Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




JINSI YA KUIONGOZA NAFSI KWA KRISTO –
USHAURI KWA WONGOFU!

HOW TO LEAD A SOUL TO CHRIST –
COUNSELING FOR CONVERSIONS!
(Swahili)

Mahubiri yaliyoandikwa na Christopher L. Cagan, Ph.D. (UCLA),
M.Div. (Talbot Seminary), Ph.D. (Chuo cha Claremont Graduate School),
na kuhubiriwa na Kasisi Yohana Samweli Cagan
katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Asubuhi ya, Agosti 26, 2018
A sermon written by Christopher L. Cagan, Ph.D. (UCLA), M.Div. (Talbot Seminary), Ph.D. (the Claremont Graduate School), and preached by
Rev. John Samuel Cagan at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Morning, August 26, 2018

“Msipoongoka-----hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”
(Mathayo 18:3).


Yesu alisema ni lazima mtu aongoke – aongoke – la sivyo hawezi kuingia mbinguni. Neno la Kiyunani lililotafsiriwa “ongofu” ni “epistrepho.” Inamaanisha “kugeuka.” Hii si kuomba ombi la mwenye dhambi ama kuinua mkono. Haya ni mabadiliko ya moyo Mungu anayempa mwenye dhambi anapozaliwa mara ya pili. Yesu alimwambia Nikodemo, “Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa upya hataweza kuuona ufalme wa Mungu” (Yohana 3:3). Tena, Kristo alisema, “ni lazima kuzaliwa upya” (Yohana 3:7). Haya ni mabadiliko halisi ya moyo. Biblia inasema, “Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, mapya yamekuja” (II Wakorintho 5:17). Hii si kuomba tu maombi ya mwenye dhambi. Huu ni uongofu! Asubuhi ya leo ningependa kuzungumzia jinsi ya kumshauri mwenye dhambi ili kumuongoza kwa Kristo.

Wongofu ni nini? Ni kipi tunahitaji kitendeke? Mwenye dhambi anahitaji wongofu, si uamuzi. Tangu wakati wa Charles Finney (1792-1875) “Maamuzi” yamechukua nafasi ya wongofu katika makanisa mengi duniani kote. Mamilioni ya watu wamefanya uamuzi, lakini hawajaongoka.

“Maamuzi” ni nini? Wongofu ni nini? Haya ndiyo maelezo kutoka kwa kitabu kitwacho Mkengeuko wa leo, kilichoandikwa na Dkt. Hymers na babangu, Dkt. Cagan.

      Maamuzi ni imani kwamba mtu ameongoka kwa kuja mbele, kuinua mkono, kuyasema maombi, kuamini mafundisho, kuyasema maneno ya kujitolea ama mambo mengine ya nje, matendo ya mwanadamu, ambayo yanachukuliwa kuwa sawa na, na ushahidi wa, mujiza wa wongofu ulio ndani; ni lile wazo kwamba mtu anaokolewa kwa njia tu ya kufanya maamuzi ya nje; imani kwa kufanya mojawapo ya haya mambo ya kibinadamu inayoonyesha ya kwamba mtu ameokolewa.
      Wongofu ni matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu anayemvuta mwenye dhambi kwa Yesu Kristo ili kuhesabiwa haki na kuzaliwa upya, na ubadilisha hali ya mwenye dhambi mbele za Mungu kutoka kwa aliyepotea na kuwa aliyeokolewa, kushirikisha maisha ya kiungu kwa aliyepotea, hivyo kutoa mwongozo mpya katika maisha ya aliyeongoka. Lengo la wokovu ni kuhesabiwa haki. Na sababu ya wokovu ni kusaliwa upya. Mtokeo ni wongofu. (Mkengeuko wa Leo, uk. 17, 18).

Kufanya uamuzi ni kazi ya mwanadamu inayoweza kufanywa na yeyote, wakati wowote. Wongofu ni kitendo kisicho cha kawaida cha kiungu kinachobadilisha maisha ya mwanadamu na hatima yake.

Kupata uamuzi ni rahisi kuliko kuileta nafsi kwa wongofu. Mhubiri anaweza kupata idadi kubwa ya wanaofanya “uamuzi” anayoweza kuhesabu. Unaweza kupata wanaofanya uamuzi kila mahali, wakati wowote. Unaweza kuomba ombi la menye dhambi na watu katika milango yao, ndani ya ndege, ama mahali popote. Unaweza kuwahesabu, lakini pengine hautawaona tena. Walifanya uamuzi, lakini hawakuongoka.

Kahusu wongofu, watu wengi wanahitaji kuja kanisani na kusikia injili mara nyingi kabla ya kuielewa na kumwamini Kristo. Watu wengine huja kanisani miezi kadhaa na hata miaka kabla ya kupokea wongofu.

Kuwaongoza watu kwa Kristo ni lazima uongee nao mmoja mmoja, wewe mwenyewe, baada ya wao kuitikia mwaliko wako. Waelekeze mahali pengine ambapo utazungumza nao. Usiwaongoze moja kwa moja katika maombi haraka haraka. Kuomba ombi la mwenye dhambi si sawa na kumwamini Yesu. Kuinua mkono, kwende mbele unapoalikwa, ama unapobatizwa si sawa sawa na kumwamini Yesu. Kufanya mambo hayo yote siyo dhibitisho ya kwamba mtu amemwamini Yesu. Kumwamini Yesu ni jambo tofauti, ni la kipekee na maalum. Kumwamini Yesu ni kumwamini Yesu.

Kumwongoza mtu ili amwamini Kristo na kupokea wongofu kamili uchukua muda, juhudi, ufahamu, maombi, na neema ya Mungu. Dkt. Hymers na Dkt. Cagan wamekuwa wakiwashauri watu kwa wongofu kwa zaidi ya miaka thelathini. Yafuatayo ni baadhi ya mambo waliyojifunza.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

1. Kwanza, wachungaji lazima wawasikilize wenye dhambi.

Usidhanie – kama wanavyofanya wahubiri wainjilisti karibu wote – ya kwamba mwenye dhambi tayari anaelewa Injili. Ni lazima umsikilize na ujue anachoamini. Historia yake ya kidini ni gani? Ni nini anachoamini kumhusu Yesu? Je! Anadhani Kristo ni roho? Je! Anadhani tayari Kristo anaishi moyoni mwake? Je! Anafikiria Yesu amemkasirikia? Je! anadhani anaenda Mbinguni, au la? Jua anavyofikiria. Alafu mwonyeshe ukweli na umwongoze kwa Kristo.

Anaishi namna gani? Kuna jambo linaloweza kumrudisha nyuma asiweze kuishi maisha ya Ukristo – ponografia, uzinzi, au upinzani kutoka kwa jamii? Wenye dhambi hawapaswi kujifanya wakamilifu ili waokolewe – hawawezi. Lakini yeyote ambaye kwa hiari na kila mara anaendelea katika dhambi hamwamini Kristo. Badala yake, anajiamini.

Ikiwa hautawasikiliza wenye dhambi, hauwezi kuwasaidia. Jua ni kwanini mwenye dhambi amekuja kuongea na wewe. Anataka Yesu amfanyie nini? Ni kwa nini alikuja? Mtu mmoja alisema alitaka Yesu ampe kazi. Lakini hiyo si wokovu! Hata ikiwa Yesu atampa kazi, angekuwa tu amepotea. Lazima yule mtu atake dhambi zake zisamehewe kupitia damu ya Yesu.

2. Pili, wenye dhambi hukosea kumhusu Yesu Kristo.

Mwenye dhambi anafikiria nini kumhusu Yesu? Muulize, “Yesu yuko wapi sasa?” Biblia inasema ya kwamba Yesu yuko mbinguni “ na ambaye sasa amekaa upande wa kulia wa Mungu” Baba (Warumi 8:34). Lakini Wabaptisti wengi waliopotea wanafikiria ya kwamba Yesu yuko tayari mioyoni mwao, au Yeye ni roho inayoelea angani. Hauwezi kuja kwa Yesu kama haujui mahali alipo.

Muulize mwenye dhambi, Yesu ni nani?” Watu wengi udhani ni mwanadamu tu, au mmoja wa waalimu mashuhuri katika historia. Lakini huyo “Yesu” hawezi kumwokoa yeyote. Watu wengine ufikiria ya kwamba Yeye ni roho, au Yesu ndiye Roho Mtakatifu. Lakini Kristo si roho. Baada ya Yesu kufufuka kutoka kwa wafu, Biblia inasema,

“Wakashtuka na kushikwa na hofu wakidhani wameona mzimu. Lakini yeye akawaambia, “Kwa nini mnafadhaika? Mbona mnakuwa na mashaka mioyoni mwenu? Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapaseni mkanione, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo.” Baada ya kusema hayo, akawaonyesha mikono na miguu. Wakiwa bado katika hali ya kutosadiki kwa sababu ya furaha yao, na wakiwa wanastaajabu, akawauliza, “Mnacho chakula chochote hapa?” Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. Akakichukua, akala, wote wakimwona” (Luka 24:37-43).

Alipofufuka kutoka kwa wafu, Yesu alikula. Roho haiwezi kula. Roho haina nyama na mifupa kama alivyokuwa Kristo. Na roho – hata Roho Mtakatifu – hana damu ya kuosha dhambi!

Muulize mwenye dhambi, “Je! Yesu amekukasirikia?” Wakatoliki wengi na baadhi ya wengine wengi hufikiria hivyo. Wanamwamini “Kristo” aliyekasirika – Ambaye si Yesu wa Agano Jipya. Biblia inasema ya kwamba Yesu anawapenda wenye dhambi. Alimsamehe mwivi msalabani na mwanamke aliyepatikana katika uzinzi. Mwenye dhambi anaweza kumwamini mtu aliyemkasirikia namna gani? Rekebisha makosa haya na umwelekeze mwenye dhambi kwa Yesu halisi.

3. Tatu, wenye dhambi hukosea kuhusu wokovu.

Kuna aina tatu kuu za makosa kuhusu wokovu. Wenye dhambi wengi ufikiri wakifanya mojawapo ya haya mambo, wataokolewa – au wakiwa wamefanya mojawapo ya hayo, hiyo ni dhihirisha wameokolewa. Hapa kuna hayo mambo matatu kuu ambayo wenye dhambi uamini badala ya Kristo.

Kitendo cha kimwili: Ubatizo, kwenda mbele, kuinua mkono, kufanya maamuzi kwa Bwana, kuacha dhambi chache (hii siyo toba ya Biblia, ambayo ni kubadilisha mawazo), au kusema maombi ya mwenye dhambi. Hizi ni kazi za mwanadamu ambazo haziwezi kumwokoa yeyote. Biblia inasema, “alituokoa. alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali alituokoa kwa sababu ya huruma yake” (Tito 3:5).

Kitendo cha akili: Kuwa na mawazo sahihi, au kuamini ukweli katika Biblia kuhusu Yesu au kuhusu wokovu. Wenye dhambi mara nyingi husema, “Namini ya kwamba Yesu alikufa msalabani kwa ajili yangu.” Lakini mamilioni ya watu wanaamini hili jambo. Hata Shetani anaamini kwamba Yesu ni mwana wa Mungu aliyekufa msalabani na akafufuka tena. Aliiona. Biblia inasema, “ Sawa! Lakini hata pepo huamini hilo, na hutetemeka kwa hofu” (Yakobo 2:19). Mwenye dhambi lazima amwamini Yesu Kristo Mwenyewe, si tu ukweli kumhusu.

Kitendo cha hisia: Hisia na vile ulivyosikia, kutafuta “hakikisho” badala ya Kristo, kujisikia vizuri katika maisha. Hisia huenda juu na chini. Kila mtu ana mawazo sahihi na hisia. kila mtu ana mawazo maovu na hisia. Mwenye dhambi anajua hivyo. Alikuwa na hisia hizo mwenyewe. Ukiamini hisia zako, utadhani umeokolewa alafu ukapotea, umepotea alafu ukaokolewa, maisha yako yote. Wokovu unapatika kwa Kristo pekee, si kwa hisia. Wimbo mzuri wa zamani unasema,

Tumaini langu halijajengwa kwingine
   Ila kwa Damu ya Yesu na haki yake.
Sita thubutu hata ubunivu mzuri [ubunivu wa akili, hisia]
   Lakini nitategemea kabisa Jina la Yesu.
Kwa Kristo, Mwamba imara, Nasimama,
   Kwingine ni mchanga unaozama;
Kwingine ni mchanga unaozama.
   (“Mwamba Imara” na Edward Mote, 1797-1874).

Rekebisha makosa haya na umwelekeze mwenye dhambi moja kwa moja kwa Yesu Mwenyewe, ili asamehewe dhambi kwa Damu Yake.

Dhana nyingi za uongo humtaja Kristo, lakini “wanamweka chini ya” au “wanampitishia kwa” jambo lingine. Watu wengine wanafikiria ya kwamba unapobatizwa, unapokea wokovu katika Kristo. Hii umweka Kristo “chini” na “kupitia” ubatizo wa maji. Wengi ufikiria ya kwamba ukisema ombi la mwenye dhambi utaokolewa, na kwamba hilo ombi ni sawa na kumwamini Yesu. Hivyo wanawashawishi watu kuomba hilo ombi na wanakisia wameokoka, wakati ambapo ni wachache wao umwamini Yesu na kuongoka. Hivyo ni kumweka Kristo “chini ya” na “kupitia” maneno katika maombi. Biblia inasema “Yesu Kristo Mwenyewe” ndiye jiwe la pembeni (Waefeso 2:20), siyo maneno katika ombi la mwenye dhambi. Mwelekeze mwenye dhambi kumwamini Yesu Kristo Mwenyewe.

Nimewaona watu wakitoka kutoka kwa kosa moja hadi lingine. Wanaanza kwa kutafuta kama kuna hisia. Wakati ule mwingine wanasema, “Sikuwa na hisia zozote. Ninaamini tu ya kwamba Kristo alinifia.” Mwenye dhambi ametoka kutoka kwa kosa la kuwa na hisia hadi kwa kosa la kuhufahamu ukweli kuhusu Yesu. Mwondoe mwenye dhambi kutoka hapo amejificha na umwelekeze kwa Yesu.

4. Nne, wenye dhambi wanahitaji kuhukumika kwa dhambi za mioyo yao.

Mwenye dhambi lazima ahukumike kuhusu dhambi ya moyo wake. Kila mmoja ukubali kwamba ni mwenye dhambi kwa jia fulani. Kila mmoja anakubali ya kwamba si wakamilifu, ya kwamba wamefanya mambo mengine kwa makosa. Siongei kuhusu hayo.

Siongei kuhusu ufahamu wa dhambi halisi au dhambi fulani. Ndiyo, mwenye dhambi amefanya dhambi nyingi. Lakini kufikiria tu kuhusu hiyo dhambi hakutamuokoa. Ukipitia orodha ya dhambi fulani, mwenye dhambi anaweza fikiria, “Sifanyi hayo mambo, hivyo lazima niwe nimeokoka.” Au anaweza fikiria, “Nitaacha kufanya hayo mambo na hiyo itaonyesha ya kwamba nimeokoka.”

Dhambi inaenda ndani kuliko hivyo. Kila mmoja ni mwenye dhambi ndani yake, wana asilia ya dhambi waliyoirithi kutoka kwa Adamu. Kila mmoja ana moyo mwovu. Biblia inasema, “Moyo wa mtu ni mdanganyifu kuliko vitu vyote; hauwezi kuponywa” (Yeremia 17:9). Kila mwenye dhambi ana ubinafsi ndani yake. Kila mwenye dhambi yuko kinyume na Mungu moyoni mwake. Hii ni ya kina zaidi kuliko dhambi fulani ambayo mtu amefanya. Kile wanachokifanya hutokana na kile walicho. Ni ya kina zaidi kuliko chochote mwenye dhambi anachofanya, moyo wake, hali yake yote, ina dhambi na makosa. Mwenye dhambi ni lazima ahisi dhambi za moyo wake. Mwambie kuhusu dhambi za moyo wake unapohubiri, na unapozungumza na yeye baada ya mahubiri.

Mwenye dhambi haweze kuubadilisha moyo wake mwenyewe, kama vile mbuzi hawezi kujibadilisha kuwa kondoo. Hiyo ndiyo maana ya kwamba amepotea na hawezi kujiokoa. Hawezi kumwamini Kristo kwa uwezo wake. Ni Mungu tu anayeweza kumvuta kwa Yesu. Kristo alisema, “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama asipovutwa na Baba aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho” (Yohana 6:44). Hii inaitwa “visa ya Injili” – mwenye dhambi lazima aje kwa Kristo, lakini hawezi kufanya hivyo. Hawezi kufanya lolote kujiokoa. Kama inavyosema Biblia, “Mwenyezi-Mungu, ndiye aokoaye” (Yona 2:9). Mwenye dhambi lazima awe kama Isaya aliyesema, “ Ole wangu! Kwa maana nimepotea.” (Isaya 6:5). Mwonyeshe dhambi ya moyo wake. Mwonyeshe kwamba hawezi kujiokoa. Mwonyeshe ya kwamba anahitaji reheme. Kwa hiyo anaweza kuja kwa Kristo.

5. Tano, ikiwa mwenye dhambi amehukumika kuhusu dhambi ya moyo wake, jaribu kumwongoza kwa Kristo.

Si mwongozi kila mtu anayekuja kuongea nami kwa Kristo! Watu wengine ni tamaa waliyo nayo. Hawataki kusamehewa dhambi zao. Watu wengine wanakuja kwa sababu waliwaona watu wengine wamekuja. Watu wengine hawana hisia za dhambi zao na hawana uamsho wa Mungu. Kuwaongoza watu wanaojidanganya katika maombi kumwamini Kristo huwaleta katika uongofu wa uongo. Ni wakati gani uliobora kwa mtu kumwamini Kristo?

Mwenye dhambi lazima “ajichukie,” kama alivyosema msichana mmoja kanisani kwetu. Ni lazima “ajikane.” Ni lazima “afike mwisho wake.” Isaya alifika mwisho wake aliposema, “Ole wangu! Kwa maana nimepotea” (Isaya 6:5). Basi ni rahisi zaidi kumwani Kristo. Yeye hatafuti kujifunza kitu. Anahitaji Kristo amuokoe.

Mwenye dhambi lazima amwamini Kristo Mwenyewe. Mwelekeze mwenye dhambi kwa Yesu Kristo Mwenyewe na msamaha wa dhambi zake kupitia Damu Yake. Unaweza kumwongoza mtu kwa maombi rahisi tu kama “Yesu, Nina kuamini. Zioshe dhambi zangu na Damu yako.” Ama kunaweza kuwa hakuna ombi lolote, ni kumgeukia Kristo kwa msamaha wa dhambi kupitia Damu Yake. Mwenye dhambi hahitaji kuomba ombi. Mwenye dhambi hahitaji kuwa na picha ya Yesu katika mawazo yake. Maneno si lazima yawe “sahihi.” Watu wengine ukariri– na wanayarudia– maneno “sahahi” lakini hawamwamini Kristo. Yule mwivi msalabani hakuyasema maneno makamilifu. Alisema, “Bwana, Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako” (Luka 23:42). Lakini alijua alikuwa mwenye dhambi asiye na tumaini na alimgeukia Kristo. Ilikuwa rahisi hivyo tu! Bwana alimjibu, “Nakuambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi” (Luka 23:43). Kumwamini Yesu Kristo mwenyewe kuna umuhimu kuliko kuyasema maneno!

6. Sita, baada ya kumzungumzia mwenye dhambi, muulize maswali machache rahisi.

Muulize, “Umemwamini Yesu?” Ikiwa atasema “hapana” mzungumzie tena. Ikiwa atasema “ndiyo” muulize ni lini alimwamini Yesu. Ikiwa atasema, “Nimemwamini maisha yangu yote” ama “Nilimwamini kitambo,” hajapokea wongovu.

Ikiwa atasema, “Nimemwamini Kristo sasa hivi,” muulize amefanya nini. Jaribu kumsaidia kuelezea kitendo chake cha kumwamini Kristo kwa maneno yake mwenyewe. Watu wanaweza kuyakariri “maneno ya kanisa” na kuyarudia hata ingawa hawajaongoka Mwenye dhambi alifanya nini kumwamini Kristo? Aliamini jambo lolote kuhusu Kristo? Aliamini hisia fulani? ama alimwamini Yesu Kristo Mwenyewe moja kwa moja?

Muulize, “Yesu Kristo amekufanyia nini?” Ikiwa yule mtu hatazungumzia kuhusu Kristo kumsamehe dhambi zake kupitia Damu Yake, lakini anazungumzia kuhusu mawazo yake ama vile anavyohisi, hajaongoka!

Muulize, “Ikiwa ungekufa leo, unaweza kwenda mbunguni au Jahanamu?” Ikiwa atasema “Mbinguni” muulize kwa nini. Yeye angemwambia Mungu nini ikiwa Mungu atamuuliza ni kwa nini anataka kuingia mbinguni? Ikiwa yule mtu ataanza kuzungumzia matendo mema ama jambo lingine kando na Kristo na Damu, hajaokoka! Alafu muulize, “Mwaka mmoja kutoka sasa, ikiwa utakuwa na wazo mbaya na halafu ufe, utaenda wapi?” Ikiwa atasema “Jahanamu,” anategemea uzuri wake na amtegemei Kristo. Basi unaweza kumuuliza, “Mwaka mmoja kutoka sasa, ukitoka kanisani na ukose kurudi tena, na uishi na mwanamke (au mwanamume) bila kufunga ndoa, na kujamiiana, na unatumia madawa ya kulevya kila siku, utakuwa Mkristo au la?” Ikiwa atasema “ndiyo” hajashughulikia tatizo la dhambi, na bado amepotea.

Ni muhumu kumuuliza asiseme tu, “Nilimwamini Yesu,” lakini aeleze alichofanya na Yesu wakati ule alipokuwa akimwamini. Unataka kusikia wakati wake wa kuamini, si habari ya maisha yake ama mambo yote yaliyotendeka siku hiyo. Si tafuti mawazo fulani ama hisia. Lakini ni hali ya dhambi zake na msamaha wa dhambi kupitia Damu ya Kristo na kupitia kitendo cha kumwamini Yesu Krsito Mwenyewe lazima kiwepo. Maelezo kuhusu hali waliopitia wakipokea wongofu ni tofauti kutoka kwa watu tofauti. Ninachotafuta ni uhalisia, uhakika katika mambo anayoyasema.

Ikiwa yule mtu amefanya makosa, rekebisha yale makosa na uzungumze naye tena. Lakini mtu anayerudia kosa moja mara kwa mara ni dhihirisho kwamba hayuko tayari kwa wongovu. Wale ambao Mungu anawaongoza kwa uokovu watayasikiliza mahubiri na mawaidha yako. Wale ambao hawasikilizi hawataongoka.

Usivujike moyo ikiwa mtu hataongoka baada ya kuzungumza na yeye. Watu wachache wanaongoka mara ya kwanza wanaposikia Injili, lakini wengi hawaongoki. Baathi ya watu huja mara kwa mara kabla ya kumwamini Kristo.

Mshughulikie mtu mmoja zaidi ya mara moja. Usiwabatize watu moja kwa moja. Waulize wangoje kwa mwaka mmoja hivi, na pengine miaka miwili ingekuwa bora kutokana na hali ya ukengefu katika makanisa siku hizi. Pengine miaka miwili ama mitatu ingekuwa bora. Hiyo itakupa muda wa kuona kama kwamba imani yao ni halali. Unaweza kumuangalia mtu kwa njia nyingi katika hicho kipindi. Unaweza kumuuliza ashuhudie – nje ya ibaada. Unaweza kumuuliza tena baada ya majuma kadhaa ama miezi kadhaa. Wale ambao hawakumwamini Kristo watasahau ule “ushuhuda” waliutengeneza ule ushuhuda na watakosea wanapoulizwa tena baada ya mwaka mmoja ama miwili. Walitaka tu “kufaulu” na kuidhinishwa, lakini hawakumwamini Yesu. Wengine wanaweza kukariri maneno fulani na kuyarudia, lakini unapowauliza kwa njia tofauti wakati tofauti hawajui la kusema, kwa sababu hawakumjua Yesu kibinafsi.

Angalia tabia zake na mwenendo wake. Mtu ambaye ataliacha kanisa lako na kukataa kukusikiliza huonyesha ya kwamba hakuhukumika kuhusu dhambi zake na hakumwamini Kristo. Mtu aliye na mtazamo mbaya wa kila mara kuhusu kanisa na maisha ya Ukristo uonyesha ya kwamba hakuhukumika kwa dhambi zake na hakumwamini Kristo.

7. Saba, kumbuka jaribio la kweli la huduma ya ushauri.

Jaribio la kweli la huduma ya ushauri ni hili: UNAWEZA KUMWAMBIA MTU YA KWAMBA HAKUMWAMINI KRISTO NA HAKUONGOKA SIKU HIYO? UNAWEZA KUMWAMBIA MTU YA KWAMBA NI LAZIMA AJE MARA NYINGINE NA KUZUNGUMZA NA WEWE KUHUSU WOKOVU? Simfahamu Mchungaji yeyote anayefanya hivi. Hii ndiyo sababu makanisa yetu yamejaa watu waliopotea, pamoja na walimu wa watoto kanisani, mashemasi, wake wa Wachungaji, na Wachungaji wenyewe. Wachungaji wanasisitiza kuomba ombi na kila mmoja anayeitikia mwaliko wao. Wanafanya hivyo ili wawe na hesabu ya watu waliowabatiza. Pengine karibu wote waliobatizwa hawakuokoka. Hawawezi kuendelea kuwa waaminifu kanisani kwa sababu hawajaokoka. Hawa si watu ambao “wamerudi nyuma.” Wamepotea kwa sababu mhubiri hakushughulika kuona kwamba wameongoka. Ikiwa unaweza kumwambia mtu bado amepotea na anahitaji kurudi tena ndilo jaribio la kweli kwa huduma yako. Wewe ni kama wale watu “Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu”? (Yohana 12:43). Au unaongea ukweli ikiwa watu wanautaka ama hawautaki?

Hii ni njia ya kusema: Unaamini wongovu halisi – imani ya kweli katika Kristo inayoleta maishi halisi ya Ukristo? Ukisisitiza kuendelea kuongoza kila mmoja katiaka maombi, ama wainue mikono yao, ama kujaza kadi fulani, Wewe ni “Muamuzi.” Haushughulikii nafsi za watu ambao Mungu amewatuma kwako.

Natumaini wengine wenu wanaamini wongovu kamili. Natumaini kwamba wengine wenu wanaona umuhimu wa kuchukua muda na kila mmoja, kuhakikisha ya kwamba amemwamini Kristo na ameongoka. Hivi ndivyo anavyo fanya Mchungaji mwaminifu. Mchungaji mwaminifu ushughulikia kondoo. Natumaini ya kwamba utafanya lililobora kuhakikisha ya kwamba watu wako wamemwamini Kristo na wameongoka.

UNAWEZA FIKIRIA KWAMBA NIMEINGIA KATIKA MAELEZO YA NDANI SANA KUHUSU HILI, KWAMBA WONGOVU NI JAMBO TU RAHISI AMBALO HALIHITAJI FIKIRA NYINGI. Lakini ingekuwaji kama taaluma ya matabibu haikuhitaji mkunga? Ingekuwaji kama wote wangekuwa wanafanya kitu kimoja, au hawakuosha mikono yao, au hawakujua jinsi ya kusalisha mtoto aliyetangulia kwa makalio, n.k.? Kama tungeshughulikia ukunga wa watoto kama vile tunavyoshughulikia nafsi, mamilioni ya watoto wangekufa pasipo sababu – kwa sababu sasa hivi mamilioni ya nafsi zinakufa bila sababu na kwenda Jahanamu kwa sababu hatuchukui muda wa kutosha kuhakikisha ya kwamba wameongoka, au kuwafundisha watu jinsi ya kufanya hivi katika shule za Biblia na seminari – AMBAPO HAYA HAYAFUNDISHWI KABISA!!!

Naenda kuyasoma maneno ya “Alafu Yesu Akaja,” na Oswald J. Smith na wimbo wa Homer Rodeheaver. Yesu anapokuja maishani mwako, Damu Yake inakuosha dhambi zote; Damu aliyomwaga msalabani hata sasa inapatikana kuziosha dhambi zako. Na Yesu alifufuka kutoka kwa wafu kukupa uzima wa milele. Mwamini tu Yesu na atakusamehe dhambi zako na kukupa uzima wa milele. Natumaini utarudi na kula chakula cha jioni pamoja nasi saa kumi na mbili na robo usiku huu. Dkt. Hymers atahubiri ujumbe wa kiinjilisti unaoitwa, “Kipovu aliyeponywa na Yesu.” Hakikisha umerudi saa kumi na mbili na robo usiku huu na ubakie baada ya mahubir ya Dkt. Hymers ili ushiriki chakula cha jioni.

Mmoja aliyeketi kado ya njia akiomba,
Macho yake yalipofuka, angeweza kuuona mwangaza.
Aliyashikilia matambara yake na kutetemeka gizani
Alafu Yesu akaja akafukuza giza chake.
Yesu anapokuja, nguvu za Shetani zinashindwa;
Yesu anapokuja, machozi yanafutwa,
Anaondoa giza na kujaza maisha na utukufu,
Maana yote yabadilika Yesu anapokuja kukaa.
.
Mbali na nyumbani na marafiki mapepo wachafu wakamfukuza,
Katika makaburi aliishi kwa taabu;
Alijikatakata alivyopagawa na nguvu za mapepo,
AlafuYesu akaja na kuweka mateka huru.
Yesu anapokuja, nguvu za Shetani zinashindwa;
Yesu anapokuja, machozi yanafutwa,
Anaondoa giza na kujaza maisha na utukufu,
Maana yote yabadilika Yesu anapokuja kukaa.

Hivyo watu leo wamemjua Mwokozi anaweza,
Hawangeweza kushinda tamaa, uchu na dhambi;
Mioyo yao iliyovujika iliwaacha na huzuni na upweke,
Alafu Yesu akaja na kuishi, Mwenyewe, ndani.
Yesus anapokuja, nguvu za Shetani zinashindwa;
Yesu anapokuja, machozi yanafutwa,
Anaondoa giza na kujaza maisha na utukufu,
Maana yote yabadilika Yesu anapokuja kukaa.
   (“Alafu Yesu Akaja” na Dkt. Oswald J. Smith, 1889-1986;
      wimbo wa Homer Rodeheaver, 1880-1955).


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Benjamini Kincaid Griffith:
“Alafu Yesu Akaja” (na Dkt. Oswald J. Smith, 1889-1986;
wimbo wa Homer Rodeheaver, 1880-1955).


MWONGOZO WA

JINSI YA KUIONGOZA NAFSI KWA KRISTO –
USHAHURI KWA WONGOVU!

HOW TO LEAD A SOUL TO CHRIST –
COUNSELING FOR CONVERSIONS!

Mahubiri yaliyoandikwa na Dkt. C. L. Cagan
na kuhubiriwa na Kasisi Yohana Samweli Cagan

“Msipoongoka-----hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”
(Mathayo 18:3).

(Yohana 3:3, 7; IIWakorintho 5:17)

1.  Kwanza, wachungaji lazima wawasikilize wenye dhambi.

2.  Pili, wenye dhambi hukosea kumhusu Yesu Kristo, Warumi 8:34;
Luka 24:37-43.

3.  Tatu, wenye dhambi hukosea kuhusu wokovu, Tito 3:5; Yakobo 2:19;
Waefeso 2:20.

4.  Nne, wenye dhambi wanahitaji kuhukumika kwa dhambi za mioyo yao,
Yeremia 17:9; Yohana 6:44; Yona 2:9; Isaya 6:5.

5.  Tano, ikiwa mwenye dhambi amehukumika kuhusu dhambi za moyo
wake, jaribu kumwongoza kwa Kristo, Isaya 6:5; Luka 23:42, 43.

6.  Sita, baada ya kumzungumzia mwenye dhambi, muulize maswali
machache rahisi.

7.  Saba, kumbuka jaribio la kweli la huduma ya ushauri, Yohana 12:43.