Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.
GHARAMA YA KUWA MKRISTO MWANAFUNZI

WHAT IT COSTS TO BECOME A CHRISTIAN DISCIPLE
(Swahili)

Na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana jioni ya, Februari 17, 2019
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Evening, February 17, 2019

“Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?” (Luka 14:28).


Sasa tufungue pamoja kitabu cha Mathayo, sura ya 16, mstari wa 24.

“Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate”
(Mathayo 16:24).

Vijana wengi siku ya leo hawana mwelekeo wa kufuata na hawana azimio katika maisha yao. Unaishi siku iishe uingie katika siku nyinngine. Kwa kweli, vijana siku ya leo wanaonekana wanaishi dakika kwa dakika. Unayashughulikia maisha kama vile kutafuta mawimbi katika runinga – kila wakati unabandilisha mawimbi kwenda mengine bila hata kutazama programu yote.

Sasa kuna hatari katika hilo jambo. Haupati habari kamili. Hivyo ndivyo vijana wengi hulichukulia kanisa. “Unabandilisha mawimbi” – ukiingia na kutoka. Unaenda Las Vegas Jumapili hii na kwenda kanisani Jumapili ifuatayo. Lakini hauwezi kupata habari kikamilifu kwa njia hiyo. Unapata tu mambo yasiyomakamilifu. Kwa mfano, unasikia tu kuhusu mafundisho ya mageusi, na unakosa kusikia kuhusu mafundisho ya nyakati za mwisho, mafundisho kuhusu wokovu, mafundisho kuhusu mapepo, na mafundisho mengine mengi.

Kuwa Mkristo mkamilifu ni lazima ujitolee kikamilifu kwa Yesu Kristo:

“Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate”
(Mathayo 16:24).

Sasa, wokovu ni kwa neema. Mtu asiyeongoka hawezi kuyafanya aliyoyasema Yesu, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.” Lakini Mungu amekuvuta katika kanisa hili kuisikia Injili. Na mtu wa Mungu Thomas Watson alisema sahihi, “Mungu anapoanza kuvuta tunaweza kufuata.” Ama, unaweza kuamua usifuate, hata ingawa, ndani yako, unajua unastahili kufuata.

Mtu asiyeongoka amejaa ukinzani. Unakuja kanisani na ndani yako unabishana na mhubiri na Biblia. Ndani ya moyo wako unasema, “Si amini Biblia.” Lakini baadaye unafikiria, “Nimeshindwa na maisha. Sina tumaini yeyote jinsi nilivyo.” Unavutwa mbele na nyuma. Sehemu moja yako inamuasi Mungu na sehemu nyingine yako inataka kuamini kwamba kuna tumaini kwa Mungu. Kuna mabishano ndani yako. Na kila mtu aliye hapa jioni ya leo amepitia mabishano ya aina hii.

Naweza tembea juu na chini katikati ya mistari ya viti katika kanisa hili usiku wa leo na niwape hadithi baada ya hadithi kutoka kwa vijana waliohapa. Kila mmoja wao alikuwa na mabishano ndani mwake. Inaweza kuwa haifanani na mabishano yako, lakini kila wakati kuna mambo yanayofanana. Kwa upande mmoja unataka kuja kanisani na unatumainia kuna Mungu na wokovu na upande mwingine unamuasi Mungu, Biblia na mhubiri.

Kwanza, ni nini chanzo cha mabishano ndani yako? Kwanza, kuna ulimwengu (wazazi, marafiki, furaha). Halafu kuna mwili wako (unataka kukosa kanisa, ufanye ngono unavyotaka, na ufanye vitu vyako). Halafu kuna Shetani. Upand ule mwingine, kuna Roho Mtakatifu. Ndiye sauti nyororo inayozungumzia dhamiri yako. Anakuita uje kwa Yesu Kristo na katika kanisa hili. Kwa hivyo, kuna mabishano kwa ajili ya nafsi yako. Mungu anakuita kwa upande mmoja – nayo dhambi na raha za ulimwengu zinakuita upande ule mwingine.

Biblia inasema, “Chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia…au kwamba ni miungu ya wale Waamori [Wamarekani] ambao mnakaa katika nchi yao: lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA” (Yoshua 24:15). Ni lazima uchague. Kwa bahati mbaya, wengi wenu watafanya chaguo mbaya. Uzoefu wangu wa miaka 60 katika huduma uniambia kwamba pengine utafanya chaguo mbaya. Biblia inasema,

“Na kufa kutachaguliwa kuliko kuishi” (Yeremia 8:3).

Na wewe je?

Pili, kwa nini ufanye chaguo nzuri? Kwa nini uje katika kanisa hili na uwe hapa kila Jumapili? Kwa nini uje kwa Kristo na uongoke?

1. Kwa sababu itakupa maana ya kuishi.

2. Kwa sababu itageuza hali yako ya kushindwa. Hakuna anayempata Kristo na kubakia katika hali ya kushindwa.

3. Kwa sababu itakupa tumaini la siku za usoni.

4. Kwa sababu itaondoa kosa lako na ikuongoze katika utele, wa maisha ya amani.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

Kwa majaribu yote katika maisha ya Sabina Wurmbrand alikuwa mkunjufu, mwanamke aliyejaa tabasamu kwa sababu alimjua Yesu Kristo binafsi. Sabina alikuwa katika kanisa letu mara nyingi kabla hatuja geuza taratibu na kuwa kanisa la Kibaptisti lililohuru. Mke wangu na mimi tulishiriki chakula cha jioni pamoja na Mchungaji Wurmbrand na Bi Wurmbrand katika chumba chao. Alijitoa kwa hali na mali kwa sababu ya Kristo. Lakini alikuwa mmoja wa wanawake wenye furaha kati ya wale nimewahi kuwajua.

Muulize mtu yeyote ambaye amekuwa hapa kwa muda! Ulizia Sabina Wurmbrand, sasa ako mbinguni! Watakwambia huo ni ukweli! Unastahili kuchagua kuwa katika kanisa hili na uongoke kwa sababu huo ni uamusi ulio sawa. Hiyo ndiyo sababu kuna sauti ndogo nyororo katika moyo wako inayosema, “Unajua anasema ukweli.”

Halafu, la tatu, ni lazima nikuambie kuna mambo unastahili kuyaacha na kuna mambo unastahili kuanza kufanya ikiwa unataka kuishi maisha ya Ukristo.

Yesu alisema:

“Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate”
(Mathayo 16:24).

Unapokuja kwa Biblia utaona ya kwamba Mungu anahitaji ujitolee kabisa.

Angalia ni nini Mungu alihitaji kwa Ibrahimu. Mungu alisema siku moja, “Ibrahimu, nataka huende katika Mlima wa Moria na nataka umchukue mwanao, mwana ambaye umemngojea kwa miaka mingi, mwana unayempenda kuliko vitu vyote ulimwenguni, na nataka umtoe kama dhabiu katika madhabau.”

Ibrahimu alimtii Mungu na alienda akamweka mwanae katika madhabau na akakichukua kisu kirefu kilichokuwa na makali na alikuwa anakielekeza kuudunga moyo wa mwanawe katika kumtii Mungu. Lakini Mungu aliusimamisha mkono wake uliokuwa umeinuliwa kumudunga mwanae. Mungu alisema, “Hadi hapa hiyo inatosha, Ibrahimu. Ninajua uko tayari kwenda pamoja nami katika hii njia sasa.”

Ama umwangalie Musa. Musa alikuwa mwana wa kiume ambaye bintiye Firauni alikuwa mzazi mlezi. Alikuwa mrithi wa kiti cha ufalme cha Misri. Pengine angekuwa mfalme wa milki iliyokuwa kuu katika ulimwengu wa wakati wake. Alikuwa na utajiri wote na mamlaka yote na utukufu wote ambao mwanadamu angekuwa nao. Lakini Musa aliyaacha hayo yote ili ashiriki mateso pamoja na watu wa Mungu. Mungu alimhitaji Musa aache hayo yote ili amtumie. Na halafu Mungu akamweka kule nyikani kusoma, kuomba, na kujifundisha.

Ama Yusufu.Yusufu aliuzwa kama mtumwa na ndugu zake. Alienda Misri kufanya kazi kwa mtu aliyeitwa Potifa. Alikuwa mbali na jamii yake na marafiki. Alikuwa tu tineja. Angeridhiana na lile jambo. Hakuna mtu angelijua, ila Mungu. Na mke wa Potifa alikuwa mrembo mno. Alijaribu kumchawishi ajamiiane naye. Alijua ya kwamba angefanikiwa katika ule ufalme kupitia usaidizi wa mke wa Potifa – lakini alikataa. Aliliacha koti lake mke wa Potifa alipomshika. Jambo hili lilisababisha apelekwe jela na kuhukumiwa kifo. Mungu alikuwa anamjaribu kijana huyu mchanga ili kuona kama hakika amemaanisha. Baadaye aliachiliwa kutoka jela na akapanda gazi hadi cheo cha juu kilichokuwa cha pili katika nchi ya Misri.

“Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate”
(Mathayo 16:24).

Ama mchukue Danieli. Walisema, “Danieli, hakuna maombi tena katika Babeli. Ukiomba, utatupwa katika tundu la simba.”

Lakini Danieli aliomba mara tatu kila siku madirisha yakiwa yamefunguliwa. Hata ingawa alikuwa waziri mkuu katika ile nchi, walimuweka katika tundu la simba. Na Danieli hakujua ya kwamba Mungu atavifunga vinywa vya simba. Mungu alimuita kulipa gharama naye alikuwa radhi kufanya hivyo.

Na Yesu anakwambia jioni ya leo,

“Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate”
(Mathayo 16:24).

Ina maana kwamba uwe tofauti na watu wengine. Vijana wengi leo wanavaa mavazi yanayofanana. Wanafanana. Wanafanya mambo kwa njia inayofanana. Wanaogopa kuwa tofauti. Ukiwa na marafiki ambao wananyoa nywele na kuweka kipini katika mapua yao, unataka kunyoa nywele na kuweka kipini katika pua lako pia – ili usionekane kama uko tofauti – ili uweze kuingiana nao. Lakini Biblia inakuita ili uwe mtu tofauiti – utoka katikati ya umati na uwe mtu asiyeridhiana nao katika mawazo na kiroho.

Wakati wengine wanasema hakuna Mungu ama Mungu ana maana, ni lazima usimame na useme ya kwamba Mungu ana maana na Mungu anaumuhimu na yeye ndiye nguzo ya maisha yangu! Sabina Wurmbrand alifanya hivyo, hata ingawa kaka zake wawili na dada zake wawili, na wazazi wake wote wawili waliuawa katika kambi za mateso za Hitler walipowasafirisha Wayahudi kutoka Romania wakati wa vita vya pili vya dunia.

Wakati wengine wanasema, “Usirudi katika kanisa hilo la Baptisti. Nifuata. Twende mahali pengine,” Ni lazima uwe tayari kusema, “Hapana. Ninarudi huko. Namhitaji Mungu. Namhitaji Yesu Kristo na haijalishi itanigharimu nini! Nataka kumsikiliza tena yule mhubiri asili. Nahitaji kile hawa watu walichonacho katika kanisa la Baptist Tabernacle!”


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Jack Ngann:
“Bwana Amekuja” (na Sarah Doudney, 1841-1926).