Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




BIBLIA NA WASALITI WA KANISA

THE BIBLE AND TRAITORS TO A LOCAL CHURCH
(Swahili)

Mahubiri yaliyoandikwa na Dkt. R. L. Hymers, Jr.
na kuhubiriwa na Kasisi Yohana Samweli Cagan
katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana asubuhi ya, Novemba 4, 2018
A sermon written by Dr. R. L. Hymers, Jr.
and preached by Rev. John Samuel Cagan
at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Morning, November 4, 2018

“Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu” (I Yohana 2:19).


Albert Camus na Jean-Paul Sartre ni wana falsafa wawili walioeneza udhanaishi. Fikira za watu wengi ziko chini ya misingi ya falsafa yao siku ya leo, ingawa pengine hawatambui hivyo. Dkt. R. C. Sproul alisema, “Tunakutana na ushawishi wa udhanaishi karibu kila siku katika kila eneo la tamaduni zetu…tunaishi chini ya ushawishi wa udhanaishi kila siku” (Dkt. R. C. Sproul, Maoni ya maisha, Fleming H. Revell, 1986, uk. 49).

Msingi wa mada ya udhanaishi wa Camus na Sartre usisitiza “msingi wa upweke wa mwanadamu katika ulimwengu usiomcha Mungu” (Dkt. John Blanchard, Does God Believe in AtheistsJe! Mungu ana Amani wasiomwamini Mungu?, Evangelical Press, 2000, uk. 138).

Je! R. C. Sproul yuko sahihi anaposema tunaishi “chini ya ushawishi” wa falsafa hii “kila siku”? Ndiyo, Nafikiria hivyo. Hiyo ndiyo sababu mada hii ya upweke ina mvuto wa kina, hasa kwa vijana. Bila kutambua falsafa hii ilitoka wapi, or who said itama ni nani aliyesema hivyo, bado unaihisi – “msingi wa upweke wa mwanadamu katika ulimwengu usiomcha Mungu.” That phrase has a ring of truth to itMsemo huo una ukweli unaouandama. Kila kijana ameuhisi – “msingi wa upweke wa mwanadamu katika ulimwengu usiomcha Mung.”

Na unaweza kujisikia upweka katika chumba ambacho kimejaa watu. Unaweza kuwa katika hafla, au katika soko iliyo na watu wengi, na bado ujihisi upweke. Kijana mmoja alimwambia Mchungaji wetu, Dkt. Hymers, “Najihisi upweke sana na sijui nitafanya nini.” Wiki chache baadaye alijiua. Na vijana wengi wanasumbuliwa na hisia za upweke siku ya leo. Ni matokeo ya udhanaishi ambayo yamepenya “kila nyanja ya utamaduni wetu.”

Upweke ndilo tatizo, lakini dawa ni nini? Tiba ni nini? Tuba ni kumjua Yesu Kristo kibinafsi – na kuwa sehemu ya jamii ya Mungu katika kanisa fulani. Tunatoa jawabu la hofu inayoletwa na udhanaishi, “Kwa nini uwe na upweke? Kuja nyumbani– kwa kanisani! Kwa nini upotee? Kuja nyumbani – kwake Yesu Kristo, Mwana wa Mungu!” Tunatoa jibu kwa Camus, na Sartre, na kwa udhanaishi kwa jumla tunaposema hivyo! Tunatoa jibu kwa uchungu, lonelyupweke, na kutengwa ambako hakuna maana kwa dunia ya kisasa tunaposema hivyo! Itamke kwa sauti! Inongone! Tell it far and wideIseme kwa marefu na mapana! Kwa nini uwe na upweke? Kuja nyumbani – kanisani! Kwa nini upotee? Kuja nyumbani – kwake Yesu Kristo, Mwana wa Mungu!

Lakini kuna wengine ambao wanataka jambo moja bila kutaka lile lingine. Wanataka urafiki katika kanisa wanaloshiriki bila kumgeukia Yesu Kristo. Lakini mwishowe haitafanya kazi. Mambo haya yanapaswa kuambatana. Hivyo ndivyo ilivyo katika Ukristo – urafiki kanisani na kumgeukia Kristo uambatana pamoja. Huwezi kuwa na moja pasipo lile lingine!

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

Hivi ndivyo inavyo tendeka unapojaribu kuwa na urafiki bila uongofu. Hatimaye urafiki utavujika. Hivi karibuni au baadaye haitafanya kazi. Hayo ndiyo somo hili letu linazungumzia leo.

“Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu” (I Yohana 2:19).

Dkt. W. A. Criswell alisema, “Wengine waliondoka makanisani…Kutoka kwao hakika kulidhihirisha kwamba imani inayookoa, na hivyo, ushirika halisi haukuwepo” (Biblia ya Kujifunza ya Criswell, maelezo juu ya I John 2:19). Hapa kuna tafsiri ya kisasa ya I Yohana 2:19,

“Watu hao wametokea kati yetu lakini hawakuwa kweli wa kwetu na ndiyo maana walituacha; Kama wangalikuwa wa kwetu, wangalibaki nasi. Lakini waliondoka, wakaenda zao, kusudi ionekane wazi kwamba hawakuwa kamwe wa kwetu” (I Yohana 2:19).

Wacha tufikirie kuhusu maneno haya kwa kina.

I. Kwanza, kile walichofanya.

Dkt. Criswell alisema, “Wengine walikuwa wameondoka kanisani.” Bila shaka walikuja makanisani kwa sababu walifurahia ushirika. Makanisa ya kwanza yalikuwa mahali pa urafika wa kina wakati wa ulimwengu wa Warumi uliokuwa mwovu na usiokuwa na huruma. Watu walipenda ukunjufu na urafiki waliopata kanisani,

“wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote” (Matendo ya Mitume 2:47).

Lakini waligundua ya kwamba maisha ya Ukristo si rahisi kila wakati. Wengine wao waliondoka walipogundua hivyo. Mtume alisema,

“Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia. Luka peke yake yupo hapa pamoja nami” (II Timotheo 4:10-11).

Dema, Kreske na Tito waliondoka matatiso yalipokuja.

Hiyo inatendeka leo? Ndio inatendeka. Watu huja kanisani kwa muda. Wanafurahia urafika wanaofanya kanisani. Huonekana jambo la kufurahia. Lakini baandaye jambo linguine linatokea. Nilisikia kuhusu mtu mmoja aliyeenda Las Vegas Juma pili asubuhi. Mtu huyo alipenda kuja kanisani, lakini Las Vegas ilionekana mahali pa kufurahia zaidi! Wengine wanavutwa na sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya. Wanajaribiwa na tafrija za dunia na sikukuu – na hivyo wanaondoka kanisani. “Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu” (I Yohana 2:19).

II. Pili, kwa nini walifanya hivyo.

Somo letu linasema, “Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi” (I Yohana 2:19). Anapoeleza juu ya I Yohana 2:19, Dkt. J. Vernon McGee alisema,

Jinsi unavyoweza kumjua mtoto wa Mungu wa kweli ni kwamba hatimaye mtu atajidhihirisha na ataondoka katika makutano ya Mungu ikiwa yeye si mtoto wa Mungu. ChristiansAtajiondoa kutoka kwa Wakristo, mwili wa waumini, na ataenda…duniani alikotoka…Kuna wengi wanaokiri kwamba wao ni Wakristo, lakini kwa kweli wao sio Wakristo (J. Vernon McGee, Th.D., Kupitia Biblia, Wachapishaji waThomas Nelson, 1983, sehemu V, uk. 777).

Nitakupatia bila kuongeza chochote maneno yaliyosemwa na Albert Barnes, katika mafafanusi yake ya Biblia,

Maana kama wangalikuwa wa kwetu. Ikiwa walikuwa Wakristo waaminifu na wa kweli. Bila shaka wangeendelea kuwa pamoja nasi…Kama wangekuwa Wakristo wa kweli hawangeondoka kanisani. Anatamka tamko hili kwa upana kiasi cha kwamba linastahili lichukulewe kama ukweli wa ulimwengu wote, kwamba ikiwa kuna yeyopte kwa ukweli ‘ni wetu,’ yaani, ikiwa wao ni Wakristo wa kweli, wataendelea kuwa kanisani, au hawataanguka. Tamko hili limetamkwa pia kufundisha ya kwamba ikiwa yeyote atatoka kanisani, ukweli unaodhihirika ni kwamba hawakuwa waumini wa dini, kwa maana kama wangekuwa hawangeliondoka kanisani (Albert Barnes, Maelezo juu ya Agano Jipyat, Baker Book House, 1983 chapa ya pili ya toleo 1884-85, maelezo juu ya I Yohana 2:19).

Yesu alisema,

“Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga (Luka 8:13).

III. Tatu, jinsi ya kurekebisha.

“Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu” (I Yohana 2:19).

Matthew Henry alisema,

Ndani yao hawakuwa kama vile tulivyo; Lakini hawakuwa wetu; hawakuyatii mafundisho mazuri waliyohubiri katika mioyo yao; hawakuwa wa muungano wetu na Kristo aliye kichwa (Mafafanusi ya Biblia nzima ya Matthew Henry, Hendrickson, 1996 reprint, sehemu 6, uk. 863).

Hawakuwa wameunganika na Kristo. Hawakuwa “wa kwetu.” Dkt. McGee alisema haya kuhusu mstari huu,

Yohana amesimulia hapa maneno mazito yaliyo na taratibu za Mungu, na anayasema haya maneno kwetu leo. Bwana Yesu alimwambia mtu aliyekuwa wa dini, Nikodemo, ya kwamba lazima azaliwa mara ya pili. Alimwambia… “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu ” (Yohana 3:3). Yohana anasema hapa, “Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu.” Walionekana kama walikuwa wana wa Mungu wa kweli, lakini kwa hakika hawakuwa (J. Vernon McGee., ibid.).

Ni lazima uzaliwe mara ya pili ili uwe “wa kwetu,” kama alivyosema Dkt. McGee. Ni lazima uunganike na Kristo. Hii inatendeka unapokuwa kwa hakika umezaliwa mara ya pili. Yesu alisema,

“Hamna budi kuzaliwa mara ya pili” (Yohana 3:7).

Marekebisho ya ukengeufu ni ni kuzaliwa upya! Hii inatendeka unaposadiki dhambi zako na kuja kwa Kristo. Unapokuja Kwake, Atakupokea na kusiosha dhambi zako na Damu Yake. Unaweza kumwamini, kwa sababu alisema,

“wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe” (Yohana 6:37).

Unapokuja kwa Kristo, na kuungana Naye, unapokea maisha mapya. Dhambio zako zinafutwa, na unafanyika mwana wa Mungu. Ni wakati tu unapozaliwa mara ya pili ndipo unapofanyika kwa hakika mshirika aliyehai wa kanisani mahali unaposhiriki. Udhanaishi unatupiliwa mbali unapokuja kwa Kristo na kuokoka. “Man’s fundamental loneliness in a godless world” inarekebishwa na kutibia unapokutana na Kristo aliyefufuka kutoka kwa wafu, na matokeo ni kwamba utakuwa sehemu iliyo hai ya kanisa unaloshiriki. Yesu alisema,

“wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe” (Yohana 6:37).

Kwa nini upotee? Kuja nyumbani – kwake Yesu Kristo, Mwana wa Mungu!

Charles Spurgeon alihubiri ujumbe ulio na kichwa cha “”Uzima uliothibitishwa na upendo.” Msingi wa mahubiri hayo ulikuwa I John 3:14,

“Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu” (I Yohana 3:14).

Spurgeon alisema,

Hadi utakaposaliwa mara ya pili, hautawahi kuelewa maana ya neema ya Mungu. Lazima upokee uhai mpya, upite toka mautini kuingia uzimani, ama hautajua mambo haya… “unajua ya kwamba tumetoka mautini na kuingia uzimani, kwa sababu tunapenda ndugu kanisani Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu.” Hivyo, ndugu, ikiwa tunaweza kusema tunawapenda watu wa Mungu, kama watu wa Mungu, kwa sababu ni watu wa Mungu, hiyo ni ishara ya kwamba tumepita toka mautini kuingia uzimani (C. H. Spurgeon, “Uzima uliothibitishwa na upendo,” The Metropolitan Tabernacle Pulpit, Chapisho laPilgrim, 1976 chapa ya pili, sehemu XLIV, uk. 80-81).

Tunapopita toka mautini kuingia uzimani kupitia uongofu, tutawapenda ndugu kanisani!

Ikiwa unadhamini urafiki ambao umefanya katika kanisa hili, hakikisha umepokea uongofu. Ni lazima uongoke. Kristo ndiye “gamu” inayaoshikamanisha ushirika kanisani!


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Jack Ngann:
“Amebarikiwa Anayepatanisha” (na John Fawcett, 1740-1817).


MWONGOZO WA

BIBLIA NA WASALITI WA KANISA

THE BIBLE AND TRAITORS TO A LOCAL CHURCH

Mahubiri yaliyoandikwa na Dkt. R. L. Hymers, Jr.
na kuhubiriwa na Kasisi Yohana Samweli Cagan

“Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu” (I Yohana 2:19).

I.   Kwanza, kile walichofanya, Matendo ya Mitume 2:47;
II Timotheo 4:10-11.

II.  Pili, kwa nini walifanya hivyo, Luka 8:13.

III. Tatu, jinsi ya kurekebisha, Yohana 3:3, 7; 6:37; I Yohana 3:14.