Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




WANAFUNZI NA MAPEPO

DISCIPLES AND DEMONS
(Swahili)

Mahubiri yaliyoandikwa na Dkt. R. L. Hymers, Jr.
na kuhubiriwa na Kasisi Yohana Samweli Cagan
katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Asubuhi ya, Julai 22, 2018
A sermon written by Dr. R. L. Hymers, Jr.
and preached by Rev. John Samuel Cagan
at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Morning, July 22, 2018


Hili ndilo somo la tatu tunalolitoa juu ya Kristo alipowafundisha wanafunzi Wake. Tunapofuatilia Yesu anapowafundisha, tunajifundisha jinsi ya kuwafundisha wanafunzi siku hizi.

Yesu hakuwafundisha wanafunzi wake jinsi makanisa yetu yanavyojaribu kuwafundisha vijana siku hizi. Tunastahili kuwa makini kwa njia ambayo Yesu alitumia kuwafanya wanafunzi, kwa sababu alifaulu sana, na makanisa yetu kwa kawaida hushindwa. Mojawapo ya makosa tunayoyafanya siku hizi ni kujaribu kuwafanya wanafunzi wetu waongoke kabla hatujawafundisha kuwa wanafunzi. Lakini Yesu alitumia miaka mitatu kuwafundisha wanafunzi Wake, kabla hawajazaliwa mara ya pili (Yohana 20:22; tazama J. Vernon McGee na Thomas Hale). Hiyo ndiyo tofauti kuu kati ya jinsi Yesu alivyofanya, na vile tunavyojaribu kufanya siku hizi.

Tofauti nyingine kuu ni masomo Kristo aliyowafundisha. Mwanzo kabisa Yesu aliwaita na akasema, “nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu” (Marko 1:17). Aliwafundisha akiwa na lengo moja kuu – kuwawezesha kuwasaidia wengine kuwa wanafunzi. Yesu aliwaambia hilo ndilo lilikuwa lengo lake kutoka pale mwanzo. Na hili ndilo lengo langu vilevile. Siko hapa kuwafundisha hadithi za biblia, kama wanavyofanya katika kanisa la watoto siku hizi. Lengo langu nikuwafundisha kuwa wavuvi wa watu, kuwaleta wengine wamfuate Kristo na kuwafikia waliopotea. Kristo aliwaambia hivyo hapo mwanzo kabisa (tazama Marko 1:16-20).

Jambo la pili Kristo alilowafundisha ni jinsi ya kupambana na Shetani na mapepo wake. Angalia Marko 1:21-27.

“Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha.Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi. Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke. Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii!” (Marko 1:21-27).

Tazama. Jambo la pili Kristo alilowafunza wanafunzi Wake wa kwanza ni kuhusu nguvu Zake dhidi ya Shetani na mapepo wake. Biblia ya kujifundisha ya matengenezo (ukurasa 290) inasema,

Mapepo ni malaika walioanguka...wanaomtumikia Shetani. Walipoungana na uasi wa Shetani, walitupwa kutoka mbinguni...Jeshi la Shetani la mapepo [utumia] undanganyifu na kuvunja moyo kwa njia nyingi. Kuwapinga ndiyo kazi ya vita vya kiroho (Waefeso 6:10-18).

Kama mwanafunzi mpya, Yesu anataka ujue kuhusu Shetani na mapepo wake. Mmoja wa watu ambao Yesu aliwatia moyo alikuwa amepagawa na mapepo. Katika tafsiri ya Biblia ya Mfalme Yakobo neno la Kuyunani linalomaanisha mapepo lametafsiriwa “pepo.” Tazama Marko 1:39,

“Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo” (Marko 1:39).

Unapokuwa mwanafunzi wa Yesu, lazima ufahamu mapepo walio katika mazingira yaliyokuzunguka. Mapepo wanawapofusha watu wasiuone ukweli ulio katika Biblia. Mapepo watajaribu kukutisha na kukufanya uache kuja kanisani kwetu. Mapepo watajaribu kukufanya usiwe Mkristo. Dkt. Thomas Hale alisema,

Ni lazima tukumbuke ya kwamba kupagawa na pepo si aina ya ugonjwa wa akili. Mapepo au roho chafu, ni watumishi wa pepo mkuu, Shetani. Ni watenda kazi wa uovu. Wanapopagawa mtu, wanamfanya kuwa mfungwa au mtumwa wa Shetani. Ni kupitia tu nguvu za Yesu ambapo mapepo hawa wanaweza kushindwa na yule mtu awe huru (Thomas Hale, M.D., Ufafanuzi unaofaa kwa Agano Jipya; maelezo juu ya Marko 1:21-28).

Watu upagawa na mapepo kupitia utumizi wa madawa ya kulevya, uchawi, na aina nyinginezo za uasi kinyume na Mungu.

“Vyema,” mtu atasema, “Sijatumia madawa ya kulevya, sijashiriki katika uchawi, Sijafanya mambo haya.” Nina furaha ya kwamba haujaingia kwa dhambi kiasi hiki. Lakini hata hivyo, mawazo yako yamefanyiwa kazi (yamewezeshwa) na “mfalme wa uwezo wa anga” (Shetani; Waefeso 2:2). Kwa hiyo mawazo yako yasiyoongoka yanawezeshwa na Shetani, “mfalme wa uwezo wa anga.”

Jambo la pili Shetani analolifanya ni kukupofusha kwa ukweli. Sikiliza II Wakorintho 4:3-4.

“Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu” (II Wakorintho 4:3-4).

“mungu wa dunia hii” linatafsiriwa vizuri “mungu wa wakati huu.” Shetani ndiye mungu wa wakati huu. Shetani amepofusha mawazo ya “hao wanaopotea.” Unaweza shangaa ni kwa nini hauelewi Injili ya Kristo. Jibu ni rahisi – mungu wa wakati huu [Shetani] amepofusha mawazo yako. Lakini Kristo ana nguvu zaidi kumshinda Shetani, au yeyote kati ya mapepo wake. Hiyo ndiyo sababu Kristo kwa urahisi alimtoa yule pepo kule Kapernaumu. Kristo alisema, “umtoke” na yule pepo “akamtoka” (Marko 1:25, 26).

Ikiwa unataka kuwa Mkristo halisi na mwanafunzi wa Yesu, basi Kristo lazima aondoe utawala wa Shetani katika mawazo yako. Mtu mmoja asiye amini kuna Mungu alimwambia Dkt. Hymers, “Ninahitaji kubandilishwa ubongo wangu.” Hiyo ilikuwa imezidi sana. Alichohitaji huyo kijana ni kuoshwa mawazo yake na Yesu. Jinsi Yesu anavyofanya hivyo ni rahisi. Anayaosha mawazo yako na neno la Mungu – Biblia. Biblia inazungumzia kuhusu “ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno” (Waefeso 5:26). Zaburi 119:130 inasema,

“Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga” (Zaburi 119:130).

Je! Unataka kuwa mwanafunzi wa Yesu? Hapa kuna njia inayofaa ya kuanza. Soma nakala moja ya mahubiri ya Dkt. Hymers kutoka kwa tovuti yetu kila usiku kabla haujalala. Tovuti yetu ni www.sermonsfortheworld.com. Ikiwa utasoma nakala moja ya mahubiri ya Dkt. Hymers kila usiku kabla haujalala, vifungu vya Biblia pamoja na maelezo vitatakaza mawazo yako na muda usiyo mrefu utamwamini Yesu na utaokolewa! Tafadhali simama na uimbe wimbo nambari 5, “Najua Biblia ni ukweli.”

Najua Biblia ilitumwa kutoka kwa Mungu, Agano la kale, pamoja na Agano Jipya;
   Ina pumzi ya Mungu na ni takatifu, Neno linaloishi, Najua Biblia ni ukweli.
Najua, Najua, Najua Biblia ni ukweli;
   Ili puliziwa na Mungu moja kwa moja, Najua Biblia ni ukweli.

Najua Biblia yote ni ukweli, Kwa maana inanipa amani ndani mwangu;
   Inanipata, inanifariji siku kwa siku, Na inanipa ushindi dhidi ya dhambi.
Najua, Najua, Najua Biblia ni ukweli;
   Ili puliziwa na Mungu moja kwa moja, Najua Biblia ni ukweli.

Ingawa maadui wanaikataa kwa roha ya ujasiri Ujumbe wa kale, na bado ni ujumbe mpya,
   Ukweli wake ni mtamu kila mara unaposemwa, Najua Biblia ni ukweli.
Najua, Najua, Najua Biblia ni ukweli;
   Ili puliziwa na Mungu moja kwa moja, Najua Biblia ni ukweli.
(“Najua Biblia ni Ukweli” na Dkt. B. B. McKinney, 1886-1952).


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Benjamini Kincaid Griffith:
“Najua Biblia ni Ukweli” (na Dkt. B. B. McKinney, 1886-1952).