Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




SIRI YA USHINDI KULE CHINA

(MAHUBIRI YALIYOHUBIRIWA KATIKA TAMASHA ZA WACHINA KATI YA MSIMU WA VULI)
THE SECRET OF SUCCESS IN CHINA
(A SERMON GIVEN AT THE CHINESE MID-AUTUMN FESTIVAL)
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana jioni ya, Septemba 30, 2018
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord's Day Evening, September 30, 2018

“Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri)…” (Ufunuo 2:9).


Wasifu wa mmoja wa waanzilishi wa Ukristo kule China Mchungaji Wang Mingdao alisema,

Haijalishi ni sera gani serikali ya China itafuata, kanisa la China litaathiri sura ya Ukristo duniani kote kwa vizazi vingi vijavyo. Kukiwa na [karibu] nafsi milioni sabini [kwa sasa milioni 160] na ongezeko la asilimia 7 kila mwaka, hesabu ya Wakristo kule China inashinda hesabu ya Wakristo katika mataifa mengi dunian. Kama walivyo Wakristo katika nchi zinazoendelea, Wakristo wa China wanawakilisha kundi la mbele [cheo cha mbele] cha kanisa katika karne ya ishirini na moja (Thomas Alan Harvey, Anayefahamu majonzi, Brazos Press, 2002, uk. 159).

Daudi Aikman, katika kitabu chake Yesu katika Beijing, alisema,

Ina maana kufikiria kwamba si tu hesabu, lakini kiini cha ueledi…cha Ukristo kinaweza ondoka kwa haraka kutoka Ulaya na Marekani ya Kasikasini unavyoendelea kuenea Ukristo katika China na China inapoendelea kuwa nchi yenye uwezo katika dunia…Mchakato unaweza kuwa tayari umeanza katika matumaini na kazi ya viongozi wa makanisa ya ndani ya nyumba kule China (David Aikman, Yesu katika Beijing, Regnery Publishing, 2003, uk. 291, 292).

Maelezo ya Kristo kuhusu kanisa la Smirna yanatoa picha nzuri ya jinsi mambo yalivyo katika maendeleo ya kanisa za “ndani ya nyumba” kule China siku hizi “,

“Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri)…” (Ufunuo 2:9).

Kuhusu kanisa la Smirna, Dkt. Yakobo O. Combs alisema,

Smirna, kasikasini mwa Efeso, kanisa lilochungwa kwa miongo kadhaa na Polycarp aliyefariki kama mfia dini mwaka wa 155 A.D. katika miaka yake ya 90…walivumilia mateso mengi na kunyanganywa mali zao, lakini walikuwa na utajiri wa kiroho (Yakobo O. Combs, D.Min., Litt.D., Upinde wa mvua kutoka Ufunuo, Tribune Publishers, 1994, uk. 33).

Kama kanisa la Smirna, Wakristo waaminifu wa makanisa ya dani ya nyumba kule China wana vumilia udhalimu mkuu na “taabu” na bado wao ni “matajiri” wa kiroho na uinjilisti wao unakua kwa kiasi cha asilimia “7 kwa mwaka” (Thomas Alan Harvey, ibid.). Hivyo, hesabu ya Wakristo kule China tayari “inashinda hesabu ya Wakristo katika mataifa mengi duniani.” Nafikiria ya kwamba wengi wa Wakristo walio zaidi ya 160 milioni ni waongofu halisi, na tayari kuna Wakristo wa kweli wengi kule China kuliko Marekani. Hii inashtusha! Lazima tujiulize, “Ni nini inayosababisha ushindi wao? Siri ya uinjilisti wao ni nini?” Kwa nini inaweza kusemwa juu yao,

“Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri)…”? (Ufunuo 2:9).

Tunapozingatia ukweli kwamba Ukristo wa kinjilisti haukui kabisa katika Marekani, na ukweli kwamba hata wengi wanasema Ukristo wa kiinjilisti hapa unafifia, Sisi hapa Marekani tunastahili kufikiria kwa kina ni nini hawana ambacho tuko nacho, na ni nini wakonacho ambacho hatuna.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

I. Kwanza, kile hawana ambacho tukonacho.

Hawana majengo ya kanisa! Ni kanisa tu la “Three-Self” liko na majengo. lakini “makanisa ya ndani ya nyumba” ndiyo yanayokua, na wako na majengo machache sana. Wengi wao hawana majengo ya kanisa kama sisi!

Hawana idhini ya serikali. Kila wakati wanadhulumiwa na serikali ya China. Hawana uhuru wa kuabudu kama sisi!

Hawana vyuo vya theolojia vya kufundisha Wachungaji kama sisi. Mafundisho ya pekee wanayopata Wachungaji kule China ni kwa nyumba ya mtu – na ni mafundisha mafupi na si ya kina. Wanapata tu mafunzo kidogo yanayopatikana “wakiwa mbiuni.”

Hawana majengo ya kufundishia watoto kanisani. Hawana mabasi ya “huduma za mabasi.” Hawana“RUNINGA za Kikristo.” Hawana “redio ya Kikristo.” Hawana makampuni ya ushapishaji ya Kikristo. Hawana vifaa vya “kuifadhi nishati.” Hawana vifaa vya kutupia picha ili kumwonyesha mhubiri katika skrini. Hawana “bendi za muziki wa Kikristo.” Hawana vyombo vya muziki, na kwa kawaida hawana piano. Hawana vitabu vilivyo chapishwa vya mafundisho ya watoto. Mara nyingi hawana Biblia kwa kila mmoja, ama vitabu vya nyimbo. Hapana, hawana vitu ambavyo tukonavyo! Badala ya hiyo, mara kwa mara wana dhuluma na mateso kutoka kwa serikali. Mara kwa mara wanafungwa gerezani kwa sababu tu ya kuwa Mkristo. Kila wakati kuna hilo tisho kwa kila mmoja anayekuwa Mkristo kwa kumaanisha! Tembelea www.persecution.com husome habari kuhusu dhuluma kwa Wakristo kule China. Na badoWakristo kule China wamefanikiwa kwa wingi kuhubiria nafsi zilizopotea. Hesabu ya Wakristo inaongezeka kila mahali kule China, katika ufufuo ulio mkuu katika hitoria ya kisasa!

“Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri)…” (Ufunuo 2:9).

Ninaogopa kwamba mengi ya makanisa katika Marekani yanaweza kuelezewa vizuri na kile Yesu alichosema kuhusu kanisa la Laodikea,

“Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi” (Ufunuo 3:17).

II. Pili, kile wanacho ambacho hatuna.

Hapa kuna yale waliyonayo ambayo hatuna. Na hapa ndipo kuna siri ya ushindi wao – na sababu ya kushindwa kwetu!

Wana mateso – na hivyo wanajifunza kubeba msalaba! Wakristo wengi wa Marekani hawataki kupoteza jioni hata moja kwa juma ili kwenda katika mkutano wa maombi. Wakristo wengi wa Marekani hawataki kupoteza hata jioni moja kila juma kwenda kuhubiria nafsi za watu. Wakristo wengi wa Marekani hawataki kupoteza starehe ya jumapili jioni kuwa kanisani! Wachungaji wengi katika Marekani wanahitaji kupunguza uzito. Tunahitaji tuwe na upungufu wa kalori. Lakini kule China wahubiri ni wembamba. Hivyo wanaweza kuhubiri kwa nguvu na ushupavu. Tunahitaji kupunguza uzito, ama hatuwezi kuhubiri kwa ushupavu. Kule China wana watu wembamba ambao wamejawa na Roho wanapo hubiri. Sijawahi kumuona mhubiri wa “kanisa za ndani ya nyumba” za China akiwa amepitiliza uzito. Si ajabu kwamba watu kule China wana ufufuo mkuu, wakati ambapo Ukristo unadidimia na kufifia hapa Marekani, na kila mahali katika nchi za magharibi! Inahitaji kiwango fulani cha mateso ili kufanya mazoezi. Inagharimu mateso kutumia chakula bora na kula chakula kichache hadi upunguze uzito! Inagharimu mateso kuwa aina ya mtu ambaye Mungu anataka uwe! Mwinjilisti mashuhuri wa China Dkt. John Sung alisema,

Mateso mengi huleta ufufuo mkuu…Mungu huwatumia kwa njia kuu…wale ambao wamenolewa kupitia mazingira magumu…Mateso mengi huleta manufaa mengi…Maisha ya wanafunzi yamelinganishwa na mizeituni: tunapotaabishwa zaidi, divyo mafuta mengi yatatoka ndani yetu. Ni wale tu wamepitia mateso wanaoweza kuonyesha huruma [upendo] na faraja kwa watu wengine (Yohana Sung, Ph.D., Jarida la waliopotea mara moja, Genesis Books, 2008, uk. 534).

Yesu alisema,

“ Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate” (Mathayo 16:24).

Tena, Yesu alisema,

“Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri)…” (Ufunuo 2:9).

Wana mateso kule China! Hivyo wana utajiri wa baraka za Mungu katika ufufuo! Hebu hapa kanisani kwetu tujikane, na tujitwike misalaba yetu na tumfuate Yesu – haijalishi inagharimu nini!

Pili, wana machozi wanapowaombea waliopotea! Ndugu mmoja, anayejua, aliniambia,“Kuna machozi mengi kule China.” Yuko sawa kabisa! Wanalia wanapowaombea waliopotea. Si ajabu kwamba kuna watu wengi wanaomwamini Kristo! Biblia inasema,

“Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha” (Zaburi 126:5).

Omba ya kwamba Mungu atakupa moyo uliovunjika kwa sababu ya nafsi zilizopotea! (nyote muombe).

Tatu, wanafanya lolote wawezalo kuwaleta waliopotea katika “makanisa ya ndani ya nyumba.” D. L. Moody alisema, “Wapende uwalete ndani.” Hiyo ndiyo njia wanayotumia kuwaleta watu katika makanisa ya ndani ya nyumba kule China – na hivyo ndivyo tunavyostahili kufanya! “Wapende uwalete ndani.” Kuwahubiria waliopotea hasa ni kuwapenda na kuwaleta ndani ya Kristo – na kuwaleta ndani ya kanisa. “Wapende uwalete ndani.” Huo si uhuria! Huo sio “mtindo wa maisha” wa uinjilisti! Huo ni wa D. L. Moody! Nafikiri alikuwa sawa kabisa. Huo mtindo unafanya kazi kule China – na huo mtindo utafanya kazi hapa! “Wapende uwalete ndani.”

Tukikimbia tunapofanya huduma hatutaweza kuwahubiria waliopotea. Ni wale tu wanaosalia wanaoweza kuhubiria nafsi zilizopotea. Ni wale tu wanaofanya urafiki na waliopotea kabla na baada ya kuwahudumia wanaoweza kuhubiria hizi nafsi. Hakuna njia nyingine ya kuwaleta waliopotea kanisani! Ni lazima “Tuwapende tuwalete ndani” – kama wanavyofanya kule China! Imba “Nifanye Mtiririko wa Baraka”! Ni nambari 4 katika karatasi yako ya nyimbo.

Nifanye mtiririko wa Baraka leo,
   Nifanye mtiririko wa baraka, Ninaomba;
Maisha yangu, huduma yangu iwe baraka,
   Nifanye mtiririko wa Baraka leo.
(“Ni fanya Mtiririko wa Baraka” na Harper G. Smyth, 1873-1945).

Si lazima nifunge ibada hii bila kuyasema maneno machache kwenu ambao hamjaongoka. Kuja kanisani haimaanishi umeongoka. Kusoma Biblia hakutakuokoa Ni lazima utubu dhambi zako. Ni lazima umgeukie Yesu Kristo na uje Kwake. Alikufa kwa uchungu na Damu Msalabani kuokoa nafsi yako. Ni lazima huoshwe uwe msafi kwa Damu Yake. Kuja kwa Yesu huokolewe kutoka kwa dhambi, mauti na Jahanamu. Na iwe hivyo kwako leo, ndio ombi langu. Amina.


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya Mahubiri na Bw. Benjamini Kincaid Griffith:
“Yesu ananipenda” (na Anna B. Warner, 1820-1915).


MWONGOZO WA

SIRI YA USHINDI KULE CHINA

THE SECRET OF SUCCESS IN CHINA

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

“Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri)…” (Ufunuo 2:9).

I.   Kwanza, kile hawana ambacho tukonacho, Ufunuo 3:17.

II.  Pili, kile wanacho ambacho hatuna, Mathayo 16:24;
Zaburi 126:5.