Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




HUZUNI KATIKA GETHSEMANE

THE SORROW OF GETHSEMANE
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Jumamosi Jioni, Machi 18, 2017
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Saturday Evening, March 18, 2017

“Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu” (Waebrania 5:7).


Usiku ule kabla Yesu hajafa Msalabana aliwaongoza Wanafunzi wake katika giza cha Bustani ya Gethsemane. Kulikuwa usiku sana, usiku wa manane. Yesu aliwaacha Wanafunzi wake wanane ukingoni mwa Bustani. Aliwachukua Petro na Yakobo na Yohana wakaingia ndani zaidi katika Bustani ya Gethsemane. “Akaanza kufadhaika sana na kuhangaika” (Marko 14:33). Aliwambia hao Wanafunzi watatu, “Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa” (Marko 14:34). Alienda mbele hatua chache na kuanguka kifudifudi. Aliomba kwa maumivu ya kwamba ikiwezekana “saa hiyo imwepuke” (Marko 14:35). Muda wote walioutumia kwa maombi katika ile Bustani ya Gethsemane ulikuwa kama saa moja – kwa maana Yesu aliwaambia, alipowapata wakiwa wamelala, “Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?” (Mathayo 26:40).

Jambo la kuogofya lilimpata Yesu – usiku wa manane katika Bustani ya Gethsemane. Yesu alisema, “Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa” (Mathayo 26:38). Neno la Kiyunani “perilupos” lina maana “kuzungukwa na huzuni.” Angesema pamoja na mtunga zaburi, “Shida za kuzimu zilinipata” (Zaburi 116:3). Mawimbi ya huzuni yalimzingira. Juu yake, chini yake, kando yake, nje yake, na ndani yake – yote yalikuwa huzuni – hata kiasi cha kufa – huzuni kiasi cha kwamba ilikuwa karibu kumuua! Hakukuwa na njia ya kuepuka uchungu! Hakuna majonzi ambayo yangekuwa mabaya kuliko haya! Alibanwa sana na hofu hii na “hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini” (Luka 22:44).

Ni usiku wa manane, ukingoni mwa Mizeituni
   Mwangaza wa nyota ulififia usiku ule;
Ni usiku wa manane Bustani sasa,
   Mwokozi anayeteseka yu aomba pekee.

Ni usiku wa manane; na ametenganishwa na wote,
   Mwokozi apambana pekee katika maombi;
Hata yule mwanafunzi aliyependa
   Hakujali huzuni na machozi ya Bwana wake.
(“‘Ni usiku wa Manane; Ukingoni mwa Mizeituni”
      na William B. Tappan, 1794-1849).

Biblia inatuambia ya kwamba Yesu alikuwa “Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko” (Isaya 53:3). Lakini hakuonekana kila mara akiwa mwenye uso ulio na huzuni. Alijua sikitiko. Alijua huzuni. Lakini wakati mwingi Yesu alikuwa na amani, na mtu mwenye furaha. Alihudhuria sherehe nyingi hadi Mafarisayo wakalalamika. Wakisema, “Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi” (Mathayo 11:19, n.k., n.k.). Hili linaonyesha ya kwamba Wakristo halisi wanastahili kuwa watu wenye furaha muda mwingi. Wakati mwingine tunapitia hali ya unyong’onyevu. Lakini tunaweza kuwa na furaha tena tunapokumbuka ya kwamba Yesu alifufuka na kushinda kifo!

Lakini katika Bustani ya Gethsemane mambo yote yalibadilika. Amani yake imetoweka. Furaha yake imebadilika na kuwa majonzii yanayovuruga. “Perilupos” – amezungukwa na huzuni; amefinywa karibu kufa! Huu ndio mfano wa majonzi mtu anayopitia anapohukumika kwa sababu ya dhambi.

Yesu hakusema neno lolote kuhusu huzuni au unyong’onyevu katika maisha yake yote. Lakini sasa, katika ile Bustani, yote yamebadilika. Alimlilia Mungu, “Ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke” (Mathayo 26:39). Hakuwahi kulalamika hapo awali. Lakini sasa “akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini” (Luka 22:44). Kwa nini? Kwa nini? Yesu, ni nini inayosababisha mateso yako?

Dkt. Yohana Gill alisema ni kwa sababu Shetani alikuja katika ile Bustani. Katika wakati huu wetu Mel Gibson, katika sinema yake “Maumivu makali ya Kristo,” inamwonyesha Shetani akiingia Gethsemane kama nyoka, kumtesa Yesu pale gizani. Lakini Dkt. Gill na Mel Gibson wamekosea wanapotoa hiyo hoja. Shetani hakuwa katika Bustani ya Gethsemane. Hilo haliko katika Biblia. Watu wengine wananukuu Luka 22:53, Wakati Yesu aliwaambia maaskari waliokuja katika ile Bustani kumkamata, “Lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza” (Luka 22:53). Wako sawa wanaposema hili linamzungumzia Shetani. Lakini angalia kwamba Kristo alisema haya kwa wale maaskari waliokuja kumkamata baada ya maombi na hari ya matone ya damu pale Gethsemane. Baada ya maumivu yake katika ile Bustani, Aliwaambia wale maaskari, “Hii ndiyo saa yenu [sio saa ya Gethsemane], na mamlaka ya giza.” Hivyo Shetani alikuja baada ya maumivu ya Kristo katika ile Bustani. Yuda alipagawa na pepo (hasa, alipagawa na Shetani) siku chache kabla. Tunaambiwa katika Luka 22:3, “Shetani akamwingia Yuda.” Shetani alienda pale Bustani baada ya Kristo kuwa na mapambano ya kutisha, akiwa amempagawa Yuda na kuwavuta askari kumkamata Yesu na kumfedhehesha.

Kwa hivyo, bado tunabaki tukishangaa ni kwa nini Yesu aliteseka hivyo kiasi cha kwamba hari yake ikawa matone ya damu alipokuwa akiomba akombolewe. Nina hakika ya kwamba jibu limepeyanwa katika andiko letu. Katika Bustani, Yesu “akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke” (Mathayo 26:39). “Kikombe” hiki kilikuwa ni nini? Ikiwa ni mateso yake Msalabani siku iliyofuata, maombi yake hayakujibiwa. Ikiwa “kikombe” kilikuwa kukombolewa kutokana na Shetani usiku huo, maombi yake hayakujibiwa, kwa sababu watu waliopagawa pepo walimchukua wakaenda kumsulubisha. Andiko letu katika Waebrania 5:7 linapeyana jibu. Tafadhali simama na uisome kwa sauti.

“Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu” (Waebrania 5:7).

Mnaweza kuketi. Sasa, andiko linatwambia ya kwamba Yesu aliomba ombi hili “siku hizo za mwili wake” – yaani, alipokuwa akiishi hapa duniani. Aliomba kwa “kilio kikuu na machozi” aokolewe na kifo – hivyo hili ombi liliombwa kabla hajasulubishwa. Andiko linatwambia ya kwamba ombi lake lilisikika, na Mungu akamwokoa na kifo katika Bustani ya Gethsemane! Dkt. J. Oliver Buswell, mwana theolojia mashuhuri, alisema hivi,

Jasho iliokithiri iliyomtoka kama inavyoelezewa na Luka [katika Bustani ya Gethsemane] ni kawaida kwa mtu aliyekatika hali ya mshituko ambapo mwenye kuteseka ako katika hatari ya kuzimia na hata kufa...Bwana wetu Yesu Kristo, alipojipata katika hali hii ya mshituko mkuu wa mwili, aliomba kukombolewa kutoka kwa kifo pale Bustani, ili aweze kukamilisha kusudi lake msalabani (J. Oliver Buswell, Ph.D., Theolojia ya Utaratibu wa Dini ya Kikristo, Zondervan Publishing House, 1971, sehemu ya III, uk. 62).

Dkt. Yohana R. Rice alisema jambo linalokaribiana na hilo,

Yesu alihuzunika na kuwa na uzito na nafsi yake ilikuwa na “huzuni nyingi kiasi cha kufa,” yaani, ilikuwa hasa inakufa kwa majonzi...Yesu aliomba kwamba kikombe kimwepuke usiku huo aweze kuishi ili afe msalabani siku iliyofuatia (Yohana R. Rice, D.D.,Injili kulingana na Mathayo, Upanga wa Bwana, 1980, uk. 441).

Dkt. Buswell alisema,

Tafsiri hii ingeoanisha Waebrania 5:7, na inaonekana ndiyo tafsiri inayooanisha (ibid.).

Dkt. Rice alisema,

Hili limewekwa wazi na Waebrania 5:7 ambapo tunaambiwa ya kwamba Yesu alitoa “maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu.” Alipokuwa karibu kufa katika Bustani ya Gethsemane, Yesu aliomba kwamba kikombe cha kifo kimwepuke usiku huo ili apate kuishi na kufa msalabani siku iliyofuatia. Maandiko yanasema “Akasikilizwa”! Mungu alijibu maombi yake (ibid.).

“Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu” (Waebrania 5:7).

Mtazame Mwana wa Mungu anayeteseka,
   Akihema, akiugua, akitokwa na hari ya damu!
Vilindi vya neema ya Mungu isiyo na mipaka!
   Yesu, upendo huu wako ulikuwa wa namna gani!
(“Mateso Yako Yasiyojulikana” na Yusufu Hart, 1712-1768).

Lakini ni lazima bado tueleze ni kwa nini Yesu aliteseka kiasi hicho usiku huo. Hapa kuna kile ninachoamini kilimtendekea Yesu katika ile Bustani. Nina amini hapo ndipo

“Na BWANA ameweka juu yake maovu yetu sisi zote” (Isaya 53:6).

“Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu” (Isaya 53:4).

Lakini ni lini aliyachukua? Aliyachukua pale Gethsemane, na akayabeba Msalabani asubuhi iliyofuatia.

“Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti” (I Petro 2:24).

Lakini dhambi zetu ziliwekwa “katika mwili wake” usiku huo, katika Bustani ya Gethsemane. Alichukua dhambi zetu kutoka Gethsemane hadi Msalabani! Aliridhisha ghadhabu ya Mungu. Aliichukua yote.

Ni Mwokozi pekee aliyeomba gizani pale Gethsemane;
   Pekee alikimimina kikombe chungu, Na aliteseka pale kwa ajili yangu;
Pekee, pekee, Alikichukua pekee;
   Alijitolea kuokoa kilichochake;
Aliteseka, alimwaga damu na kufa, Pekee, pekee.
   (“Pekee” na Ben H. Price, 1914).

Dkt. Yohana Gill (1697-1771) aliyekuwa mashuhuri alisema vizuri,

Sasa amechubuliwa, na kutiwa katika majonzi na Baba yake: ameanza kuhuzunika sasa, maana huzuni haikukoma pale, lakini pale msalabani,...na kuwa na uzito sana; kwa sababu ya uzito wa dhambi za watu wake, na ile hali ya ghadhabu ya Mungu, ambayo ilimfinyilia na kumgharikisha, kiasi cha kwamba roho yake ilikuwa karibu kutoka; alikuwa tayari kuzimia, kuzama na kufa; moyo wake ulilemewa...nafsi yake ilisongwa pande zote na dhambi za watu wake; haya yalimkamata, na kumzunguka...huzuni za kifo na jahanamu zilimzunguka kila upande, kiasi cha kuwa hakuna hata tone la farajalililokuwa ndani yake...hivyo nafsi yake ilizongwa na huzuni; moyo wake uliokuwa mkuu ulikuwa karibu kuvunjika; aliletwa chini, kama ilivyokuwa, kwa mavumbi ya kifo; wala huzuni zake hazikumwacha, hadi pale nafsi yake na mwili wake zilipotenganishwa (Yohana Gill, D.D., Maelezo kuhusu Agano Jipya, The Baptist Standard Bearer, sehemu I, uk. 334).

Hivyo tunajifunza yale Yesu aliyafanya kutuokoa na ghadhabu ya Mungu, kutokana na hukumu kwa sababu ya dhambi zetu, na adhabu ya milele katika Jahanumu. Aliteseka kwa ajili yetu, akachukua mahali petu. Mateso aliyoteseka kwa ajili ya watu, mahali petu, yalianza katika Bustani ya Gethsemane, mahali ambapo alizichukua dhambi zako na kuzipeleka Msalabani asubuhi iliyofuatia.

Rafiki yangu, tunakaribia Jumapili ya Pasaka, siku ambayo Yesu alifufuka kutoka kaburini. Lakini kufufuka kwake kutoka kwa wafu hakutakuwa na maana yeyote kwako pasipo wewe kujua ya kwamba aliteseka vibaya pale Gethsemane na Msalabani kukuokoa ili usiadhibiwe kwa sababu ya dhambi zako. Unahitaji kufanya nini ili Yesu awe alikufa badala yako? Lazima uanguke miguuni pake na umwamini!

Ninapouangalia msalaba wa ajabu
   Mahali ambapo Mfalme wa utukufu alikufa,
Utajiri wangu wote nauhesabu kuwa hasara,
   Na kumiminia dharau kiburi changu.

Zuia, Bwana, kwamba nisiwe na kiburi,
   Ila tu kwa kifo cha Kristo, Mungu wangu;
Mambo yote ya bure yanayonipendeza zaidi,
   Nayatoa dhabihu kwa damu yake.

Tazama, kutoka kichwani Mwake, mikononi Mwake, miguuni Mwake,
   Huzuni iliyo changanyika na upendo ilitiririka;
Je, upendo wa namna hii na huzuni zilikutana,
   Ama miiba kutengeneza taji nzuri hivyo?

Hata ingekuwa dunia yote ni yangu,
   Ingekuwa zawadi ndogo mno kwangu;
Upendo wa ajabu, wa Mungu,
   Nafsi yangu yahitaji, maisha yangu, vyote vyangu.
(“Ninapouangalia Msalaba wa Ajabu” na Isaac Watts, D.D., 1674-1748).

Mwamini Yesu usiku wa leo na dhambi zako zitalipiwa kupitia mateso yake na kifo chake mahali pako – pale Msalabani. Damu yake itakuosha dhambi zako wakati ule ule utakapomwamini!


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo Ulioimbwa Kabla ya Mahubiri:
     “Ni usiku wa Manane, Ukingoni mwa Mizeituni”(na William B. Tappan, 1794-1849).