Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.
MAHUBIRI MATANO YALIYOTUMIKA KWA UONGOFU WA MWIJILISTI MCHANGA

FIVE SERMONS USED IN THE CONVERSION
OF A YOUNG EVANGELIST
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana jioni ya, Octoba 9, 2016
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Evening, October 9, 2016

“Tena wamsikieje pasipo mhubiri?” (Warumi 10:14).


Pengine mahubiri muhimu kabisa niliyowahi kuhubiri yalihubiriwa Juni, 2009. Mahubiri haya matano yalitumiwa na Mungu kwa uongofu wa kijana mchanga mliosikia akihubiri asubuhi ya leo. Haya ndiyo mahubiri matano Yohana Samweli Cagan aliyosikia muda mfupi kabla ya kupokea uongofu. Kwa kuwa nina uhakika Yohana atakuwa mhubiri mashuhuri, mahubiri haya matano yaliyotumika kwa uongofu wake pengine ndiyo ya muhimu kabisa nitakayowahi kuhubiri. Mahubiri ya uongofu ni nadra sana siku hizi. Lakini kuhubiri ndiyo njia kuu Mungu ametoa kwa kuokoa wenye dhambi. Bibilia inasema, “Tena wamsikieje pasipo mhubiri?” (Warumi 10:14). Mahubiri haya matano yafuatayo ndiyo hasa aliyoyasikia Yohana Cagan kabla ya kuokoka. Nitasoma ushuhuda wake wote mwisho wa ujumbe huu. Lakini kwanza nitakupa muhtasari wa haya mahubiri matano Yohana aliyoyasikia kabla ya kupokea uongofu. Maneno muhimu nitakayoyasema jioni hii ni kutoka kwa vichwa vya mahubiri haya matano.

I. Kwanza, “Kutiwa moyo kwa Wale ambao Hawako Mbali na Wokovu” (Yalihubiriwa Jumapili asubuhi ya, Juni 7, 2009).

Andiko la mahubiri haya lilikuwa “Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu” (Marko 12:34). Roho Mtakatifu kwa hakika alikuwa anafanya kazi ndani ya moyo wa huyu mtu, kwa sababu ni Roho wa Mungu tu anayeweza kuvunja upinzani mwanadamu alionao kwa Mungu pamoja na kule kumkataa Kristo. Mtu asiyeongoka ni muasi kwa Mungu na adui wa Kristo. Nilizungumza kuhusu kijana mwingine mchanga aliyeniuliza, “Kwa nini Yesu akafa msalabani?” Huyu kijana alinisikia nikisema “Kristo alikufa msalabani kulipa deni ya dhambi zetu.” Amenisikia nikirudia kusema haya maneno kwa miaka mingi, lakini hayakuwahi kupokelewa katika akili yake iliyopofushwa. Ni lazima ufikirie kwa undani hayo maneno, “Kristo alikufa msalabani kulipa deni ya dhambi zetu.” Ni nini inayokuzuia usije kwa Kristo? Unaogopa ni nini watu watasema? Sahau vile watakavyosema. Maneno yao hayatakuwa na maana yeyote utakapokuwa Jahanamu. Geuka kutoka kwa dhambi zako na uje kwa Kristo. Hakuna njia nyingine ya kuepuka Jahanamu.

II. Pili, “Ukalvini wa Kisasa na Uongofu Halisi” (Yalihubiriwa Jumapili jioni ya, Juni 7, 2009).

Andiko la mahubiri haya lilikuwa, “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya” (II Wakorintho 5:17). Si kuhubiri kinyume na mafundisho ya Ukalvini. Badala ya hiyo nilisema kuamini mafundisho hakutakuokoa. Hata kuamini mafundisho ya kweli hakutakuokoa. Nilisema ya kwamba kutosheka na mafundisho ya kweli hayatakuokoa. Ni lazima uhukumike kuhusu dhambi zako. Lazima uungame dhambi zako. Ni lazima uje kwa Yesu Mwenyewe ama utaende Jahanamu. Utakapochoka na dhambi zako – hasa, ni wakati huo tu – utakapotambua unamhitaji Kristo akuokoe. Ikiwa haumhitaji Kristo aubadilishe moyo wako muovu, hautawahi ongoka. Hauna aibu kwa sababu ya dhambi za moyo wako? Haikusumbui? Ni lazima ikusumbue ikiwa unatumaini kuongoka. Ni wakatu tu utakapochoka na dhambi za moyo wako ndipo Damu inayoosha ya Yesu itakuwa na umuhimu kwako. Spurgeon alisema, “Ni lazima kuwe na mabadiliko halisi ya moyo yatakayobadili maisha yako yote.” Uongofu halisi unapatikana wakati ambapo mwenye dhambi aliyepotea atahukumika kwa dhambi zake na kuzichukia.

Katika mahubiri hayo nilinukuu kifungu kutoka kwa mahubiri ya Spurgeon, “Je! Uongofu ni lazima?” Spurgeon alisema,

Katika hali zote za uongofu kamili kuna kanuni nne zinazokubaliana: katika zote lazima kuwe na kuungama kwa dhati kwa dhambi, na kumtazama Yesu kwa msamaha wa dhambi, na ni lazima kuwe na mabadiliko halisi ya moyo, yatakayobadilisha maisha yote ya baadaye, na kutakapokuwa na ukosefu wa hizi kanuni muhimu hakutakuwa na uongofu halisi (C. H. Spurgeon, “Je! Uongofu ni lazima?”, Metropolitan Tabernacle Pulpit, Pilgrim Publications, 1971, vol. xx, uk. 398).

III. Tatu, “Ni kwa Maombi na Kufunga tu” (Yalihubiriwa Jumapili asubuhi ya, Juni 14, 2009).

Andiko lilikuwa, “Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba na kufunga” (Marko 9:29). Nilisema haya maneno “na kufunga” yaliondolewa kwa sababu maadishi mawili ya zamani, yaliyonakiliwa na Waagnostiki wazushi, waliyaacha nje haya maneno mawili, hivyo kudhofisha makanisa yanayotumia Bibilia ya kisasa. Hata hivyo maandiko mengi ya zamani yana maneno “kuomba na kufunga”. Kule China haya maneno yako katika Bibilia. Na hiyo ndiyo sababu wana mfululizo wa ufufuo, nao walio katika nchi za magharibi, na tafsiri zao za kisasa wanapata uchache wa ufufuo wa kweli. Lakini ni lazima tuwe na wakati wa kuomba na kufunga kwa sababu ya vijana kanisani ili waongoke. Lazima tufunge na tuombe kwa ajili yao ili wahisi dhambi zao, watubu, na wawe na mapatano halisi na Mwokozi aliyesulubishwa na kufufuka, na waoshwe na Damu Yake ya thamani. Mahubiri yalimalizika kwa kusoma kifungu kutoka kwa wimbo, “Nyeupe kuliko theluji.” Wimbo huu unasema, “Bwana Yesu, waona nangojea kwa subira, Njoo sasa, na ndani yangu niumbie moyo mpya.” Lakini Wakristo walipokuwa wakifunga na kuomba katika kanisa letu, Yohana Cagan alichukizwa na kufunga. Hili lilimfanya awe na hasira – hata ingawa bado kidogo angalipokea uongofu maana wazazi wake waliomba na kufunga kwa sababu ya wokovu wake!

IV. Nne, “Dhamiri na Uongofu” (Yalihubiriwa Jumapili jioni ya, Juni 14, 2009).

Andiko lilikuwa, “Dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea” (Warumi 2:15). Dhamiri ni mfumo uliondani yetu unaohukumu maadili yetu, kwa kuridhia au kutoridhia matendo yetu, fikira au matendo, ikitujulisha kwamba tumefanya jambo mbaya, na ikitujulisha kwamba tunastahili adhabu. Adamu alitenda dhambi na dhamiri yake ikachafuliwa, hivyo alitoa sababu nyingi kwa sababu ya dhambi zake. Dhibitisho kwamba upotovu huu wa dhamiri yao uliendelezwa kwa kizazi cha mwanadamu ni kwamba mwana wao wa kwanza Kaini alimuua nduguye na hakuhukumika na akawa na visababu. Mtu anapoendelea kufanya dhambi ndivyo dhamiri yake uendelea kuchafuka na kupotoka. Watu unguza dhamiri zao wanapoendelea kufanya dhambi zaidi na zaidi, “kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe” (I Timotheo 4:2). Niliwaambia vijana kanisani kwetu kwamba waliunguza dhamiri zao kwa kuwandanganya mama zao, kudanganya shuleni, kwa kuiba vitu, kuiunguza dhamiri yako tena na tena na dhambi ovu zaidi – ambayo sitaitaja. Unasijua ni gani. Unajua ya kwamba imekaribia kuwa vigumu kwako kuhisi unahatia – kwa sababu umetenda dhambi mara kwa mara, ukimcheka Mungu unapoendelea kutenda dhambi mara kwa mara na kuiangamiza dhamiri yako. Ninaweza kufanya nini nikusaidie? Ni wewe umeiunguza dhamiri yako kupita kiasi. Naweza tu kukuhurumia – kama kiumbe kilichoangamizwa kisicho na mbele wala tumaini. Naweza tu kukuhurumia. Siwezi kukusaidia, kwa sababu umehukumiwa na adhabu yako imepitishwa tayari. Yesu alisema, “Asiyeamini amekwisha kuhukumiwa” (Yohana 3:18). Uko na hakika ya kwenda Jahanamu kama kwamba uko tayari uko. Na hakuna chochote ninachosema ama ninachofanya kinachoweza kukusaidia. Ni Mungu tu anayeweza kukusadikisha kuhusu dhambi zako. Ikiwa Mungu alikusadikisha hapo awali, hakuna uhakika kwamba atakusadikisha tena. Mara nyingi wale waliohisi hali ya kusadikishwa hawatembelewi na Roho wa Mungu tena. Baada ya dhihaka zote na ujinga ambao umefanya, hahustahiki ata nafasi moja ya kusadikishwa. Ukikosa ile hali ya kusadiki dhambi zako, huenda ikawa Mungu hatakupa hiyo nafasi tena. Kuja mbele za Mungu kama mwombaji! Kuja ukiwa mnyenyekevu, ukijua ya kwamba Mwenyezi Mungu hana deni na wewe. Umemtemea mate usoni Mwake katika moyo wako miaka hii yote. Hebu fikiria kuhusu hilo! Umemtemea Kristo mate usoni Mwake kupitia nia yako. Sasa Kristo hana deni na wewe. Deni aliyo nayo yako ni ghadhabu, adhabu na miali ya moto wa Jahanamu. Sasa hivi unaweza kuwa unafikiria, “Ni kweli – Mungu hana deni nami yeyote isipokuwa miali ya moto wa Jahanamu. Sistahiki kingine chochote.” Halafu, ikiwa unahisi hivyo nakusihi uje kwa Yesu kama yule mwanamke alikuja kwa Yesu na kuibusu miguu Yake. Kuja ukiwa mnyonge jinsi ulivyo. Kuja ukilia na kuomboleza Kwake, kama alivyofanya Yohana Bunyan; kama alivyofanya Whitefield – ukilia na kupiga kiyowe. Pengine atakuhurumia. Lakini nasema tu “pengine” – kwa sababu wakati wako wa kuokolewa unaweza kuwa tayari umepita. Unaweza kuwa tayari umetenda dhambi na kuiipa kisogo siku ya neema milele. Kuja ukilia kwa Kristo – na pengine atakupa nafasi nyingine – ingawa katika hali yako hakuna uhakika ya kwamba atakupa. Teremka uje hapa mbele ya mimbari. Piga magoti na umwambie Mungu ukuhurumie. Kristo anaweza kukusikia na akupe nafasi nyingine ya kutakaswa na Damu Yake Takatifu. Ni Damu Yake tu “itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai” (Waebrania 9:14).

V. Tano, “Bonde la Mifupa Mikavu” (Nilihubiri mahubiri haya asubuhi ile Yohana Cagan aliongoka, Juni 21, 2009).

Andiko lilikuwa, “Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi” (Ezekieli 37:5). Si fikiri Yohana alikuwa ameongoka hadi mwisho wa mahubiri haya. Sifikiri kwa hakika alikuwa anayasikiliza. Nafikiri yalikuwa mahubiri yale ya kwanza manne yaliyotumika kwa uongofu wake. Utayaona kwa ushuhuda wa Yohana nitakapousoma – hakuniheshimu. Kwa kweli, Yohana alinichukia. Nilipokuwa nikihubiri mahubiri haya alisema, yeye “alijaribu kwa makusudi kuyakataa, hakutaka kuyasikiza...nilihesabu sekunde hadi mwisho wa mahubiri, lakini Mchungaji aliendelea kuhubiri.” Hiyo ndiyo sababu hakutaja chochote nilichosema asubuhi hiyo kwa ushuhuda wake. Hakutaja hata neno moja. Yohana alisema, “Hata mwaliko ulipofanywa nilikuwa nakataa.” Na akasema, “Mchungaji alinishauri, na akaniambia nije kwa Kristo, lakini singeweza.”

Hii ina umuhimu. Ina umuhimu kwa sababu hivyo ndivyo wengi wenu wanavyo hisi sasa hivi. Hamniheshimu. Hamnipendi. Hamtaki kunisikiliza.

Lakini jambo lingine lilitendeka kwa Yohana asubuhi hiyo. Nafikiri ningesoma kurasa chache kutoka kwa kitabu cha simu na angaliongoka. Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu mahubiri manne yaliyopita yalikuwa yamegusa moyo wake, hasa yale mahubiri yangu ya dhamiri. Unaona, Mungu mwenyewe alitumia mahubiri haya pamoja na yale mengine matatu kumfanya afikirie kuhusu dhambi zake. Na akagundua ya kwamba hakuwa anashindana nami. Aligundua alikuwa anashindana na Mungu. Sasa sikiliza ushuhuda wake na utaona ya kwamba mimi mwenyewe nilikuwa na machache sana kuhusu uongofu wa Yohana. Ni Mungu aliyesababisha yale mahubiri ya kwanza manne yamsadikishe kuhusu dhambi. Mungu ndiye aliyetumia maneno yangu madhaifu kumleta huyu kijana wa miaka kumi na tano kusadiki kuhusu dhambi. Ni Mungu ambaye wakati huo “kwa nguvu sana [alimvuta] kwa Kristo.” Haikuwa mimi kabisa. “Tena wamsikieje pasipo mhubiri?” ni ukweli. Lakini ni Mungu anayetumia mahubiri ya mhubiri kuwaokoa wenye dhambi. Kama vile nabii yona alisema, “Wokovu [hutoka] kwa Bwana” (Yona 2:9). Sasa fikiria kuhusu hilo ninaposoma ushuhuda wote kuhusu kuongoka kwa Yohana Samweli Cagan.

USHUHUDA WANGU
Juni 21, 2009
na Yohana Samweli Cagan

     Ninaweza kukumbuka wakati wa kuongoka kwangu kwa njia dhahiri na kamilifu na maneno hayatoshi yanapolinganishwa na utofauti Kristo alileta ndani mwangu. Kabla sijaongoka nilikuwa mwenye hasira na chuki. Nilijivuna kwa sababu ya dhambi zangu na nilifurahia kusababisha uchungu kwa watu, na nilijihusisha na wale ambao umchukia Mungu; kwangu dhambi haikuwa “makosa” ya kujutia. Kwa hiari nilikuwa nimejielekeza katika njia hii. Mungu alianza kufanya kazi ndani yangu kwa njia ambazo singedhania mambo yalipoanza kwenda mrama. Majuma hayo kabla ya uongofu wangu nilihisi kama nakufa: Singelala, singecheka, Singepata amani aina yeyote. Kanisa letu lilikuwa na mikutano ya injili na ninaweza kumbuka vizuri nikiwacheka na kutomheshimu Mchungaji wangu na baba yangu.
     Roho Mtakatifu alianza kwa njia dhahiri kunisadikisha kuhusu dhambi zangu wakati huo, lakini makusudi nilikataa mawazo yote niliyokuwa nayo kuhusu Mungu na uongofu. Nilikataa kuhifikiria, bado singeacha kuhisi kuhangaika. Kufikia Jumapili asubuhi ya Juni 21, 2009, nilikuwa nimechoka kabisa. Hayo yalinichokesha kabisa. Nilianza kujichukia, kuchukia dhambi zangu na jinsi zilivyonifanya kuhisi.
     Wakati Dkt. Hymers alipokuwa akihubiri, kwa kiburi changu nilikuwa nakataa ule ujumbe, kukataa kuusikiza, lakini alivyoendelea kuhubiri nilihisi dhambi zangu zote nafsini mwangu. Nilikuwa nikihesabu sekunde ifikie mwisho wa mahubiri, lakini Mchungaji aliendelea kuhubiri, na dhambi zangu zikaendelea kuwa mbaya zaidi. Singeweza tena kupiga mchokoo, ilibidi niokolewe! Hata mwaliko ulipokuwa ukifanywa nilikataa, Lakini singeweza kuvumilia tena. Nilijua ya kwamba mimi ni mwenye dhambi mbaya kabisa na kwamba Mungu ako na haki ya kunipeleka Jahanamu. Nilikuwa nimechoka na kupinga, nilikuwa nimechoka na jinsi nilivyokuwa. Mchungaji alinishauri, na akaniambia nije kwa Kristo, lakini singeweza. Ingawa dhambi zangu zote zilinihukumu bado singempokea Yesu. Wakati huo ulikuwa mbaya kupita wakati mwingine wowote na nilihisi kama singeokolewa na ningeenda tu Jahanamu. Nilikuwa “najaribu” kuokolewa, nilikuwa “najaribu” kumwamini Kristo lakini singeweza, singeweza kumwelekea Kristo, singeweza kuamua kuwa Mkristo, na hilo lilinifanya nikose tumaini. Nilihisi dhambi zangu zikinisukuma kwenda Jahanamu na bado nilihisi ukaidi wangu ukiyaondoa machozi yangu. Nilikwama katika hitilafu hii.
     Ghafla maneno ya mahubiri yaliyohubiriwa miaka kadhaa iliyopita yakaingia katika mawazo yangu: “Kubali Kristo! Kubali Kristo!” Lile wazo kwamba ningejisalimisha kwa Yesu lilinitia dhiki kwamba kile kilichoonekana ni cha milele singaliweza. Yesu aliachilia uhai Wake kwa ajili yangu. Yesu mwenyewe alienda kusulubiwa kwa ajili yangu nilipokuwa bado adui Wake na singemkubali. Wazo hili lilininyenyekesha; Ilibidi nijiachilie. singengangana tena, ilibidi nimpokee Yesu! Wakati huo nilijiachilia kwake na nikaja kwa Yesu kwa imani. Wakati huo ilionekana kama ningalijiachilia nife, halafu Kristo akanipa uhai! Hakukuwa na matendo ama kusudi kwa mawazo yangu lakini ilikuwa kwa moyo wangu, kwa urahisi tu kupata pumziko katika Kristo, Aliniokoa! Aliziosha dhambi zangu kwa Damu Yake! Wakati ule ule, niliacha kupinga Kristo. Ilikuwa tu rahisi kwamba nilichostahili kufanya ni kumwamini; Ninaweza fahamu wakati hasa nilijiachilia na Kristo akachukua usukani. Ilibidi nikubali! Muda huo sikuhisi jambo lolote katika mwili au mwanga unaopofusha, sikuhitaji kuhisi lolote, nilikuwa na Kristo! Kwa kumwamini Kristo nilihisi kama kwamba dhambi zangu zimeondolewa nafsini mwangu. Niligeuka kutoka kwa dhambi zangu, na nikamtazama Yesu pekee! Yesu aliniokoa.
     Ni upendo gani huu Yesu alinipenda nao kunisamehe mwenye dhambi ambaye hastahili aliyekua akiwa katika kanisa nzuri na bado akampa Yesu kisogo! Maneno hayatoshi kuelezea kuhusu uongofu wangu na jinsi ninavyompenda Yesu. Kristo aliachilia uhai Wake kwa ajili yangu na kwa hiyo najiachilia Kwake. Yesu aliacha kiti chake cha enzi ili aje afe msalabani kwa ajili yangu hata nilipokuwa nikitemea mate kanisa lake na kudhiaki wokovu Wake; Naweza aji kutangaza kwa njia ya kuridhisha upendo wake na rehema zake? Yesu alichukua chuki yangu na hasira yangu na badala ya hayo akanipa upendo. Alinipa zaidi ya moyo mpya – Alinipa uhai mpya. Ni kwa imani tu najua ya kwamba Yesu ameziosha dhambi zote, hujipata nikishangaa jinsi ninavyojua kutokana na uhaba wa ushahindi unaonekana, lakini kila mara ujikumbusha ya kwamba “imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana” na upata amani ninapotafakari na kujua kwamba imani yangu inamwegemeaYesu. Yesu ndiye jibu langu la pekee.
     Nina shukrani kwa Mungu kwa neema aliyenipa, nafasi nyingi alizonipa, na kwa kunivuta kwa nguvu kwa Mwanae kwa sababu sikuja kwa Yesu kwa uwezo wangu. Haya tu ni maneno, lakini imani yangu imemwegemea Yesu, kwa maana amenibadilisha. Yeye daima amekuwa nami, Mkombozi wangu, pumziko langu, na Mwokozi wangu. Upendo wangu kwake ni mdogo sana unapolinganishwa na jinsi anavyonipenda. Siwezi kumuishia muda mrefu au kuwa na uaminifu wa kutosha, siwezi kamwe kufanya mengi kwa Kristo. Furaha yangu ni kumtumikia Yesu! Alinipa uhai na Amani maana nilichojua hapo awali ni jinsi ya kuchukia. Yesu ndiye tamaa yangu na mwongozo wangu. Sijiamini, lakini naweka tumaini langu Kwake pekee, kwa maana hajawahi kunitelekeza. Kristo alinijia, na kwa hiyo sitamwacha.

Wewe ni mwenye dhambi aliyepotea kama alivyokuwa Yohana Cagan. Naweza tu kukwambia maneno niliyomwambia Yohana mwisho wa mahubiri wakati ule aliokoka, “Wewe ni mwenye dhambi. Umepotea. Hakuna yeyote anayeweza kukuokoa ila Yesu. Hiyo ndiyo sababu alikufa msalabani kulipia dhambi zako – na kusiosha zote na Damu Yake. Tunapoendelea kuimba, toka kwa kiti chako na uje mbele hapa! ‘Nimepotea! Ewe, Yesu, Osha dhambi zangu na Damu Yako iliyomwagika msalabani!’ Kuja hapa tunapoimba kifungu cha kwanza cha wimbo ‘Karibu na Msalaba.’” Huu ndio wimbo wa mwaliko tulioimba wakati Yohana Cagan aliokoka. Wengi wenu wanaujua. Huimbe. Na wanapoendelea kuimba, kuja hapa kwa madhabahu na umwamini Yesu.

Yesu, nidumishe karibu na msalaba, Pale kuna chemichemi ya thamani
   Bure kwa wote, kijito cha uponyanji Kitiririkacho kutoka mlima Kalivari.
Msalabani, msalabani, Uwe utukufu wangu milele;
   Hadi siku ya kunyakuliwa nafsi yangu ipate pumziko ng’ambo ya mto.
(“Karibu na Msalaba” na Fanny J. Crosby, 1820-1915).


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Maandiko yalisomwa kabla ya mahubiri na Bw. Haruni Yancy: Warumi 10:9-14.
Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Benjamini Kincaid Griffith:
“Karibu na Msalaba” (na Fanny J. Crosby, 1820-1915).


MWONGOZO WA

MAHUBIRI MATANO YALIYOTUMIKA KWA UONGOFU WA MWINJILISTI MCHANGA

FIVE SERMONS USED IN THE CONVERSION
OF A YOUNG EVANGELIST

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

“Tena wamsikieje pasipo mhubiri?” (Warumi 10:14).

I.   Kwanza, “Kutiwa Moyo kwa Wale ambao Hawako mbali na Wakovu” (Yalihubiriwa Jumapili asubuhi ya, Juni 7, 2009). Marko 12:34.

II.  Pili, “Ukalvini wa Kisasa na Uongofu Halisi” (yalihubiriwa Jumapili jioni ya, Juni 7, 2009). II Wakorintho 5:17.

III. Tatu, “Ni kwa Maombi na Kufunga tu” (yalihubiriwa Jumapili asubuhi ya, Juni 14, 2009). Marko 9:29.

IV. Nne, “Dhamiri na Uongofu” (yalihubiriwa Jumapili jioni ya, Juni 14, 2009). Warumi 2:15; I Timotheo 4:2; Yohana 3:18; Waebrania 9:14.

V.  Tano, “Bonde la Mifupa mikafu” (Nilihubiri mahubiri haya asubuhi ile Yohana Cagan aliongoka, Juni 21, 2009), Ezekieli 37:5; Yona 2:9.