Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




BARAKA ZA MAISHA YANGU

THE BLESSINGS OF MY LIFE
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa katika maktaba ya Rais Richard Nixon,
Yorba Linda, California
Siku ya Bwana, Aprili 8, 2018
A sermon preached at the Richard Nixon Presidential Library,
Yorba Linda, California
Lord’s Day Evening, April 8, 2018


Tafadhali simama ninaposoma mstari huu muhimu katika maisha yangu.

“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”
   (Wafilipi 4:13).

Mnaweza kuketi.

Unaweza shangaa kwa nini nimechagua maktaba ya Nixon kusherehekea siku kuu yangu ya ukumbusho wa miaka sitini katika huduma. Ukisoma habari za maisha yangu utagundua jinsi nilivyopata andiko muhimu katika maisha yangu kutoka kwa Rais Nixon.

“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”
   (Wafilipi 4:13).

Baba yangu aliondoka nilipokuwa na umri wa miaka miwili. Si kuwahi kuishi nayeye tena. Niliishi tu na mama yangu hadi nilipofikisha miaka 12. Baada ya hiyo nilisafirishwa kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine, nikiishi na jamaa zangu ambao hawakunipenda. Nilihudhuria shule 22 tofauti kabla ya kuhitimu kutoka shule ya upili. Kila wakati nilikuwa yule “mtoto mgeni.” Nilikuwa yatima wa kweli. Lakini ukosefu uliokuwa mkubwa zaidi ulikuwa kukua bila baba. Nilikuwa peke yangu, bila usaidizi wowote au msaada. Lakini lililokuwa baya zaidi, Sikuwa na baba ambaye ningemuiga kama mfano. Hivyo nilianza kuwaangalia watu mashuhuri katika historia ili kutoka kwao nijue jinsi mwanaume anavyostahili kuwa. Watu hawa wakawa mashujaa kwangu.

Niliwaweka kuwa mifano ya kidunia na ya Kikristo. Mashujaa wangu wote walikuwa wanaume waliopitia majaribio makubwa na wakayashinda. Mashujaa wangu wa Kikristo walikuwa watu kama Ibrahimu Lincoln, Yohana Wesley, Richard Wurmbrand na Yohana R. Rice. Mashujaa wangu wa kidunia walikuwa Winston Churchill na Richard Nixon. Mmoja wa wale walizoziandika habari muhimu za maisha ya Nixon alisema, “Alikuwa mtu aliyejali mambo kiundani miongoni mwa watu wasiojali mambo kwa undani. La kushangaza ni kwamba aliweza kuwa mwanasiasa mashuhuri. Alikuwa mtu mwenye soni na aliyependa kusoma vitabu, alijua angeshindwa, angewekwa nje, na bado – kila wakati na pasipo kujali vizuizi – kuinuka tena.” Hapana, hakuwa Mkristo. Lakini, ndio, kila mara alirejea kupigana vita tena. Wafilipi 4:13 lilikuwa andiko muhimu sana la Bibilia kwa Nixon.

Nilipogundua ni kwa nini Rais Nixon alilipenda andiko hili sana, singeweza kumuchukia. Alishinda vikwazo vingi sana hivyo roho yake ilifungamana na roho yangu. Nyakati za giza katika maisha, kila mara nilifikiria, “Ikiwa Richard Nixon aliponea Watergate, naweza kuponea dhambi.” Newsman Walter Cronkite alisema, “Ikiwa wewe na mimi tungekuwa Richard Nixon, tungekuwa tumekufa.” Kwangu mimi alikuwa kielelezo kikuu cha ushupavu. Nixon alisema, “Mwanadamu hajaisha wakati ameshindwa. Anaisha wakati anaposalimu amri.” Hakuna chochote ambacho kingemsimamisha. Alipoteza katika uchaguzi wa Urais kwa John F. Kennedy mwaka wa 1960. Alipoteza katika uchaguzi wa gavana katika jimbo la California mwaka wa 1962. Alishinda Urais mwaka wa 1968. Aliondolewa kwa ofisi kwa sababu ya kashfa ya Watergate. Lakini kila mara alirejea tena. Hii ndio sababu, ingawa hakuwa Mkristo, ni mmoja wa mashujaa wangu wa kiulimwengu.

Mtume Paulo alisema,

“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”
   (Wafilipi 4:13).

Hiyo haimaanishi ningemea nywele katika kichwa changu! Haimaanishi ya kwamba ningeruka! Sikumaanisha ya kwamba ningefanya vyema katika hisabati! Mtume alimaanisha kwamba angefumilia katika majaribu yote, kwamba angetekeleza majukumu yake yote, kwamba angeshinda vizuizi vyote – kupitia Kristo aliyemtia nguvu. Na nimegundua ya kwamba hili ni kweli hata kwangu. Nashukuru Mungu kwa andiko hili. Lakini namshukuru Mungu zaidi kwa Kristo aliyenipa anitie nguvu! Sikuhitimu katika chuo, lakini Kristo alinipa nguvu nikarudia na nikapata shahada tatu za uzamifu. Sikuweza kuwa mjumbe wa Injili, lakini Kristo alinifanya kuwa chanzo cha nguvu kwa watu duniani kupitia tovuti yetu.

Na unavyoendelea kusoma kitabu changu, utaona ni kwa nini wimbo ulioimbwa na Bw. Griffith ni wimbo unaonipendeza.

Bwana ametuita; barabara yaweza kuwa baya
   Na hatari na huzuni zimo njiani;
Lakini Roho Mtakatifu wa Mungu atawafariji wanolegea;
   Tunamfuata Mwokozi na haturudi nyuma;
Bwana ametuita, ingawa shaka na majaribu
   Zinaweza zingira safari yetu, tunaimba kwa furaha:
“Songa mbele, tazama juu,” kupitia taabu nyingi;
   Wana wa Zayuni lazima wamfuate Mfalme wao.
(“Bwana amekuja” na Sara Doudney, 1841-1926).

Niliandika habari za maisha yangu kwa sababu mwanangu Robert aliniambie niandike. Sikufurahia kuiandika kwa sababu maisha yangu yalijawa na pingamizi nyingi, mapambano na uchungu. Mara nyingi nilihisi kuzitupa karatasi nilizokuwa nikiziandikia kwa sababu zilijaa maneno yasiopendeza. Lakini Yohana Samweli Cagan alisema, “Usiyatupe, Dkt. Hymers. Kinachohitajika tu ni sura nyingine moja. Zungumzia kuhusu wakati mama yako alisema ‘hesabu Baraka zako.’” Nilimsikiza Yohana na nikaiandika sura ya mwisho, ambayo nitakupa sasa kwa njia fupi.

Nilikuwa nimeketi kado ya kitanda cha mama yangu kule hospitalini. Zilikuwa siku chache baada ya sherehe za Shukurani. Tulikuwa tunaongea kuhusu mmoja wa watu waliotupendeza, Ibrahimu Lincoln, na jinsi Rais Lincoln alifanya sherehe za Shukurani kuwa sikukuu ya kitaifa. Tuliimba wimbo tulioimba katika sherehe ya Shukurani.

Wakati ambapo mawimbi ya maisha yanasukasuka,
Unapovunjika moyo, ukifikiri umepoteza yote,
Hesabu Baraka zako nyingi, zitaje moja moja,
Na utashangaa yale Bwana ametenda.
Hesabu Baraka zako, zitaje moja moja,
Hesabu Baraka zako, ona yale Mungu ametenda!
Hesabu Baraka zako, zitaje moja moja,
Hesabu Baraka zako nyingi, ona yale Mungu ametenda.
   (“Hesabu Baraka zako” na Johnson Oatman, Jr., 1856-1922).

Tulipomaliza kuimba wimbo, Mama alisema, “Oo, Robert, kwa hakika tuna mengi ya kushukuru katika maisha yetu.” Halafu tukaanza kuhesabu Baraka zetu “moja moja.” Alianza kushukuru kwa sababu ya wavulana wetu, Robert na Yohana. Halafu akashukuru kwa sababu ya Ileana, mke wangu. “Yeye yu mwema kwangu, Robert, na ni mke na mama mzuri.” Alishukuru Mungu ya kwamba aliishi nyumbani kwetu. Alishukuru Mungu kwa sababu ya kanisa letu. Alishukuru Mungu kwa sababu ya washirika wetu, “moja moja.” Halafu nikayatoa mambo mengi tuliyostahili kushukuru kwayo. Na tukaimba wimbo tena.

Hesabu Baraka zako, zitaje moja moja,
Hesabu Baraka zako nyingi, ona yale Mungu ametenda.

Kulikuwa usiku sana. Nilimbusu, na nilipokuwa nikitoka kwa hicho chumba alisema jambo ambalo sitawahi sahau siku zote nitakazoishi. alisema, “Robert, wewe ndiwe jambo lililo bora zaidi lililotendeka kwangu.” Machozi yalinitoka nilipokuwa nikitoka chumbani chake, na nikatoka nje ya hospitali katika huo usiku. Yalikuwa mazungumzo ya mwisho kati yangu na yeye. Alikuwa na kiharusi kikubwa baadaye usiku huo kilichoondoa uhai wake.

“Usitupe kitabu chako, Dkt. Hymers. Kinachohitajika tu ni sura moja. Simulia wakati mama yako alikwambia ‘hesabu baraka zako.’” Hivyo hapa kuna baraka za ajabu ambazo Mungu amenipa katika safari hii ya maisha.

Kwanza kabisa, Nashukuru Mungu kwamba mama yangu hatimaye aliokoka. Alikuwa na umri wa miaka themanini na nilifikiria hataongoka. Tulikuwa na Ileana na vijana wangu kule New York, mahali ambapo nilihubiri katika makanisa mengi. Nilipokuwa nikitembea tembea katika chumba chetu, Nilikuwa naombea wokovu wa mama yangu. Halafu, ghafla, nikajua ataokolewa. Niliomba “nikahisi upenyo” kama vile wangesema waombezi wa kale. Nilimpigia Dkt. Cagan nikamuuliza aende amuongoza mama yangu kwa Kristo. Hakuwahi kumsikiza hapo awali. Lakini wakati huu alimwamini Yesu. Ulikuwa mwujiza, kama ilivyo katika hali zote za uongofu halisi. Siku hiyo aliacha kuvuta sigara na kunywa pombe. Nimeambiwa na madaktari ya kwamba mlevi anayeacha kunywa pombe ghafla jinsi hiyo atakuwa na hali ya kutetemeka hasipopewa dawa aina ya phenobartal. Lakini hakutetemeka. Ulikuwa mwujiza. Hakuwahi kuvuta sigara nyingine wala kunywa pombe tena. Alisoma Bibilia yote mara kadhaa na aliandamana nami kuja kanisani mara nne kwa wiki. Nilimbatiza tarehe 4 Julai, iliyokuwa sikukuu aliyoipenda. Nashukuru Mungu kwa sababu ya uongofu wa mama yangu.

Pili, Nashukuru Mungu kwa sababu ya Ileana, mke wangu wa ajabu. Alihudhuria harusi niliyokuwa naunganisha. Kabla ya kufunganisha harusi nilihubiri ujumbe mfupi kutoka Yohana 3:16. Ni mahubiri ya kwanza aliyosikia kutoka kwa kanisa la Kiprotestanti. Aliitikia ule mwaliko na mara hiyo akaokolewa! Nilipomuulliza mara ya kwanza kama nimpose, alisema, “la.” Nilivujika moyo. Orlando na Irene Vazquez (ambao wako hapa usiku huu) walinialika kwenda nao kule Puerto Rico. Nilienda, lakini kila mara nilifikiria juu ya Ileana. Alikuwa anafikiria juu yangu, pia. Alisema, “Natumaini ataniuliza tena.” Nilimuuliza, na wakati huu alisema, “ndio.” Tumekuwa katika ndoa kwa miaka thelathini na tano. Humshukuru Mungu kwa sababu ya mke wangu aliye kipenzi changu kila siku! Aliniandikia waraka uliosema, “Robert, nakupenda na moyo wangu wote na nafsi yangu. Nakupenda wakati wote, Ileana.” Yeye sana sana anafanana na yule mwanamke muadilifu katika Methali 31. Unachohitaji kufanya ni kuisoma sura hiyo na utaona inasimulia mpenzi wangu, Ileana. Nitamtunza moyoni mwangu milele. Baba yake yuko hapa leo. Alisafiri umbali huo wote kutoka Guatemala ili awe hapa. Asante, Bw. Cuellar! Ndugu yake na jamii yake wako hapa pia. Asante, Erwin!

Tatu, nashukuru Mungu kwa sababu ya vijana wangu wawili, Robert na Yohana. Wao ni mapacha, na sasa wako na umri wa miaka thelathini na nne. Wote wawili wamehitimu na shahada kutoka Chuo Kikuu cha jimbo la California kule Northridge. Robert amemuoa msichana mrembo Mkorea anayeitwa Jin. Wazazi wake wako hapa leo, na vilevile ndugu yake na mkewe. Asanteni kwa kuja! Robert na Jin ni wazazi wa wasichana wawili, Hana na Sara. Nashukuru Mungu kwa kunipa wajukuu warembo hivi.

Kijana wangu mwingine ni Yohana Wesley, aliyepewa jina hili kutokana na Mhubiri mashuhuri wa Uingereza. Robert na Yohana wote wawili uhudhuria kila mkutano katika kanisa letu. Wesley ni mtu wa maombi. Yeye uomba na usoma Bibilia, kila mara kwa masaa kadhaa. Yeye ni Mkristo mzuri na ni rafiki yangu. Ninapendezwa na wana wangu wawili. Wao ni baraka ya ajabu kwa mke wangu na mimi.

Namshukuru Mungu kwa sababu ya Dkt. Christopher Cagan. Yeye ndiye ndugu maana sikuwa na ndugu. Yeye ni rafiki wangu wa dhati na mshiriki aliyekaribu nami. Tunaheshimiana sana kiasi cha kwamba mtu akimuita yule mwingine hatutumii majina yetu ya kwanza. Hata tukiwa peke yetu kila mara umuita Dkt. Cagan naye kila mara uniita Dkt. Hymers. Nashukuru Mungu kwa kunipa rafiki mwenye hekima na mwaminifu. Kila mmoja anamuelewa yule mwingine. Mimi na yeye tu watu wa maneno machache, na kila mmoja wetu utumia muda mwingi kwa maombi na kusoma Bibilia. Njia yake ya kufikiria sana sana ni ya kisayansi na hisabati. Sana sana mimi ni mtu wa maono na imani. Lakini tunafanya kazi pamoja vizuri. Tunashirikiana pamoja, kama vile Holmes na Watson, ama Johnson na Boswell (mtu Fulani aidha alisema, “Kama Laurel na Hardy ama Abbott na Costello,” waigizaji-wa zamani).

Mimi uanzisha na yeye anaimarisha. Nina mawazo yanayoegemea elimu ya vitabu. Yeye ana mawazo yanayo egemea hisabati. Yeye ufikiria mimi ni kiongozi. Nami ufikiria yeye ni mwenye ustadi. Ushirika wetu umekuwa wa baraka kwetu sisi wawili. Namshukuru Mungu kwa sababu ya Dkt. Christopher Cagan.

Nashukuru Mungu kwa sababu ya Yohana Samweli Cagan. Yeye ni mwana wa kwanza wa Dkt. and Bi. Cagan. Yohana ni huyu kijana mchanga anayeongoza ibaada hii. Aliwekwa wakfu jana kuwa mhudumu wa Kibaptisti. Kwa hiyo sasa yeye ni Kasisi Yohana Samweli Cagan! Yeye ni mhubiri mzuri na mshauri. Namhesabu Yohana kuwa “mwana” katika huduma. Yuko katika mwaka wa pili katika shule ya mambo ya dini ya Talbot katika Chuo Kikuu cha Biola. Yeye ni mwerevu sana. Si jambo la kushangaza, kwa sababu baba yake ana shahanda mbili za uzamifu na mama yake Judy ni Daktari wa matibabu. Yohana ni mwanafunzi wa alama ya A chanya. Ana mpango wa kupata shahada ya uzamifu katika elimu ya dini. Akiwa na miaka 24 Yohana amehubiri katika mikutano ya injili kule India, na Jamhuri ya Dominican, na mataifa matatu kule Afrika. Yeye uhubiri katika kanisa letu kila Jumapili asubuhi. Huwa pamoja naye kila adhuhuri ya Alhamisi, tukijadili mambo ya elimu ya dini na kazi ya huduma. Namshukuru Mungu kwa sababu ya Yohana. Yeye ndiye atakayekuwa Mchungaji wa hili kanisa baada yangu. Yeye ni rafiki yangu. Ni rahisi kama hivyo nimeeleza.

Nashukuru Mungu kwa sababu ya Nuhu Song. Yeye ni “mhubiri kijana.” mwingine wangu Noah anamalizia masomo yake katika chuo na hatimaye ataenda katika chua cha mafunzo ya Bibilia. Yeye na Yohana Cagan ni timu nzuri, na wataliongoza kanisa letu katika siku za usoni.

Nashukuru Mungu kwa sababu ya Nuhu, Haruni Yancy and Jack Ngann. Wao ndio mashemasi wetu wapya waliowekwa wakfu. Haruni ni rafiki wangu wa karibu. Yeye unitunza kama vile kuku aliye na kifaranga kimoja tu. Yeye ni mmoja wa marafiki wangu wa karibu. Jack Ngann ameoa na ana wana wawili. Na hapa kuna jambo ambalo pengine haujui. Sijamaliza bado! Mwaka ujao nitakuwa nalipanda kanisa jipya la Kichina katika nyumba ya Jack Ngann.

Yohana Cagan, Nuhu Song, Haruni Yancy, Jack Ngann na Ben Griffith ni washirika wangu katika maombi. Tunakutana kuomba kila Jumatano usiku ninakosomea nyumbani kwangu. Nashukuru Mungu kwa sababu ya watu hawa. Wamenisaidia kupenya katika nyakati ngumu, hasa nilipokuwa nikipewa matibabu ya saratani.

Nashukuru Mungu kwa sababu ya Dkt. Chan, Bi. Salazar na wale “39.” Dkt. Chan ndiye Mchungaji wetu msaidizi, anayesimamia uinjilisti na huduma ya kufuatilia watu kwa njia ya simu. Bi. Salazar ndiye anayesimamia huduma yetu ya Kiispania. Wale “39” ni wale watu waaminifu walioiokoa kanisa letu katika hali ya kufilisika kulipotokea mgawanyiko mkuu. Nashukuru Mungu kwa sababu ya kila mmoja wao. Nashukuru Mungu kwa sababu ya Bw. Abel Prudhomme. Yeye ndiye aliyesimamisha kanisa lisigawanyike. Na nashukuru Mungu kwa sababu ya Virgel na Beverly Nickell. Ndio wanandoa waliotukopesha pesha nyingi za kununua jengo letu la kanisa. Hawajawahi sitasita katika kutusaidia. Wao ni washirika walioheshimiwa wa kanisa letu.

Washirika wa kanisa letu takriban asili mia hamusini ni vijana walio na umri wa chini ya miaka thelathini. Nimefurahia kila wakati kuwachunga vijana. Kikundi tulichonacho sasa ni mojawapo ya vikundi vizuri nimewahi jua. Tuko na kikundi cha ajabu cha mashemasi. Tuna mashemasi wanane waliowekwa wakfu, na tunawabadilishana baada ya miaka miwili. Haruni Yancy ndiye mwenye kiti wa kudumu wa mashemasi, Hivyo yeye habadilishwi. Nashukuru Mungu kwa sababu ya watu hawa.

Watu wakongwe katika kanisa letu utusaidia pakubwa kwa mambo tunayoyafanya.Wanahudhuria kila mkutano. Wanaomba vizuri, na wanafanya kazi kwa bidii kulijenga kanisa letu. Sina woga ninapoacha ibaada ya asubuhi ya Jumapili mikononi mwa Yohana Cagan na babake, ninapoenda kule Montebello kuanzisha kanisa jipya la Kichina. Ninawaamini kabisa. Nitakuwa nakuja kuhubiri katika kanisa la kwanza Jumapili usiku.

Maisha yangu yote yanasunguka kati ya watu wa kanisa letu.Wao ndio “jamaa wangu.” Ni furaha kuu kwangu kuwa baba wa jamii kubwa jinsi hii. Yesu alisema,

“Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi” (Yohana 13:35).

Siwezi fikiria njia nzuri zaidi ya kumalizie ujumbe huu kuliko kuwaambia hadidhi ya kweli. Nilipokuwa nikihubiri katika kanisa la Open Door kule wilaya Marin, Kila mara nilichukua kikundi cha vijana kwende San Francisco kila usiku wa Ijumaa na Jumamosi. Nilihubiri kwa barabara na hao vijana walikuwa wanapeyana makaratasi ya ujumbe wa injili. Kila mara tulienda Ufuoni wa bahari ulio Kasikasini mwa mji. Palikuwa mahali pa kupendeza, mahali ambapo watu walitumia madawa ya kulevya, na kulikuwa na vipande viembamba vingi vya buatani vilivyo “gawanyishwa”. Kila wakati nilihubiri katika njia iliyokuwa kado ya bustani iliyoitwa “Bustani ya Edeni”!!!

Usiku mmoja baadhi ya vujana walimleta kijana aliyekuwa mchnga kwangu. Aliniambia alikuwa ameyazoea madawa ya heroini yaliyokuwa gali mno. Aliniambia alitaka kuachana na kutumia hisi dawa. Nilipokuwa nikiongea na yeye niliona ya kwamba alikuwa anaongea ukweli. Mwishowe jioni nilimwambia aingie kwa gari langu na nikaenda naye katika chumba changu. Nilimweka jikoni, nikafunga mlango wa chumba change cha kulala, na nikalala.

Siku kadhaa zilizofuatia alipitia hali ngumu akiwa ameketi kwa sakafu jikoni kwa sababu mwili wake ulikuwa umezoea madawa ya kulevya. Mwishowe alitulia na akauliza ikiwa kuna mtu aliye na gitaa. Niliuliza watoto wetu wamletee moja. Aliketi sakafuni akiipigapiga kwa siku kadhaa. Halafu akauliza kitabu cha nyimbo. Tulimletea kimoja na akaanza kutafuta mdundo wa mojawapo ya zile nyimbo. Nilisahau jina halisi la yule kijana. Kila mara nilimuita MK, mkato wa mlevi wa kasumba!

Halafu siku moja MK aliniambia, “Sikiliza hii.” Akachukua gitaa, akafungua kitabu cha nyimbo, na akaimba wimbo wa Albert Midlane’s (1825-1909), “Fufua kazi Zako” kwa mdundo huu mpya. Ulikuwa mzuri kabisa! Tunaimba huo wimbo kwa mdundo wa MK hadi siku ya leo!

Fufua kazi zako, Ee Bwana! Mkono wango wenye nguvu wainua;
   Nena na sauti inayofufua wafu, Wawezeshe watu Wako kusikia.
Fufua! fufua! Na unyunyize mvua wa ufufuo;
   Utukufu wote utakuwa Wako; Baraka zitakuwa zetu.
(“Fufua kazi zako” na Albert Midlane, 1825-1909).

Nilipokuja Los Angeles, sikuweza kupatana na MK tena. Maisha yaliendelea na mwishowe kanisa letu likawekwa katika jingo tunalomiliki sasa. Simu ilipiga kengele usiku mmoja. Nilipanda ofisini mwangu na nikasema, “Hello.” Sauti katika ile simu ikasema, “Hujambo, Dkt. Hymers, huyu ni MK.” Nikauliza, “Nani?” Alisema, “MK. Unakumbuka, Mlevi wa Kasumba – MK.” Nilikuwa karibu nianguke. Sikuwa nimesikia sauti hii kwa karibu miaka thelathini! Nikamuuliza, “Uko wapi?” Akasema, “Niko Florida. Nimeoa. Nina watoto kadhaa, na mke mwema. Na ufundisha watoto kanisani kwetu.”

Nilicheka kwa furaha! Nilienda nikiimba njiani usiku huo mpaka nikafika nyumbani! Ni wakati kama huu ambao unifanya nifurahi kwamba niliingia katika huduma miaka 60 iliyopita. Hili lilistahiki mateso na maumivu hata hivi! Kuwakomboa vijana, kama MK, ni jambo ambalo limefanya furaha yangu kuwa kamilifu!

Uchungu na huzuni uniondokea ninapofikiria kuhusu watu wengi waliowachanga ambao wameokoka. Miaka yangu sitini katika huduma imekuwa wakati wa furaha. Singebadilisha huduma na jambo lingine!

Kama ilivyo kawaida, Ni lazima nichukue dakika kadhaa kueleza Injili. Yesu alikuja kutoka mbinguni kwa sababu ya jambo hili moja – Alikuja kufa msalabani kulipa deni ya dhambi zetu. Alifufuka kimwili, mwili na mifupa, siku ile ya jumapili ya pasaka. Alimwaga damu Yake ya thamani kutuosha kutoka kwa dhambi zote. Alituambia tumwamini, na tutatakaswa kutokana na dhambi zote.

Nilijaribu kujipatia wokovu kwa kuwa mkamlifu. Nilikuwa Mfarisayo. Lakini siku ya Septemba 28, 1961 kule Chuo cha Biola, Nilimwamini Yesu. Ni wimbo huu ulionileta kwa Kristo:

Roho yangu ilifungwa muda mrefu
   Ilifungwa kikiki kwa dhambi na usiku wa asilia.
Macho Yako yalitoa mwanga wa uamsho,
   Niliamka, jela ilijaa miali ya nuru.
Nyororo zangu zikaanguka, moyo wangu ukawa huru,
   Niliamka, nikaendelea, na nikakufuata Wewe.
Upendo wa ajabu! Inaweza kuwa aje
   Ya kwamba, Mungu wangu, ukafa kwa ajili yangu?
(“Na inawezekana?” na Charles Wesley, 1707-1788).

Yesu alikuwa Mungu katika mwili. Alikufa kwa ajili yangu. Nilimfikiria kwa njia mpya. Nilimwamini Kristo. Ni maombi yangu kwamba utamwamini Yesu na uokolewe. Halafu uhakikishe umejiunga na kanisa linaloamini Bibilia na humuishie Yesu Kristo katika maisha yako.

Na kwenu nyote ninasema, “Mungu awabariki kama vile amenibariki dhidi ya mateso yote na woga wote.” “Hakuna furaha kuu kuliko kusikia ya kwamba watoto wangu wanatembea katika ukweli” (III Yohana 4). Amina.

Na sasa nitamrudishia Kasisi Yohana Cagan utaratibu, ili ahitimishe ibaada hii. (Yohana anatangaza siku ya kusaliwa kwa Dkt. na Bi. Hymers akiwa na keki mbili, na akasema “Furahini katika siku hii ya kusaliwa kwenu.”)


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Maandiko yalisomwa kabla ya Mahubiri na Bw. Yohana Wesley Hymers: Zaburi 27:1-14.
Wimbo ulioimbwa kabla ya Mahubiri na Bw. Benjamin Kincaid Griffith:
“Ni Lazima Yesu Auchukue Msalaba peke Yake?”
(na Thomas Shepherd, 1665-1739; ubeti wa kwanza na wa mwisho)/
“Bwana Amekuja” (na Sarah Doudney, 1841-1926; beti mbili za mwisho).