Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.
JESHI LA GIDEONI!

GIDEON’S ARMY!
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana jioni ya, Juni 24, 2018
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Evening, June 24, 2018

“Bwana akamwambia Gideoni, Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno hata nikawatie Wamidiani katika mikono yao, wasije Israeli wakajivuna juu yangu wakisema, Mkono wangu mwenyewe ndio ulioniokoa” (Waamuzi 7:2).


Ni hadithi rahisi. Lakini ni hadithi muhimu sana. Gideoni alikuwa kijana mchanga aliyeishi nyakati za mkengeuko mkubwa. Hivyo hili linastahili usikivu wetu sasa hivi kwa sababu tunaishi katika mkengeuko mkuu wa nyakati za mwisho.

I. Kwanza, mkengeuko.

Watu wa Israeli walitenda maovu mbele za Mungu. Na Mungu akawaadhibu kwa kuwaachilia kuwa watumwa wa Wamidiani. Walikuwa maadui wa Israeli. Watu wa Israeli waliwakimbia hawa wakatili wa Midiani. Walijificha kwa mapango wasionekane na hawa Wamidiani wasio mjua Mungu. Wamidiani walikuwa na nguvu kiasi cha kwamba waliharibu mimea ya Waisraeli. Waliiba kondoo wao na ngombe wao na punda wao. Waisraeli walitwezwa na hawakuwa na tumaini. Halafu walimlilia Bwana.

Halafu Mungu akamwambia Gideoni. Mungu alimjia alipokuwa amejificha Wamidiani wasimuone. Na Mungu akamwambia Gideoni, “Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa” (Waamuzi 6:12).

Si kuwa shujaa, nilipoenda katika seminari inayokataa Bibilia kasikasini mwa San Francisco. Nilikuwa mhubiri kijana wa kibaptisti aliyekuwa mtiifu na mpole. Lakini yale niliyoyaona katika ile seminari yalinifanya nikasirike sana na uinjilisti wa kisasa. Hawakumwamini Mungu wa Bibilia. Waliongozwa na Wamidiani – waliotaka kumwongoza Mungu – wale ambao hawakutaka Mungu ayatawale mawazo yao na maisha yao.

Dkt. David F. Wells ameandika kitabu muhimu kuhusu upotovu wa uinjilisti wa wakati wetu. Kinaitwa, Hakuna nafasi ya ukweli: ama kilichotendeka katika theolojia ya uinjilisti? (Eerdmans, 1993). Dkt. Wells ni mtu aliye na hasira. Anasema, “Ulimwengu wa uinjilisti umepoteza hali yake ya uasilia” (uk. 295). Makanisa ya uinjilisti hayawashawishi vijana kuwa na ukiristo asilia. Ni wapole, wadhaifu, na wenye ubinafsi – wanaogopa kusema wakiogopa ni kipi watu watakachofikiria juu yao. Uongozi wa kiinjilisti utampinga yeyote anayetaka kuona makanisa yamebadilika na kuwa hai leo. Dkt. Wells alisema, “Ile hali ya kusawazisha ni msukumo wenye nguvu katika ulimwengu wa kiinjilisti na haraka ukomesha wasiokubaliana na mafundisho yao” (uk. 295).

Walijaribu bila kufanikiwa kunishurutisha kusingatia hali yao ya kutoamini katika hiyo seminari niliyojiunga nayo. Waliniambia sitawahi kupata kanisa la Kibaptisti la kusini ikiwa nitaendelea kuitetea Bibilia. Niliwaambia, “Ikiwa hiyo ndiyo gharama yake, sitaki kulipata.”

Nilipoteza kila kitu kwa kuchukua huo msimamo. Nilikuwa na nini cha kupoteza? Nilikuwa tayari nimepoteza chochote kilichokuwa muhimu kwangu. Kanisa la Baptisti la Kusini halikuwa na chochote ningehitaji. Nilichukia dhehebu hilo. Nilichukia hiyo seminari. Nilichukia kanisa langu kwa kutonisaidia. Nilichukia maisha yangu. Nilichukia kila kitu isipokuwa Yesu na Bibilia. Nilitembea peke yangu gizani. Ilibidi niendelee kutembea la sivyo nilihisi kana kwamba ningepoteza fikira zangu.

Hatimaye usiku mmoja polepole bila kujua niliingia chumbani mwangu kulala. Mungu mwenyewe aliniamsha. Kulikuwa na utulivu mule ndani ya bweni. Hakukuwa na sauti yeyote. Nilitoka nje ule usiku. Nilipokuwa nimesimama mbele ya kilima kado ya seminari ningeweza kuona mwangaza wa mataa ya San Francisco upande ule mwingine wa ghuba. Upepo ulivuma kupitia nywele zangu na uso wangu. Nilihisi baridi hata kwa mifupa. Na katika ule upepo Mungu akazungumza na mimi,“Hautawahi sahau usiku huu. Sasa utahubiri tu kunipendeza. Sasa utajifundisha kutoogopa. Sasa utazungumza kwa niaba yangu pekee. Nitakuwa pamoja na wewe.”

Sasa najua huo ulikuwa mwito wangu wa kuhubiri. Kabla ya hiyo nilikuwa tu mtu wa kujitolea. Na sasa nikawa mhubiri aliyeitwa na Mungu. Ninaamini ya kwamba kila mhubiri asiyeogopa ni lazima apitie changamoto kama hizi kabla Mungu kumwamini kuhusema ukweli. Hakukuwa na msisimko. Ni hili tu,“Ikiwa hautayasema hakuna atakayeyasema, na yanahitajika sana kusemwa – na wengine wanaogopa kuyasema, sasa ikiwa hautayasema hakuna atakayeyasema, ama hawatayasema vizuri.” Nilienda na hayo mawazo yakiwa yamezama katika mawazo yangu milele. Dkt. W. A. Tozer, katika insha yake inayoitwa “Kipawa cha ufahamu wa kinabii,” alisema hili: “Atabishana, atashutumu na kupinga kwa jina la Mungu na atachukiwa na kupingwa na sehemu kubwa ya jamii ya Wakristo... Lakini hataogopa chochote ambacho kinachopumua na pumzi ya binadamu.” Pengine hiyo ndiyo sababu Dkt. Bob Jones III alisema yeye ni “kama nabii wa Agano la Kale kwa namna na kwa roho.” Kwa maelezo zaidi kuhusu haya, soma kitabu cha habari za maisha yangu, “Dhidi ya woga wote.”

Hiyo hali niliyopitia usiku huo ilinifanya nimuelewe mtu kama Gideoni. Mungu alimwambia, “Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa.” Ata ingawa mimi sio Gideoni, kwa sasa namuelewa. Gideoni alisema, “Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani” (Waamuzi 6:13).

Gideoni alihisi hastahili na hana uwezo wa kufanya hayo. Kama vile Musa, Gideoni pia alitoa udhuru. Tuko hapa sasa, rafiki zangu, katikati ya ukengeufu mkuu wa nyakati za mwisho. Tunajihisi hatustahili na hatuwezi kupigana na dini ya uwongo ya uinjilisti-mpya wa Kimidiani. Uasi umekuwa wa kina sana. Nguvu za uinjilisti wa Kimidiani ni kuu sana. Hatuwezi fanya lolote kuiokoa Bibilia na Mungu wa Biblia kutokana na hawa waasi.

II. Pili, Mungu wa Bibilia bado Yu hai!

Mungu alisema, “Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeut”! (Malaki 3:6). Alafu Roho wa Mungu akaja juu ya Gedioni. Aliwatuma wajumbe waliokusanya umati wa Waisraeli kupigana na Wamidiani.

“Kisha Yerubaali, yaani Gideoni, na watu wote waliokuwa pamoja naye wakaondoka na mapema, wakapiga kambi yao karibu na kijito cha Harodi; na kambi ya Midiani ilikuwa upande wao wa kaskazini, karibu na mlima wa More, bondeni. Bwana akamwambia Gideoni, Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno hata nikawatie Wamidiani katika mikono yao, wasije Israeli wakajivuna juu yangu wakisema, Mkono wangu mwenyewe ndio ulioniokoa. Basi sasa enda, tangaza habari masikioni mwa watu hawa, na kusema, Mtu awaye yote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke katika mlima wa Gileadi. Ndipo watu ishirini na mbili elfu wakarudi katika watu hao, wakabaki watu elfu kumi (Waamuzi 7:1-3).

Mungu akamwambia Gideoni, “Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno.” Enda utangaze, “Mtu awaye yote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke” (Waamuzi 7:3).

Waliorudi ni elfu ishirini na mbili. Elfu kumi walibaki na Gedeoni. Hayo ndiyo yaliyotendeka kwetu. Kanisa letu watu waliongezeka hadi 1,100 tulipokuwa tukikutana katika shule ya upili ya Le Conte. Lakini wengi wao waliogopa kuyahatarisha maisha yao kwa ajili ya Yesu. Wengine waliliacha kanisa letu kwa “mzaha” – ama ngono – ama dawa za kulevya. Wale waliotoka walielezwa na Yesu katika mfano wa mpanzi. Katika Luka 8:10-15 mfano huo umeelezwa. Aina ya kwanza ya watu ni wale ambao ulisikia neno la Mungu, na Shetani anakuja na kuliondoa neno ndani ya mioyo yao “wasije wakaamini na kuokoka.” (Luka 8:12). Tunayaona haya karibu kila wiki. Wao huingia kanisani na kujishugulisha na kompyuta zoa badala ya kusikiliza mahubiri. Ama wanafunga macho yao na kufikiria mambo mengine. Neno la Mungu haliwafaidi chochote, kwa sababu walimwachilia Shetani akaling’oa neno la Mungu mioyoni mwao.

Aina ya pili ni wale ambao hulisikia neno la Mungu kwa furaha. Lakini hawana mizizi katika Kristo. Kwa hiyo wao huamini kwa muda. Lakini wanapojaribiwa wanaanguka.

Aina ya tatu ya watu ni wale ambao ulisikia neno na wanaenda zao. Alafu wanasongwa na waziwazi na mali na anaza za maisha, “na hawazai matunda yakakomaa.” Dkt. J.Vernon McGee alikuwa sahihi aliposema aina ya hawa watu watatu hawakuongoka. Wao ni namna ya watu wote walioliacha kanisa letu zamani. Maisha yao yanaonyesha ya kwamba hakuna aliyekuwa amepokea uongofu wa kweli. Walikuja tu kwa ushirika na furaha tuliyonayo kanisani. Lakini walipojaribiwa walienda kwa sababu hawakuwa wametubu na hawakuwa wamezaliwa mara ya pili. Wao ni namna ya wale watu elfu ishirini na mbili waliokuja kumsaidia Gideoni lakini wakaogopa kusimama na yeye na kuwa maaskari wa Mungu! Na askari wa msalaba!

“Bwana akamwambia Gideoni, Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno hata nikawatie Wamidiani katika mikono yao, wasije Israeli wakajivuna juu yangu wakisema, Mkono wangu mwenyewe ndio ulioniokoa” (Waamuzi 7:2).

Lakini bado kulikuwa na watu wengi. Mungu akamwambia Gideoni, “Hata sasa watu hawa ni wengi mno; uwalete chini majini, nami nitawajaribu huko kwa ajili yako” (Waamuzi 7:4). Kulikuwa na joto sana pale “karibu na mlima wa More, bondeni.” (Waamuzi 7:1). Waisraeli walikuwa na kiu sana. Watu wengi wa Gideoni walikimbia majini, wakainama na kujishikilia na mikono yao majini, walipokuwa wakiyanywa upesi. “Na hesabu ya hao waliokunywa kwa kuramba-ramba, wakipeleka mkono kinywani, ilikuwa watu mia tatu” (Waamuzi 7:6). Wengi wao walijishikilia na mikono yao majini kwa sababu walikuwa na kiu sana. Lakini ni watu mia tatu tu waliochota maji na mikono yao na wakanywa kwa mikono yao. Walijua walistahili kuweka vichwa vyao juu, ili wawe wakiwatazama Wamidiani.

“Bwana akamwambia Gideoni, Kwa watu hawa mia tatu walioyaramba maji nitawaokoa, nami nitawatia Wamidiani katika mikono yako; lakini watu hawa wote wengine na waende zao, kila mtu mahali pake” (Waamuzi 7:7).

Hapo ndipo mahali tutakapofika kuhusiana na hawa watu mia tatu wa Gideoni usiku wa leo. Wamidiani walikuwa pale katika ile bonde, “mfano wa nzige kwa wingi; na ngamia zao walikuwa hawana hesabu; mfano wa mchanga wa ufuoni, kwa wingi.” (Waamuzi 7:12). Usiku huo Mungu alilipeyana jeshi kubwa la Wamidiani mikononi mwa watu wa Gideoni mia tatu. Wamidiani walikimbilia maisha yao. Na Waisraeli wakawateka wakuu wa Wamidiani, Orebu na Zeebu, na wakakata vichwa vyao na wakampelekea Gideoni (Angalia Waamuzi 7:25). Mungu aliwapa ushindi kupitia kikosi dogo cha maaskari mia tatu tu!

Hapa kuna somo kwetu usiku wa leo. Makanisa mengi leo yanaongozwa na watu ambao nia yao nikuwa na watu wengi. Hawa ni Wamidiani wainjilisti. Wanafikiria ni lazima kuwa na mamia ya watu wanaoudhuria. Na bado hawana nguvu yeyote. Ingewafaa hawa wahubiri kufikiria kuhusu Gideoni na kikosi chake kidogo cha maaskari.

Jonathani S. Dickerson ameandika kitabu kisuri kitwacho Mwanguko mkubwa wa kiinjili (Vitabu vya Baker). Alitoa takwimu hizi. Leo ni asilimia saba tu ya vijana wanaoegemea Ukristo wa kiinjilisti. Asilimia arobaini na tano ya Wakristo wa kiinjilisti watakufa kwa miaka ishirini ijayo. Hiyo ina maana kwamba hesabu ya vijana Wakristo wa kiinjilisti watapungua kutoka asili mia saba hadi asilimia nne tu ama chini – isipokuwa watu wazaliwe upya kuwa wanafunzi” (ibid., uk. 144).

Kwa nini kumekuwa na kushuka kwa idadi ya vijana katika makanisa? Nina hakika ni kwa sababu hawajapewa motisha kuishi kama Wakristo. Lengo letu ni gani? Lengo letu katika kanisa hili ni kuwasaidia vijana kufikia kilele chao katika Kristo. Tuko hapa kutayarisha kikundi cha vijana kama jeshi la Gideoni. Tuko hapa kuwasaidia vijana kuja katika kanisa letu na kuwafanya wanafunzi wa Yesu. Watu tanaotaka kuwashirikisha katika jeshi la Kristo ni vijana. Ni vijana walio tayari kufanya jambo jipya na la kutia motisha. Yesu alisema,

“ Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate” (Marko 8:34).

Wale ambao hawatamani kumfuata Yesu, haijalishi inagharimu nini, wanastahili kuondolewa. Wale ambao wanataka kuangaliwa kama watoto ndio ninaowaita “wapokeaji.” Wale ambao ni “wapokeaji” hawataki kujikana. Hawataki kumtolea Yesu chochote. Ikiwa unataka kushughulikiwa milele, basi hili si kanisa lako.

Mke wangu Ileana alikuja katika kanisa letu alipokuwa na umri wa miaka kumi na sita tu. Kwa muda wa majuma matatu alikuwa anakuja kanisani mwenyewe. Hakuhitaji “kuchukuliwa” baada ya majuma matatu tu. Wakati huo huo akawa mtenda kasi katika kanisa letu. Akawa mhuduma katika huduma ya simu alipokuwa tu na miaka kumi na saba. Nilimuoa akiwa tu na miaka kumi na tisa. Wakati wavulana wetu mapacha walipozaliwa aliwaleta kanisani jumapili ya kwanza. Mwanangu Leslie hajawahi kosa kanisa tangu siku ile aliyo saliwa. Wesley amekosa tu kuja kanisani juma pili moja alipokuwa mgonjwa katika maisha yake yote. Wanawake wengine kadhaa walisema hiyo ni kazi nyingi. Walikaa na watoto wao nyumbani wanapokuwa na homa kidogo tu. Lakini mke wangu alilifanya jambo sawa na wengine walikosea. Watoto wao karibu wote waliliacha kanisa kuishi maisha ya kifinafsi. Vijana wangu wawili wako hapa katika kila ibada hadi siku ya leo. Wako hapa kwa sababu mke wangu ni mwanafunzi wa Kristo. Dkt. Kreighton L. Chan, ambaye tutakayemtunuku heshima anapoadhimisha siku yake ya kusaliwa ya miaka sitini kwa dakika chache sijazo, alisema haya kuhusu Bi. Hymers, “Nilimjua tu alipokuja katika kanisa letu mara ya kwanza. Alikuwa na upendo na aliendelea kuwa na upendo mkuu kwa Kristo na shauku kwa nafsi zilizopotea. Alipokuwa [kijana] alihusisha maisha yake na huduma katika kanisa letu kwa bidii...Vijana, hebu Bi. Hymers awe mfano kwenu. Mkiufuata mfano wake, kanisa letu litakuwa na siku za usoni angavu na zenye fahari.”

Kwa sababu tunasherehekea miaka sitini leo ya kusaliwa kwa Dkt. Chan ninaweza kusema yeye pia ni mfano mwema wa mwanafunzi wa Yesu anayengaa. Yeye ni Mchungaji aliyewekwa wakfu katika kanisa letu. Alikuwa mgonjwa sana alipokuwa mtoto. Alikuwa mgonjwa kiasi cha kwamba walimuweka katika kisaduku cha kioo wakati mwingi katika utoto wake. Alikuja kanisani kwetu akiwa kijana alipokuwa akisomea kuwa Daktari. Madaktari wale wengine walimwambia hatafikisha umri wa miaka thelathini. Angekuwa yule mtu mdhaifu tu aliyetaka kanisa limshugulikie. Lakini hapana! Alijihusisha na kazi kanisani na akawa mwanafunzi wa Kristo. Walimwambia asijichokeshe au angekufa kabla ya umri wa miaka thelathini. Lakini kazi ya Kristo ilimtia nguvu Dkt. Chan. Ameishi maisha mazuri, yenye nguvu kwa miaka thelathini zaidi kuliko ilivyodhaniwa. Alichukua msalaba wake na akamfuata Yesu. Na sasa anaketi katika jukwaa hili kama shujaa mwenye nguvu wa Mungu katika umri wa miaka sitini!

Ningeendelea na niwaambie kuhusu Bw. Mencia, and Bi. Salazar, na Bw. Ben Griffith, ambaye yuko likizo pamoja na mke wake leo. Ningewaambia kuhusu Bw. na Bi. Virgel Nickell, ambao walitukopesha kiasi kikubwa cha pesa kununua jengo hili. Bw. Nickell ako na miaka sabini na tano na anaugua ugonjwa wa kisukari – bali yeye ulipeleka gari lake zaidi ya saa moja ili kuwa katika kanisa letu kila Jumatano usiku, na kila asubuhi ya Jumapili, na kila Jumapili usiku. Ama ningewaambia kuhusu huyu kijana mchanga waajabu, Kasisi Johana Samweli Cagan ambaye hivi karibuni atachukua nafasi yangu kama Mchungaji wa kanisa hili. Watu hawa wote wamekuwa wanafunzi wa Yesu, na maaskari wa msalaba.

Mchungaji wangu Dkt. Timotheo Lin alisema, “Uchache ni bora kuliko wingi...Kila nafasi katika kila kiti inaweza kuwa imejaa kila Jumapili, lakini ukweli ni kwamba kuna tu watu wachache katika mkutano ya maombi...Hatuwezi kusema hivyo ni vizuri” (Siri ya ukuaji wa kanisa, uk. 39).

Angalia katika Bibilia nzima. Utaona tena na tena kwamba “uchache ni bora kuliko wingi.” Yesu aliwachukua wanafunzi kumi na mmoja na akaubadilisha ulimwengu kwa sababu wanafunzi Wake walikuwa tayari kufa kwa ajili Yake au kwa kusudi lake. Katika historia ya kanisa tunaona somo hilo hilo tu. Ni watu 120 walikuwapo katika Pentekoste. Ni Wakristo tu wachache waliokuwa na umoja walioanzisha harakati za kisasa za umishenari. Ni Wamethodisti wachache tu, kundi kidogo tu, walioanzisha Mwamko Mkuu. Ni watu wachache tu walimfuata Yakobo Hudson Taylor kupeleka injili katika maeneo ya ndani kule China.

Wale ambao hawataki kutoa kilicho bora kwa ajili ya Kristo wanastahili kuondolewa. Wale waliotaka kushughulikiwa kama watoto milele wanastahili kuondolewa. Wale ambao hawataki kutoka katika hali yao ya starehe wanastahili kuondolewa. Wao ni “wapokeaji” wakati wote ambao hawataki kutoa chochote kwa Kristo. Ikiwa tunataka kuwa na kanisa la wanafunzi ni lazima tuachilie “wapokeaji” waende, ili tuwe na vijana ambao watakaowapa changamoto Wamidiani wa mtido mpya mwororo wa kiinjilisti, na wawabadilishe. Ni lazima tuwatie motisha wanaotaka kumtumikia Yesu Kristo katika maisha yao. Na hatupaswi kuwahimiza wale wanaotaka tuwashughulikie kama watoto wadogo ambao hawakui! Ni lazima tuwahimize wanaotaka kuwa wanafunzi wa Yesu, na ni lazima tuwaachilie wale wengine waende nyumbani kama alivyofanya Gideoni!

Tafadhali simama na huimbe wimbo nambari 1 katika karatasi yako ya nyimbo, “Songa mbele, Mkristo Askari.” Huimbe huo wimbo!

Songa mbele, Mkristo askari, tayari kwa vita,
   Msalaba wa Yesu ututangulie:
Kristo aliye Bwana na mfalme anatuongoza dhidi ya adui;
   Songa mbele vitani, tazama bendera Yake imetangulia!
Songa mbele, Mkristo askari, tayari kwa vita,
   Msalaba wa Yesu ututangulie.

Kama jeshi kubwa la songa mbele kanisa la Mungu;
   Ndugu zangu, tunapitia mahali ambapo watakatifu walipitia;
Hatujagawanyika, tu mwili mmoja,
   Mmoja kwa tumaini na mafundisho, mmoja katika upendo.
Songa mbele, Mkristo askari, tayari kwa vita,
   Msalaba wa Yesu ututangulie.

Songa mbele basi, enyi watu, jiungeni na umati wetu ulio na furaha,
   Unganisheni sauti zenu na zetu katika wimbo wa ushindi;
Utukufu, sifa na heshima kwa Kristo Mfalme;
   Hivi kwa miaka mingi wanadamu na malaika wameimba.
Songa mbele, Mkristo askari, tayari kwa vita,
   Msalaba wa Yesu ututangulie.
(“Songa mbele, Mkristo askari” na Sabine Baring-Gould, 1834-1924).


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Noah Song:
“Songa mbele, Mkristo askari” (na Sabine Baring-Gould, 1834-1924).


MWONGOZO WA

JESHI LA GIDEONI!

GIDEON’S ARMY!

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

“Bwana akamwambia Gideoni, Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno hata nikawatie Wamidiani katika mikono yao, wasije Israeli wakajivuna juu yangu wakisema, Mkono wangu mwenyewe ndio ulioniokoa” (Waamuzi 7:2).

I.    Kwanza, mkengeuko, Waamuzi 6:12, 13.

II.   Pili, Mungu wa Bibilia bado Yu hai! Malaki 3:6; Waamuzi 7:1-3;
Luka 8:12; Waamuzi 7:4, 1, 6, 7, 12; Marko 8:34.