katika sala ya kweli, na ilikuwa na hisia.

Na hiyo inaturudisha tena katika andiko letu. Kristo aliomba katika Bustani kwa “kulia sana na machozi.” Hakuwa mtoto anayependa kulia. Hakuwa msishana mwenye hisia aliyelia kwa kila jambo. Alikuwa mtu mzima, aliyekuwa na umra wa zaidi ya miaka thelathini. Alilia kwa nini? Kwa sababu alikuwa na hitaji lililomsukuma katika moyo wake. Alihisi dhambi ya kila mwanamume na kila mwanamke alizotwikwa. Alifikiria juu ya mateso makali yaliyokuwa lazima ayapitie Msalabani siku iliyofuatia, ambapo pasipo kupitia hayo hakuna yeyote angeokolewa. Na bado uzito wa dhambi za mwanadamu ulikuwa karibu kumuua. Bila neema ya Mungu, angekufa katika ile Bustani usiku ule na hangeweza kufika Msalabani. Kristo alikuwa na uzito sana katika moyo wake. Na hivyo aliomba kwa “kulia sana na machozi.” Lilikuwa jambo la kawaida na asilia katika ile hali. Lingekuwa jambo la kushangaza kama angeomba bila hisia. Yesu aliomba kwa “kulia sana na machozi.” Na andiko letu linatuambia ya kwamba “akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu.” Mungu alilijibu ombi lake na akamweka hai ili kwenda Msalabani siku iliyofuatia. Mungu alimjibu kule “kulia sana na machozi.”

Mkristo, Ninakuuliza, “Wewe huomba kwa kulia sana na machozi?” Sizungumzii kila ombi unalo omba. Lakini mara nyingine nakuuliza, “Wewe huomba daima kwa kulia sana na machozi?” Nimewahi, lakini si kila mara ninavyostahili. Wewe wakati mwingine huomba ukiwa na uzito wa hitaji, ukimsihi Mungu akupe jibu –wakati mwingine kwa kulia sana na machozi? Ikiwa haufanyi hivyo, hauna maisha mazuri katika maombi yako. Ikiwa wewe ni wa namna hiyo, usisimamishe kuomba hadi maombi yako yawe bora. Hivyo sivyo Mungu anavyotaka. Lakini omba Mungu akusadikishe katika hitaji lako, halafu utaomba kwa hisia. Unapofunga, na kila unapohisi njaa, fikiria kuhusu jambo unaloliombea. Mgeukie Mungu na uombe.

Wengine wenu wamepotea. Hauja mwamini Yesu. Ninakuuliza, “Unahisi dhambi zako kwa kulia sana na machozi – angalau wakati mwingine?” Unahukumika kwa anjili ya dhambi zako? Kulia siyo lengo – Yesu ndiye lengo. Mwamini ikiwa utalia au hautalia. Lakini nasema, “Wewe huwa unahisi huzuni yoyote juu ya dhambi za moyo wako?” Unastahili, kwa sababu moyo wako ni “mdanganyifu kuliko vitu vyote” (Yeremia 17:9). Mwombe Mungu akuonyeshe jinsi dhambi za moyo wako zilivyo za kutisha. Halafu humwombe Mungu akulete kwa Kristo.

Yesu ndiye jibu ya hitaji lako. Yeye ndiye dawa na malipo kwa dhambi zako. Alikufa Msalabani kulipia kila dhambi, hata dhambi za moyo wako. Alimwaga Damu yake kufunika dhambi zako na kuziosha milele. Alifufuka kutoka kwa wafu kushinda mauti kupitia uhai, si kwa anjili yake tu lakini kwa anjili yako. Ukimwamini Yesu, utaokolewa milele. Ikiwa ungependa kuzungumza nasi kuhusu kumwamini Kristo, tafadhali njoo uketi katika safu mbili za mbele. Amina.


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Jack Ngann:
“Nifundishe Kuomba” (na Albert S. Reitz, 1879-1966).


MWONGOZO WA

MACHOZI KATIKA MAOMBI

TEARS IN PRAYER

na Dkt. Christopher L. Cagan

“Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu” (Waebrania 5:7).

(Luka 22:44)

I.    Kwanza, sala ya uwongo ikiwa na hisia, I Wafalme 18:26, 28, 29.

II.   Pili, sala ya uwongo bila hisia, Luka 18:11, 12; Mathayo 23:14.

III. Tatu, sala ya kweli ikiwa na hisia na pia bila hisia,
I Wafalme 18:36, 37, 39; Zaburi 39:12; II Wafalme 20:3, 5;
Marko 9:24, 17; Yeremia 17:9.