Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




JINSI KRISTO ATAKAVYOANZISHA
UFALME WAKE DUNIANI

HOW CHRIST WILL SET UP HIS EARTHLY KINGDOM
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Jioni ya, Januari 13, 2019
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Evening, January 13, 2019

“Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini. Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la mlima yangu; kwa maana bonde lile la mlima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na BWANA, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye…Naye BWANA atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja” (Zekaria 14:4-5, 9).


Karibu kila mtu duniani amesikia kuhusu kuja kwa Kristo mara ya kwanza, aliyetumwa na Mungu kwa tumbo ya bikira Mariamu, aliyezaliwa katika hori la ngombe kule Bethlehemu. Ndio, nyote mmesikia kuhusu kuja mara ya kwaza kwa Kristo. Na bado kumbukumbu katika Biblia kuhusu kuja Kwake mara ya pili zimezidi kumbukumbu kuhusu kuja Kwake mara ya kwanza kwa nane kwa moja unapolinganisha. Dkt. Daudi Yeremia alisema,

Wasomi wamehesabu kumbukumbu katika Biblia za kurudi mara ya pili kuwa 1,845, hii ni pamoja na mara 318 katika Agano Jipya. Kurudi Kwake kumetiliwa mkazo na vitabu visivyopungua kumi na saba katika Agano la Kale na sura saba katika kila sura kumi katika Agano Jipya. [Kristo] Mwenyewe alizungumzia kuhusu kurudi Kwake mara ishirini na moja. Hoja ya kuja Kwake mara ya pili ni ya pili kutoka kwa hoja ya imani katika hoja zilizokuu katika Agano Jipya (Daudi Yeremia,D.D. Ni nini kinachoendelea katika ulimwengu?,Kimechapishwa naThomas Nelson, 2008, uk 217).

Mojawapo ya mistari katika Maandiko kuhusu kuja mara ya pili kwa Kristo ni hili andiko letu, Zekaria 14:4-5, 9. Tunajifunza mambo matatu makuu kutoka kwa somo hili.

I. Kwanza, Kristo atarudi katika Mlima wa Mizeituni.

Niko na uhakika ya kwa maelezo ya Scofield yako sawa anaposema.

Zekaria 14 imeeleza mambo yote kwa muhtasari. Jinsi [matukio] yatakavyofuatana: (1) Kukusanywa kwa mataifa, mstari.wa 2 (tazama “Har-Magedoni,” Ufunuo. 16:14; 19:11, maelezo); (2) ukombozi, mstari wa 3; (3) kurudi kwa Kristo katika Mlima wa Mizeituni, na kubadilishwa kwa hali asili ya mahali pale, mistari ya 4-8; (4) kuanzisha ufalme, na baraka kamilifu katika ulimwengu, mistari ya 9-21 (Biblia ya kujifunza ya Scofield, chapa ya1917, uk. 978; maelezo kuhusu Zekaria 13:8).

Tawala za mataifa, zikiongozwa na Mpinga-Kristo, watatuma wanajeshi wao kushambulia Israeli katika bonde la Megido, inayojulikana kama Har-Magedoni. Wanajeshi wa Mpinga-Kristo watakaribia Yerusalemu, lakini Kristo atarudi ghafla kutoka mawinguni na kuwashinda. Tafadhali simama na usome Zekaria 14:3-4.

“Hapo ndipo atakapotokea BWANA, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita. Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini” (Zekaria 14:3-4).

Mnaweza kuketi.

Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni” (Zekaria 14:4). Mlima wa Mizeituni uko hasa mashariki mwa Yerusalemu. Huu ni ule Mlima wa Mizeituni mahali ambapo Yesu alienda kuomba usiku ule alikamatwa. Huu ni ule tu Mlima wa Mizeituni mahali ambapo Yesu alipaa mbinguni, kama ilivyoandikwa katika Matendo Ya Mitume 1:9-12.

“Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato” (Matendo ya Mitume 1:9-12).

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

“Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni” (Zekaria 14:4). Miguu ile ile iliyochomwa misumari msalabani itateremka katika ule mlima mahali ambapo alipaa kurudi mbinguni Matendo ya Mitume 1:9.

“Nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini” (Zekaria 14:4). Dkt. McGee alisema,

Tumetajiwa mabandiliko makuu yanayoenda kutendeka hapa. kutakuwa na mtetemeko mkubwa wa ardhi, na Mlima wa Mizeituni utagawanywa katikati. Nusu ya huo Mlima itaenda upande wa kasikasini na nusu nyingine itaenda upande wa kusini. “Na kutakuwa na bonde kuu” (J. Vernon McGee, Th.D., Kupitia Biblia, Kimechapishwa naThomas Nelson, 1982, sehemu ya III, uk. 986).

Basi,hilo ndilo jambo la kwanza – Kristo atarudi kupitia mawinguni katika Mlima wa Mizeituni.

II. Pili, Kristo atarudi pamoja na watakatifu Wake wote.

Tazama mwisho wa mstari wa tano.

“Na BWANA, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye” (Zekaria 14:5).

Hii ina maana kwamba Wakristo wote walionyakuliwa watateremka kutoka mawinguni, wakimfuata Kristo, kuelekea Mlima wa Mizeituni. Tukio hili lilitabiriwa mara ya kwanza na Henoko.

“Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adam, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu, maelfu” (Yuda 14).

Na Mtume Yohana alilizungumzia hili jambo katika Ufunuo 19:14, “Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata,” anapoteremka kuelekea Mlima wa Mizeituni kuliaribu jeshi la Mpinga-Kristo. Dkt. Yeremia alisema,

Jeshi la mbinguni litakaloandamana na Kristo katika kuja Kwake mara ya pili litajumlisha watakatifu na malaika – watu kama wewe na mimi tukisimama pamoja na viumbe vya mbinguni vilivyo na nguvu nyingi mno…hawatapigana. Yesu Mwenyewe atawauwa waasi (Daudi Yeremia, ibid., uk. 224).

“Na BWANA, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye” (Zekaria 14:5).

Dkt. McGee alisema,

Huu ni mstari wa kupendeza katika Maandiko. Ni picha ya Bwana Yesu Kristo akirudi duniani. Tunapata hili pia katika Ufunuo 19 mahali ambapo tunaambiwa ya kwamba jeshi la mbinguni litamfuata (J. Vernon McGee, ibid.).

Hili ndilo jambo la pili mhimu katika unabii wa Zekaria – Kristo atarudi pamoja na watakatifu Wake wote kulishinda jeshi la Mpinga-Kristo. Waongofu wa kweli wote, katika vizazi vyote, watarudi pamoja na Kristo duniani wakati huo.

Elfu kumi mara elfu kumi
   Wamevaa mavazi yanayometameta,
Jeshi la watakatifu waliookolewa
   Waliosongamana katika mtelemko wa nuru;
Yameisha, yote yameisha,
   Vita vyao dhidi ya kifo na dhambi;
Ifungue wazi milango ya dhahabu,
   Waache washindi waingie.
(“Elfu Kumi Mara Elfu Kumi” na Henry Alford, 1810-1871).

Yohana Cennick na Charles Wesley waliandika,

Tazama! Anateremka akija katika mawingu,
   Alichinjwa mara moja kwa wokovu wetu;
Maelfu na maelfu ya watakatifu pamoja Naye,
   Wamefurika katika mfululizo wa ushindi Wake;
Haleluya! Haleluya!
   Mungu amekuja duniani kutawala.
(“Tazama! Anakuja” na Yohana Cennick, 1718-1755;
      Uliogeuzwa na Charles Wesley, 1707-1788).

III. Tatu, Kristo atarudi kuanzisha Ufalme Wake duniani.

Tafadhali simama na usome Zekaria 14:9 kwa sauti.

“Naye BWANA atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja” (Zekaria 14:9).

Unaweza kuketi. Kristo atakuwa mfalme duniani kote siku hiyo. Hatimaye, Maombi ambayo Wakristo wameomba kwa miaka elfu mbili yatajibiwa,

“Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni” (Mathayo 6:10).

Na Ufalme Wake hapa duniani utadumu miaka elfu moja. Tafadhali fungua Ufunuo, sura ya 20, mstari wa 4 hadi 6. Soma mistari hiyo kwa sauti.

“Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu, na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu” (Ufunuo 20:4-6).

Mashahidi wa Yehova wanaamini katika miaka 1,000 ya Ufalme. Lakini hawajui jinsi ya kuingia katika ule Ufalme! Katika afisi yangu ninacho chuo cha mahubiri ya Mashahidi wa Yehova kilicho na kichwa cha “Mateso yote yataisha hivi karibuni!” Katika mwisho wa chuo hicho kuna haya maneno, “Mwisho unapokuja, ni nani atakayebaki?...ni wale wanajifundisha mapenzi ya Yehova na kuyatenda” (“Mateso yote yataisha hivi karibuni!,” Jamii ya Mnara wa Zamu kwa Biblia na chuo ya Pennsylvania, 2005, uk. 6). Hivyo, Mashahidi wa Yehova wanafundisha kwamba kuingia katika Ufalme ni “kujifundisha” ukweli wa Mungu “na kuufanya.” Hilo ni kosa kubwa. Ni kosa la wokovu kwa matendo – wokovu kwa “kujifundisha” jambo na “kulitenda” jambo hilo! Ajabu ni kwamba, kosa la Mashahidi wa Yehova linafanana na lile la Wakatoliki ambalo wanazungumza kinyume nalo kila mara. Wakatoliki na Mashahidi wa Yehova wote ufundisha wokovu kupitia matendo, wokovu kwa kujifundisha na kutenda!

Lakini Biblia yenyewe ufundisha wokovu kwa neema, si kwa kujifundisha na kutenda; si kwa bidii ya mwanadamu, lakini kwa neema pekee.

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asiye akajisifu” (Waefeso 2:8-9).

Yohana Newton alisema,

Neema ya ajabu! Sauti iliyotamu aji
   Iliyomwokoa mwovu kama mimi!
Nilikuwa nimepotea, lakini sasa nimepatikana;
   Nilikuwa kipovu, lakini sasa ninaona.

Ni neema iliyoufundisha moyo wangu kuogopa,
   Na neema iliondoa woga wangu;
Kwa njia ya thamani neema ilipatikana
   Wakati kwanza nilipoamini!
(“Neema ya Ajabu” na Yohana Newton, 1725-1807).

Na Mungu akupe neema kulipokea andiko hili

“Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka” (Matendo ya Mitume 16: 31).


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Jack Ngann:
“Anarudi tena” (na Mabel Johnston Camp, 1871-1937).


MWONGOZO WA

JINSI KRISTO ATAKAVYOANZISHA
UFALME WAKE DUNIANI

HOW CHRIST WILL SET UP HIS EARTHLY KINGDOM

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

“Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini. Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la mlima yangu; kwa maana bonde lile la mlima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na BWANA, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye…Naye BWANA atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja” (Zekaria 14:4-5, 9).

I.   Kwanza, Kristo atarudi katika Mlima wa mizeituni,
Zekaria 14:3-4; Matendo ya Mitume 1:9-12.

II.  Pili, Kristo atarudi na watakatifu Wake wote, Zekaria 14:5;
Yuda 14; Ufunuo 19:14.

III. Tatu, Kristo atarudi kuanzisha Ufalme Wake hapa duniani,
Zekaria 14:9; Mathayo 6:10: Ufunuo 20:4-6;
Waefeso 2:8-9; Matendo ya Mitume 16:31.