Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.
KWA NINI TUNAFANYA VILE TUNAVYOFANYA
– KATIKA UINJILISTI

WHY WE DO WHAT WE DO – IN EVANGELISM
(Swahili)

Mahubiri yaliyoandikwa na Dkt. C. L. Cagan
na kuhubiriwa na Kasisi Yohana Samweli Cagan
katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana asubuhi ya, Octoba 28, 2018
A sermon written by Dr. C. L. Cagan
and preached by Rev. John Samuel Cagan
at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Morning, October 28, 2018

“Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani” (Luka 14:23).


Tunafanya uinjilisti unaoleta watu kanisani kwetu kusikia Injili. Katika makanisa menggine, washirika uomba “ombi la mwenye dhambi” na watu barabarani halafu wanawaalika kanisani baada ya kufanya huo “uamuzi.” Lakini jambo la kwanza tunalolifanya ni kuwaalika watu kanisani. Halafu tunawaleta kanisani. Wanapokuja, wanafanya urafiki na watu kanisani. Wanasikia Injili ikihubiriwa. Wengine wao wanakaa na wanamwamini Kristo. Wanakuwa Wakristo wa ajabu. Utaratibu huu mpya ulitoka kwa Mchungaji, Dkt. Hymers. Alianzisha utaratibu huu kwa sababu aligundua kwamba mifumo mingine ilishindwa kuwaleta watu waliopotea kanisani kwetu.

Utaratibu wa Dkt. Hymers ni upi? Ni nini tunayofanya katika uinjilisti? Jumatano usiku, Alhamisi usiku na wakati mwingine huenda wawili wawili katika vyuo, nyumba za biashara na sehemu zinginezo zinazokaa watu katika maeneo ya Los Angeles. Wengine wetu tunafanya hivi kwa hiari yetu. Katika sehemu hizi, tunawaendea watu na kuzungumza nao. Huwa hatujaribu kuwafanya kumwamini Kristo hapo kwa hapo. Hatuwaongozi kusema “ombi la mwenye dhambi”. Badala ya hiyo, tunawaambia jinsi kulivyo kanisani kwetu. Kule kanisani kuna wavulana na wasichana amabao wanaweza kufanya urafiki nao. Watasikia mahubiri. Watakula chakula cha mchana (ikiwa watakuja asubuhi) ama chakula cha njioni (ikiwa watakuja njioni). Wataona sinema. Watakuwa katika sherehe – tutasherehekea siku ya kuzaliwa ya kila mmoja kanisani kwetu. Watakuwa na wakati mzuri. Wengi wao wanataka kuja!

Halafu tunawauliza watupatie jina lao la kwanza na nambari ya simu. Baadaye, tunapeyana majina yao na nambari zao za simu kwa mashemasi na Wakristo watenda kazi kanisani walio na uzoefu. Watenda kazi hawa huwapigia hawa watu simu, wanawaambia kuhusu kanisa letu, wanawaalika waje, na wanapanga jinsi ambavyo wanaweza saidiwa kuja Jumapili na mmoja wa washirika wetu. Siku ya Jumapili, tunawachukua, tunawaleta kanisani, na tunawapeleka nyumbani. Watu wengi huja Jumapili ya kwanza baada ya kupigiwa simu. Wengine wanakua na shughuli siku hiyo na wanakuja baadaye. wanapokuja kanisani, wanasikia injili ikihubiriwa na wanakuwa na wakati mzuri wa kupata marafiki katika chakula na katika sherehe baadaye – na wengi wao huja tena!

Utaratibu huu unafanikiwa! Katika majuma machache yaliyopita, zaidi ya watu mia moja walikuja kanisani kwetu mara ya kwanza, ya pili au ya tatu. Na wengine wao hukaa kanisani na kumwamini Kristo. Utaratibu huu kwa hakika huleta watu kanisani kwetu. Ni utaratibu unaofanikiwa!

Dkt. Hymers aliuleta utaratibu huu tunaotumia kufanya uinjilisti kwa kufuata kile Yesu alisema katika Luka 14:23, “Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani.” Kwanza, tunawaleta watu waliopotea kanisani. Na huko wanasikia Injili na kumwamini Kristo. Makanisa ya siku hizi ya Marekani wanafanya haya kwa kurundi nyuma. Wanawaongoza watu kwa “uamuzi” wa haraka kule barabarani. Lakini karibu wote hakuna atakayekuja kanisani. Utaratibu wao unaleta tu maamuzi, si wongofu. Leo nataka kueleza ni kwa nini tunafanya uinjilisti kwa njia inayotofautiana na yao.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

Kwa nin tunatoka kule nje kupata majina ya watu na kuwaalika kanisani, na hatujaribu kuwafanya watu waokoke tunapoongea na wao?

Kwanza, ni kwa sababu njia yetu ni ya Kibiblia. Inapatikana kila mahali katika Agano Jipya. Andrea alikuwa mmoja wa wale Wanafunzi kumi na wawili. Biblia inasema,

“Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu. Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe)” (Yohana 1:40-42).

Andrea hakuiua chochote. Lakini alijua Yesu ni Masihi. Andrea hakuzunguka akiwaongoza watu kwa ombi la mwenye dhambi. Lakini alimleta ndugu yake Simoni Petro kwa Yesu. Petro akawa Mwanafunzi mwenyewe. Baadaye Petro akaongoka na akahubiri siku ya Pentekoste wakati ambapo watu elfu tatu walimwamini Kristo. Lakini hiyo ilianza wakati alipomfuata ndugu yakee na kukutana na Yesu.

Mwanafunzi Filipo alisema jambo lilelile kwa Nathanaeli. Alimwambia Nathanaeli, “Njoo uone” (Yohana 1:46). Filipo hakujua mambo mengi. Lakini alimleta Nathanaeli kumwona Yesu, na hilo ndilo lilileta utofauti.

Siku moja Yesu alipitia Samaria na akamwongoza mwanamke kwa wokovu. Hakujua Biblia. Hakuwa Myahudi. Lakini alimwamini Yesu. Mwanamke huyu hakwenda kwa kijiji chao na kuwaongoza watu kusema ombi la mwenye dhambi. Lakini aliwaalika watu ili waende kwamwona Yesu. Biblia inasema,

“Basi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu, Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo?” (Yohana 4:28, 29).

Kila mmoja anaweza kufanya hivyo – hata ingawa bado haujaokoka. Hauhitaji kwenda kwa darasa na kujifundisha mafundisho ya Biblia. Haujaribu kujibu maswali ya watu. Haujaribu kuwafanya waokoke kule barabarani. Wewe tu unawaalika waje kanisani, wafanye urafiki na watu huko na wawe na wakati mzuri. Kila mmoja anaweza kufanya hivyo – na huwa tunafanya hivyo.

Pili, ni kwa sababu utaratibu huu wetu unafaulu. Makanisa mengi hayafanyi uinjilisti kabisa. Lakini ikiwa wanafanya, wanaenda kuwaongelesha watu kule barabarani au katika milango yao. Kwa haraka wanawapa watu waliopotea “mpango wa wokovu” na kuwauliza waombe “ombi la mwenye dhambi” hapo hapo. Haya ni “mahamuzi.” Mtu yule ambaye amefanya “uamuzi” anahesabiwa kama mwongofu. Wanamhesabu huyo mtu kama “aliyeokoka”. Baada ya hiyo, makanisa “wanawafuata” hawa watu – Lakini wengi wao hawakuji kanisani. Babangu, Dkt. Cagan alitembelea kanisa lenye misingi ya Kibaptisti waliokuwa wameomba na zaidi ya watu 900 kwa wiki moja – lakini kanisa lilikuwa tu na watu 125. Wale 900 walifanya uamuzi, lakini hawakuwahi kuja kanisani. Waliomba ombi, lakini hawakuja kwa Kristo.

Kwa nini hatufanyi vile haya makanisa wanavyofanya? Njia hii haifaulu. Washirika wa haya makanisa wanawaongoza mamia ya watu kuomba ombi la mwenye dhambi. Lakini karibu wote hakuna aliyekuja kanisani. Hawakufanyika kuwa Wakristo. Walifanya “uamuzi” lakini hawakuongoka.

Kwa nini hatujaribu kuwafanya wenye dhambi Wakristo hapo hapo tunapoongea na wao? Kwa sababu hawafanyiki Wakristo! Badala ya hivyo, tunatoka nje na kuwaalika watu kanisani kwetu. Tunawauliza watupe jina lao la kwanza na nambari ya simu. Mashemasi wetu na viongozi kanisani wanawapigia na kupanga na wao jinsi watakavyo wasaidia kuja kanisani Jumapili. Tunawabeba na magari yetu na kuwaleta kanisani. Tunafanya urafiki nao. Kila mara tuna chakula cha mchana baada ya ibada yetu ya asubuhi, na chakula cha jioni baada ya ibada yetu ya jioni. Tunawafanya wafurahie wakiwa kanisani. Halafu mashemasi wetu na wafanyi kazi huwapigia simu na kuwaalika waje tena.

Kwa nini tunafanya tunachokifanya? Kwa sababu njia hii inafanya kazi. Utaratibu huu wetu huwaleta watu kanisani, na kukaa kanisani. Kanisani wanasikia mahubiri ya Injili. Watu wengine humwani Kristo mara hiyo, lakini wengi wao wanahitaji kusikia Injili kwa majuma au miezi kabla hawajaongoka. Halafu wanakaa kanisani kama Wakristo maisha yao yote. Utaratibu huo mwingine ni desturi ya usemi ambayo haiwezi kumwokoa yeyote!

Miezi michache iliyopita nilienda Afrika tukiwa na babangu Dkt. Cagan na Nuhu Sang. Tulihubiri makanisani kule Uganda, Kenya na Rwanda. Kule Kenya tulihubiri katika kongamano la Wachungaji. Mkutano ulimalizika alasiri. Dkt. Cagan akawaambia Wachungaji, “Twendeni nje tupate majina ya watu.” Tulienda katika barabara za Nairobi, tukiwa na Wachungaji waliokuwa wakitafsiri kwa Kiswahili. Tuliongea na watu na tukapata namba zao za simu. Tuliwaalika kanisani. Wachungaji waliwapigia simu na wakapanga nao wakuje kanisani. Walikuwa na wageni watano siku iliyofuatia! Tulipoenda Rwanda, Wachungaji walifanya hivyo tena na wakawa na wageni wengine watano Jumapili iliyofuatia!

Wahubiri walisisimuka. Walipata utaratibu unaofaulu! Walituambia ya kwamba walifanya juhudi nyingi na kutumia pesa nyingi kuwa na mikutano ambapo watu walifanya uamuzi, lakini hakuna yeyote kati yao alikuja kanisani. Wachungaji wakafikiria hiyo ndiyo njia ya pekee ya kufanya uinjilisti. Walifurahia kujua huu utaratibu wetu, ambao kwa hakika huwaleta watu kanisani.

Tatu, Utaratibu wetu ni mzuri kwako, si tu kwa wale ambao wamealikwa. Hii itakufanya Mkristo mwenye nguvu unapofanya uinjilisti mara kwa mara. Na hii itaimarisha imani yako unapoona watu uliowaalika wakija kanisani, na kukaa kanisani, na kumwamini Kristo. Kuna furaha ya ajabu unapomuona mtu uliyemualika akija kanisani. Kuna furaha kuu unapowaona wakiokoka. Nakutakia hiyo furaha!

Kwa nini hatupeyani vijikaratasi vilivyo na maelezo yetu? Watu wengine hupeyana. Pengine haujui vijikaratasi hizi ni nini. Vijikaratasi hizi ni kipande cha karatasi, kwa kawaida huwa zimekujwa, ambazo hupeyanwa nyingi kwa yeyote anayehitaji. Vijikaratasi hizi huwa na hadithi na mpango wa wokovu. Mwisho wa hicho kijikaratasi mtu huulizwa kumwamini Kristo kwa kuomba ombi ama kuliandika jina lake kwa kile kijikaratasi.

Makanisa mengi yanao watu wanaopeyana hizi vijikaratasi. Wanafikiria wanawaleta watu kwa Kristo. Lakini karatasi hizi hasiwaleti watu kwa Kristo. Hasiwaleti kanisani. Watu hao wako wapi? Vijikaratasi hizi ni vya kupoteza muda na pesa. Na hiyo ndiyo sababu hatusisambazi.

Tunajua aji? Tulijaribu. Tulisambaza vijikaratasi milioni moja. Watu walivisoma vile vijikaratasi. Lakini hakuna yeyote aliyekuja kanisani! Hawakuongoka walipovisoma vile vijikaratasi. Utaratibu huo si wa Biblia. Biblia haiwaambii Wakristo kuvisambaza hizi vijikaratasi. Lakini Biblia anasema ya kwamba twende nje na tuwahimize wenye dhambi wanje – katika kanisa! Na hivyo ndivyo tunavyofanya.

Ni kwa nini huwa tunaenda wawili wawili? Ni kwa sababu Yesu aliwatuma Wanafunzi Wake hivyo. Biblia inasema kwamba Kristo “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili” (Marko 6:7). Tena, Biblia inasema ya kwamba “Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.” (Luka 10:1).

Bila shaka, unaweza kwenda peke yako kufanya uinjilisti. Biblia haikatazi kamwe. Hakuna kosa unapoenda peke yako. Lakini mnapoenda wawili wawili ni njia ya Biblia, na hufaulu!

Kwenda wawili wawili huwaleta watu wengi kanisani. Katika Los Angeles na miji mingine mikubwa, watu huwa wanashuku. Hawataki kuongea na mtu ambaye hawamjui. Watu ambao ni vijana huwa wanawashuku watu ambao ni wazee. Wasichana huwashuku wavulana. Kuwa na watu wawili wakienda nje pamoja kutatuliza woga wao na wataleta majina mengi.

Kwenda wawili wawili itakuwa vizuri kwako. Unapoenda na Mkristo aliye na uzoefu, utajua jinsi ya kuwaalika watu kanisani na utafanya hivyo kwa mustarehe. Mwanzoni, unaweza kuwa na woga. Haujui la kufanya. Lakini unapoenda nje na mtu mwingine utajua jinsi ya kufanya hivyo. Na muda usiyo kuwa mrefu utayaleta majina wewe mwenyewe!

Mtakuwa na ushirika mzuri wa Kikristo. Unapomfanyia Yesu kazi ni jambo linalokuleta karibu na Wakristo unaofanya kazi nao. “Ushirika wa kikazi” ni ushiriki ulio mzuri kweli kweli.

Ni jinsi gani tunajua njia hiyo nyingine haifaulu? Tuliijaribu kwa miaka! Tulienda mlango kwa mlango na tukawaongoza watu kupitia mpango wa wakovu ulio katika vijikaratasi vilivyo na maelezo vya Billy Graham. Tuliomba ombi la mwenye dhambi nao katika milango yao, au barabarani. Tulisambaza vijikaratasi vilivyo na maelezo milioni moja. Lakini watu hawakuja. Hawa kuongoka. Njia hiyo haifaulu.

Lakini utaratibu wetu unafanikiwa! Tuko na kanisa katikati mwa mji wa Los Angeles. Los Angeles ni mji ulio na watu wasio amini Mungu na wenye uovu. Kila aina ya dhambi utendeka hapa. Watu wanajishughulisha na kazi na shule na marafiki. Kuna mambo mengi sana ya kusahaulisha watu, kama runinga na mtandao na simutamba na mengineo. Watu wachache sana uenda kanisani. Ni wachache mno walio Wakristo halisi. Tulijaribu kuwaongoza watu kwa maombi barabarani. Lakini njia hiyo haijengi kanisa. Haiwaleti watu kwa Kristo.

Tumejifunza kupitia uzoefu. Tulienda nje na tukawaalika watu kanisani. Halafu tukawaleta kanisani mahali ambapo wanaweza pata marafiki na kusikia Injili. Katika kanisa letu tumewapoteza watu kila Jumapili. Hawatoki katika makanisa mengine. Hawatoki katika jamii za Wakristo. Wanatoka kule duniani na dhambi zake zote. Na wengine wao hufanyika Wakristo wa ajabu. Hiyo ndiyo sababu kanisa letu ni la kiroho na changamfu. Utaratibu wetu huwafanya watu Wakristo halisi, na tunashukuru kwa ajili yao! Amina.


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Jack Ngann:
“Walete ndani” (na Alexcenah Thomas, karne ya 19).