Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




MWOYO WA KRISTO ALIPOKUWA NJIANI KUELEKEA MSALABANI

THE HEART OF CHRIST ON THE WAY TO THE CROSS
(Swahili)

na Dkt. C. L. Cagan

Mahubiri yaliyo hubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Asubuhi ya, Machi 10, 2019
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Morning, March 10, 2019

“Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka” (Mathayo 16:21).


Sasa tuko katika ule wakati Wakatoliki wanaouita “Kwaresima.” Ni kipindi cha siku arobaini kabla ya Pasaka. Kipindi hiki kilianza Jumatano iliyopita, Ambayo wengine wanaiita “Jumatano ya majivu.” Aprili 19 ni Ijumaa kuu ambayo tutakumbuka kusulubishwa kwa Yesu. Aprili 21 ni Pasaka, siku ambayo Kristo alifufuka kutoka kwa wafu.

Biblia imetenga nafasi kubwa kuhusiana na juma ya mwisho ya Kristo hapa duiniani, kuhusu kifo chake na kufufuka kwake. Injili ya Mathayo ina vifungu 28. Vinane kati ya vifungu hizi vinazungumzia muda huu mfupi. Kufa na kufufuka kwa Kristo ni matukio yaliyomuhimu kabisa katika historia yote. Bila matukio haya hakuna yeyote angeza kuokolewa.

Ni vyema kufikiria kuhusu Yesu na kusulubiwa kwake. Kristo kila wakati alifikiria kuhusu kusulubiwa kwake. Kila wakati jambo hili lilikuwa katika mawazo yake. Aliwambia wanafunzi wake hili siku kadha kabla ya kwenda msalabani. Andiko letu linasema, “Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka” (Mathayo 16:21).

Yesu alikuwa njiani kuelekea msalabani kwa miaka kadha. Hiyo ndiyo sababu ilimfanya aje duniani. Hata akiwa Mbinguni, kabla hajasaliwa Bethlehemu, kila wakati alikuwa njiani akielekea msalabani. Na hili linaonyesha moyo wake. Leo nitazungumzia kuhusu moyo wa Kristo. Lakini kwanza ni lazima niwaambie kuhusu moyo wa wanafunzi wake waliopotea.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

I. Kwanza, moyo wa wanafunzi wapotevu walipokuwa njiani kuelekea msalabani.

Petro alikuwa wa kwanza katika hawa wanafunzi. Lakini Petro hakuwa na moyo wa Kristo. Petro hakuelewa kwa nini Yesu aende msalabani. Wakati Kristo alisema “imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi...na kuuawa” (Mathayo 16:21),

“Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata” (Mathayo 16:22).

Petro almkemea Mwana wa Mungu! Petro hakuupenda moyo wa msalaba. Yesu alimjibu Petro,

“Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya mwanadamu” (Mathayo 16:23).

Petro hakuwa na moyo na mawazo ya Kristo. Petro alikuwa na moyo na mawazo ya mwanadamu. Huo moyo ulikuwa moyo wa Shetani. Kristo alimwambia, “Nenda nyuma yangu, Shetani.” “Petro, unaongea kama Ibilisi. Unayasema yanayosemwa na Ibilisi.”

Petro hakukubaliana na Yesu. Alikuwa kinyume na yale Kristo aliyasema kuhusu kusulubishwa kwake. Hakuwa na moyo na mawazo ya Kristo. Alichokuwanacho ni moyo na mawazo ya mwanadamu aliyepotea na mwenye dhambi, kwa maana alikuwa bado hajaongoka. Mwalimu mashuhuri wa Biblia Dkt. J. Vernon McGee alisema wanafunzi hawakuwa wameongoka hadi pale Kristo alifufuka kutoka kwa wafu. Dkt. McGee alisema, “Mimi binafsi ninaamini wakati ule Kristo aliwapulizia [baada ya kufufuka kwake, Yohana 20:22] watu hawa walihuishwa [waliokolewa]. Kabla ya hilo, Roho wa Mungu akuwa ameingia ndani yao” (J. Vernon McGee, Th.D., Kupitia Biblia, Wachapishaji waThomas Nelson, seheme IV, uk. 498; maelezo kuhusu Yohana 20:21). Kabla ya wakati huo, Petro alifikiria kama mtu mwingine yeyote yule aliyepotea. Wanafikiria aji?

Watu wasioongoka wanaamini kuwa mbele kila wakati. Wanafanya hivyo kwa uwezo na nguvu na fikira na ustahiki. Wengine wao usema uongo na undanganya. Kwa waliopotea, jambo la kwanza huwa pesa na mafanikio na uwezo kuliko mambo mengine. Kuwahusu hawa watu Biblia inasema, “Jumla ya mawazo yake ni, Hakuna Mungu” (Zaburi 10:4).

Umewahi kusikia mtu akiongea kuhusu “dola yenye nguvu”? Wanafikiria kuhusu pesa. Pesa ndiyo njia yao ya ushindi – ndiyo njia wanayotumia kujithamini. Kwa wanariadha, ni alama wanazopata. kwa wengine, ni marafiki wa kike au wa kiume walionao. Lakini utakapokufa Mungu atakwambia, “Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako” (Luka 12:20). Alama zako za juu asitakusaidia wakati huo.

Kujiendeleza kibinafsi ndiyo njia ya ulimwengu. Biblia inasema, “ Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu” (Wafilipi 2:21). Biblia inasema, “Hakuna amtafutaye Mungu” (Warumi 3:11). Lakini kila mmoja “anatafuta vyake mwenyewe.” Unatafuta vyako mwenyewe. Lakini utakapokufa, “Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako.”

“Wote wanatafuta vyao wenyewe.” Kila mmoja anatafuta vyake mwenyewe. Hivyo ndivyo Petro na wanafunzi wengine walivyofikiria. Hawakutaka Yesu aende msalabani. Walimtaka ajitawaze Mfalme wakati huo. Halafu wangetawala pamoja naye. Wangekuwa wenye uwezo na wa maana. Wangejipatia “vyao wenyewe.” Kristo aliwafundisha wanafunzi wake, “Mwana wa Adamu yuaenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hata akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka. Lakini hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza” (Marko 9:31, 32). Wanafunzi walikuwa wakiyazungumzia mambo yaliyokuwa kinyume na hayo, “kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa” (Marko 9:34). Baadaye kidogo Kristo aliwauliza Yakobo na Yohana, “Mwataka niwafanyie nini?” (Marko 10:36). “Mnataka niwafanyie nini?” Walisema, “Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wa kuume, na mmoja mkono wa kushoto, katika utukufu wako” (Marko 10:37).

Wanafunzi walikuwa na moyo wa ulimwengu. “Kila mmoja anatafuta vyake mwenyewe.” Walimwona Yesu akitenda miujiza. Alikuwa Masihi, Kristo wa Mungu. Wanafunzi walifikiria Kristo ataanzisha Ufalme wake na kutawala ulimwengu wakati huo. Walitarajia kutawala pamoja naye. Kristo alipokamatwa, ilionekana kana kwamba tumaini hilo limekwisha. Hiyo ndiyo sababu “Ndipo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia” (Mathayo 26:56).

Yuda alikuwa na moyo huo huo. Ndiye aliyembebea Kristo pesa na wanafunzi wake. Biblia inasema “naye ndiye aliyeshika mfuko” (Yohana 12:6). Lakini Yuda alikuwa mwizi. Alichukua pesa kutoka kwa ule mfuko. Alikaa pamoja na Yesu kwa sababu alifikiria Kristo atatawala kama Mfalme, na alafu yeye, Yuda, angehusika katika mambo yote ya pesa. Halafu angekuwa tajiri kabisa! Lakini Yesu alizungumzia kuhusu kusulubishwa. Kule Yerusalemu alihubiri kinyume na makuhani na Mafarisayo. Yuda alifikiria Kristo hakustahili kufuatwa. Hatawahi kuwa Mfalme. Ataingia katika matatiso. Yuda alitaka kutoka katika machua kabla haijazama. Na alipata pesa kutokana na hilo. Alimsaliti Kristo kwa “vipande thelathini vya fedha” (Mathayo 26:15).

Watu waliopotea walio kanisani wana mawazo kama yale yaYuda na Petro. Kwa muda ule wote watakapokuwa wakipata kitu kutokana na kanisa, na inaonekana kama watapata zaidi – urafiki, furaha, heshima, rafiki wa kiume au wa kike – watakaa. Lakini wanashuka kutoka kwa machua kunapotokea dhoruba, au ikionekana kama ile machua inaweza zama. Hawana moyo wa Kristo. “Wote wanatafuta vyao wenyewe.”

Watu waliopotea wanapoingiwa na udini, bado wako na ule moyo tu, “Wote wanatafuta vyao wenyewe.” Wangekuwa na moyo mwingine gani? Wanaonyesha moyo wao wanapojaribu kuingia mbinguni kupitia wema wao, si kwa msamaha wa Mungu kupitia Kristo. Kwao, kuongoka ni kazi ya wema wao na maarifa yao. Wanaongozwa na kiburi na kujipenda. Wanaweza kuwa kanisani kwa muda mrefu bila kuwa Mkristo halisi ndani yao.

Watu waliopotea hawana moyo wa Kristo. Si ya kwamba tu wanafunzi hawakuelewa. Hilo lingerekebishwa kupitia mafundisho. Petro na wengine hawakupenda Yesu aende msalabani. Kristo alipozungumzia hilo jambo, Petro “alianza kumkemea” Yesu (Mathayo 16:22). Wanafunzi walitaka Yesu atawale kama Mfalme na awahusishe. Msalaba ulikuwa kinyume na mambo yote waliyoyapenda maishani.

Biblia inazungumzia “kwazo la msalaba” (Wagalatia 5:11). Msalaba ulikuwa kikwazo kwao. Neno la Kiyunani linalotafsiriwa “kikwazo” ni skandalon. Tunapata neno “Kikwazo” kutokana na hili neno. Kristo, Mungu Mwenye enzi, alisulubishwa, kifo kilichokuwa kibaya zaidi katika ulimwengu wa Warumi – na kwa wenye dhambi. Kilikuwa kikwazo! Kwa watu wa dini wenye kiburi, msalaba ulikuwa kinyume na mambo yote wanayoyajua. Msalaba ni kikwazo kwao.

Ni kwa nini Petro alichukua hicho kikwazo? Ndilo lilikuwa jambo la pekee ambalo angeweza kulifanya! Hakuwa na moyo na mawazo ya Kristo. Alichokuwanacho ni mawazo ya mtu asiyeongoka, ambayo Biblia inasema “ni uadui juu ya Mungu” (Warumi 8:7). Mwanadamu aliyepotea “haitii sheria ya Mungu, wala hawezi kuitii” (Warumi 8:7). Hawezi kuwa na moyo wa Kristo.

Na hauna moyo wa Kristo. Wewe ni mwenye dhambi. Yote uliyonayo ni dhambi. Na yote uliyo ni dhambi. Unatafuta vyako mwenyewe. Hivyo ndivyo ulivyo.

Hata wakati unapojaribu “kuokoka” hauwezi. Kwako uongofu ni “ufanisi mkuu” wako, kama vile kupata alama nzuri katika shule au kupata pesa. Lakini bado haujaokolewa. Unaweza kuja kanisani. Unaweza kujilazimisha kuhisi jambo – ama ungojee kupata hisia kutoka kwa Ibilisi. Utajikaza kuamini mafundisho fulani kuhusu Kristo – “kwamba” alikufa kwa anjili yako – na utajaribu kutokuwa na hisia zozote. Lakini bado wewe ni mchoyo, anayejaribu “kuwa sawa” kwa njia yake mwenyewe. Haujioni kama chukizo, mtu aliyefilisika, mwenye dhambi mpotovu, ambaye hawezi fanya lolote ila tu ajitupe kwa Yesu.

Unaweza kuyasema maneno ya mtoza ushuru, “Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi” (Luka 18:13) lakini hauna chochote kinachohusu moyo wake. Unaweza kuomba ombi lakini ndani yako hauna chochote kinachohusiana na maana ya ombi hilo. Wewe ni mwanamume au mwanamke aliyepotea ambaye haelewi. Ndani mwako, ni kikwazo kwako kwamba haujaokoka, na kwamba wengine waliotenda dhambi kukuliko wameongoka, ambao wamekuwa kanisani muda mfupi kukuliko, wanaojua machache na wewe unajua zaidi kuwaliko. Yote uliyonayo ni kwamba umepotea, u mchoyo, mbinafsi asiyeongoka. Hauna moyo na mawazo ya Kristo. Na hii inanileta katika sababu ya pili.

II. Pili, moyo wa Kristo alipokuwa akielekea Msalabani.

Kristo alijua kabisa kile alikuwa anafanya. Hakusulubishwa kwa bahati mbaya. Alichagua kufa. Angejinasua na awe huru wakati wowote. Pale msalabani alisema, “Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?” (Mathayo 26:53). Yesu alienda msalabani kwa kusudi. Andiko letu linasema,

“Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka” (Mathayo 16:21).

Kristo alikusudia kusulubishwa. Biblia inasema, “Yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu;” (Luka 9:51). Aliwambia Andrea na Filipo,

“Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa anjili ya hayo nilivyoifikia saa hii” (Yohana 12:27).

Kwa tafsiri nyingine katika Kiswahili, “Nastahili kumuuliza Baba yangu aniokoe na haya? Hapana, hii ndiyo sababu nilikuja hapa!” Yesu alikusudia kwenda Msalabani na kufa.

Lakini ni nini kilikuwa katika moyo wake? Kristo hakustahili kuja na kufa. Yesu hakuja kwa sababu ya sharti au wajibu. Yeye Mwenyewe hakutenda dhambi. Hakustahili kuja. Kristo alikuja kwa kujitolea. Ni nini kilichokuwa katika moyo wake? Biblia inasema,

“Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho” (Wafilipi 2:5, 6).

Kama Mungu Mwana, Alikuwa Mungu sawasawa na Mungu Baba. Angekaa Mbinguni. Hakuwa na dhambi. Wenye dhambi ulimwenguni walistahili kuadhibiwa. Kristo angekuwa sawa kabisa na angekuwa na haki ya kukaa Mbinguni. Lakini ni nini kilikuwa katika moyo wake? Yeye “hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho” (Wafilipi 2:6). Katika tafsiri nyingine inasema, “Yeye, ingawa alikuwa Mungu, hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho”. Kwa Yesu, kuwa Mbinguni, Uungu wake ukiwa sawasawa na Uungu wa Mungu Baba, haukuwa kitu cha kushikamana nacho. Haukuwa kitu cha kushikamana nacho. Kristo aliachilia utukufu wake wa Mbinguni na kuja hapa ulimwenguni, si kutawala lakini kufa kama jambazi, si kwa sababu ya jambo mbaya alilolifanya, lakini kwa sababu ya dhambi ya wengine. Biblia inasema ya kwamba Yeye

“bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii ata mauti, naam, mauti ya msalaba” (Wafilipi 2:7, 8).

Kristo hakustahili kuja. Alichagua kuja – kwa sababu ya upendo. Kama alivyoandika Joseph Hart,

Kwa nini, Mwokozi mpendwa, niambie kwa nini ulikaa pale ukitokwa na damu na kuteseka?
Ni kusudi gani lililokusukuma? kusudi liko wazi – ilikuwa kwa sababu ya upendo!
   (“Gethsemane, Shinikizo la zabibu!” na Joseph Hart, 1712-1768; katika wimbo
      “‘Ni usiku wa manane, ukingoni mwa mizeituni”).

Kristo hakuja kama Mfalme, lakini kama mtumishi aliyekuwa katika mateso. Hakuja kutumikiwa, lakini kutumika. Yesu alisema,

“Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Marko 10:45).

Hilo ndilo lilikuwa Kusudi lake. Huo ndio uliokuwa moyo wake. Hiyo ndiyo sababu alikuja. Mtume Paulo alisema, “Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi” (I Timotheo 1:15) kwa sababu anakupenda.

Hakuja kuwafundisha watu waliofikiria tayari wameokoka. Alikuja kuwaokoa wenye dhambi. Wakati Zakayo aliyekuwa mwovu aliokoka, Kristo alisema, “Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea” (Luka 19:10). Tena, Yesu alisema, “Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu” (Luka 5:32). Kama vile Bw. Ngann alivyoimba kabla ya mahubiri,

Si kwa watakatifu, si kwa watakatifu; Yesu alikuja kuwaita wenye dhambi.
Si kwa watakatifu, si kwa watakatifu; Yesu alikuja kuwaita wenye dhambi.
(“Njooni, Enyi wenye dhambi” na Joseph Hart, 1712-1768).

Ukija kama mwenye haki, hautaokolewa. Lakini ukijiona kama mtu aliyepotea na mwenye dhambi ambaye hawezi kujisaidia, unaweza kuja kwa Kristo. Utampata akiwa tayari kukupokea na kukusamehe – sasa hivi. Wezi wawili walisulubishwa kado ya Kristo, mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto. Mmoja wao alizungumza na Yesu. Hakujua mengi. Lakini alisema kwa kuamini, “Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako” (Luka 23:42). Mwizi huyo aliokolewa papohapo. Yesu alimjibu, “Leo hivi utakuwa pamoja nami peponi” (Luka 23:43). Dkt. Hymers amekueleza jinzi watu wemehangaika kwa njia mbalimbali bila kupokea uongofu. Mwishowe wanapookoka kupitia kumwamini Kristo, kila mara wanasema, “Hivi tu ndivyo ulivyotaka?” Ndio, hivyo ndivyo tunavyotaka! Mwamini Yesu! Ni rahisi – lakini Kristo unayemwamini atakuokoa milele! Kama alivyoimba Bw. Ngann sang,

Njooni, enyi wenye dhambi, maskini na wenye mashaka, Wanyonge na wenye majeraha, wagonjwa na wenye vidonda;
Yesu yuko tayari kukuokoa, Amejaa huruma, upendo na uwezo;
Anaweza, Anaweza, Amekusudia, usiwe na shaka tena!
Anaweza, Anaweza, Amekusudia, usiwe na shaka tena!
(“Njooni, Enyi Wenye dhambi” na Joseph Hart, 1712-1768).

Yesu aliniokoa, niliyekuwa mchoyo, mlafi, mwenye dhambi aliyejaa dhihaka. Alimwokoa Petro aliyekuwa mwoga na msaliti. Alimwokoa Musa aliyekuwa muuaji. Alimwokoa Paulo aliyekuwa mdhalimu. Kristo atakuokoa ikiwa utamwamini. Damu Yake itaziosha dhambi zako. Ikiwa ungependa kuzungumza na kuomba kuhusu kumwamini Yesu, tafadhali njoo na uketi katika safu hizi mbili za kwanza. Amina.


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Jack Ngann:
“Njooni, Enyi wenye Dhambi” (na Joseph Hart, 1712-1768; umefanyiwa mageuzi na Dkt. Hymers).


MWONGOZO WA

MWOYO WA KRISTO ALIPOKUWA NJIANI KUELEKEA MSALABANI

THE HEART OF CHRIST ON THE WAY TO THE CROSS

na Dkt. C. L. Cagan

“Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka” (Mathayo 16:21).

I.   Kwanza, moyo wa wanafunzi wapotevu walipokuwa njiani kuelekea msalabani, Mathayo 16:22, 23; Zaburi 10:4; Luka 12:20;
Wafilipi 2:21; Warumi 3:11; Marko 9:31, 32, 34;
Marko 10:36, 37; Mathayo 26:56; Yohana 12:6; Mathayo 26:15;
Mathayo 16:22; Wagalatia 5:11; Warumi 8:7; Luka 18:13.

II.  Pili, moyo wa Kristo alipokuwa njiani kuelekea msalabani,
Mathayo 26:53; Luka 9:51; Yohana 12:27; Wafilipi 2:5, 6;
Wafilipi 2:7, 8; Marko 10:45; I Timotheo 1:5; Luka 19:10;
Luka 5:32; Luka 23:42, 43.