Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.
UONGOFU WA KWELI – TOLEO LA 2015

REAL CONVERSION – 2015 EDITION
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Ujumbe uliohubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Katika siku ya Bwana Asubuhi ya, Januari 4, 2015
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Morning, January 4, 2015

“Akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 18:3).


Yesu alisema wasi, “Msipoongoka…hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.” Hivyo aliweka bayana kwamba lazima huwe mwongofu. Alisema ikiwa hautakuwa mwongofu “hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.”

Asubuhi ya leo nitakueleza ni nini inayotendeka kwa mtu aliyepata uongofu kamili.Tizama nilisema uongofu “kamili”. Kupitia kwa kutumia “ombi la mwenye dhambi,” na aina nyingine za uamuzi, mamilioni ya watu walipata tu uongofu wa uongo.

Tuna watu wachache kanisani kwetu,mke wangu akiwa mmoja wao, walioongoka mara ya kwanza injili ilipohubiriwa kwao kwa njia wasi. Lakini hawa wote walikuwa watu wazima waliokuwa tayari kwa sababu ya hali walizopitia katika maisha kabla ya kusikia Injili. Hakuna yeyote kati yao alikuwa mtoto mdogo. Wengi wa waongofu wa kweli kwetu, hadi sasa, ni kati ya vijana waliokuja kwa Kristo baada ya miezi kadhaa ( na hata miaka) ya kusikia mahubiri ya Injili. Spurgeon alisema, “Kunaweza kuwa na jambo kama imani mara ya kwanza, lakini kwa kawaida tunafikia imani kwa viwango” (C. H. Spurgeon, Mzunguko wa mlango wa wicket, Pilgrim Publications, 1992 reprint, p. 57). Hinzi ndizo “hatua” watu wengi hupitia.

I. Kwanza, unakuja kanisani kwa sababu zinginezo pasipo ile ya kuongoka.

Karibu kila mmoja huja kanisani mara chache za kwanza kwa sababu ambazo “si halisi”, kama nilivyofanya. Nilikuja kanisani nikiwa kijana kwa sababu jamii iliyoishi mlango uliokuwa karibu na wangu walinikaribisha kuja kanisani nao. Kwa hiyo nilianza kuja kanisani 1954 kwa sababu nilikuwa na upweke, na watu walioishi karibu nami walikuwa wazuri kwangu. Hiyo kwa kweli haikuwa sababu “sahihi”,sivyo? Nilitokea pale “mbele” baada ya mahubiri ya kwanza na nikabatizwa pasipo kufanyiwa ushahuri wowote, hata bila kuulizwa ni nini ilisababisha nitokee hapo mbele. Hivyo ndivyo nilivyo fanyika Mbaptisti. Lakini sikuwa nimeongoka. Nilikuja kwa sababu watu walioishi karibu nami walikuwa wazuri kwangu, si kwa sababu nilitaka kuongoka. Kwa hiyo nilipitia mapambano ya muda mrefu yaliyodumu miaka saba kabla ya kuongoka hatimaye Septemba 28, 1961, nilipomsikiza Dkt. Charles J. Woodbridge alipohubiri pale chuo cha Biola (ambacho sasa ni chuo kikuu cha Biola). Hiyo ndiyo siku niliyomwamini Yesu na akanitakaza na akaniokoa kutoka kwa dhambi.

Na wewe je? Ulikuja kanisani kwa sababu ulikuwa na upweke – ama kwa sababu wazazi wako walikuleta kanisani ukiwa mtoto? Ikiwa uko hapa asubuhi ya leo kwa sababu ya mazoea, kama mtoto aliyelelewa kanisani, haimaanishi ya kwamba umeongoka. Ama ulikuja nilivyokuja, kwa sababu ulikuwa na upweke na mtu alikukaribisha, na watu walikuwa wazuri kwako? Ikiwa ni hivyo, haimaanishi ya kwamba umeongoka. Usinielewe vibaya. Nina furaha kwamba uko hapa– iwe ni kwa mazoea kama mtoto kanisani, ama kwa sababu ya upweke, kama mimi nilipokuwa na umri wa miaka kumi na mitatu. Hizo ni sababu zinazoeleweka za kuja kanisani – lakini hazitakuokoa. Lazima huwe na uongofu wa kweli ili uokolewe. Ni lazima kwa hakika utake kuokolewa na Yesu. Hiyo ndiyo sababu “halisi” – ambayo ni ya pekee itakayokuokoa kutokana na maisha ya dhambi.

Si vibaya kuwa hapa kwa sababu ya mazoea ama kwa sababu ya upweke. Ni vile tu siyo sababu halisi. Ni lazima utake zaidi kuongoka, na si kwa sababu tu wewe ulihisi vizuri kuja kanisani.

II. Pili, unaanza kufahamu ya kwamba kuna Mungu.

Unaweza kuwa ulitambua ya kwamba Mungu anaishi kabla ya kuja kanisani. Lakini watu wengi wana tu ile hali ya kutokujua vizuri ,na kuwa na imani isiyo na uhahika kumhusu Mungu kabla hawajahubiriwa Injili. Pengine hiyo ndiyo iliyokuwa hali yako, ikiwa ni mtu alikuleta hapa.

Ikiwa ulilelewa kanisani, tayari unajua mengi kuhusu maandiko. Unaweza kupata kwa urahisi mahali unapohitaji kwa bibilia. Unajua njia ya uokofu. Unajuo vifungu vungi vya bibilia na pia nyimbo. Lakini Mungu bado kwako ni kama hayuko ama haumwelewi vizuri.

Alafu, ikiwa wewe ni mgeni ama mtoto wa kanisa, jambo linaanza kutendeka. Unaanza kutambua kwamba kuna Mungu – si tu kuongea kumhusu Mungu. Wewe sasa unamtambua ya kwamba Mungu yupo.

Tangu nilipokuwa mtoto mdogo sikumwelewa Mungu kikamilifu. Lakini sikumfahamu “ Mungu mkuu, mwenye kuogofya” ( Nehemia 1:5) wa bibilia hadi nilipotimiza miaka kumi na tano – kwa zaidi ya miaka miwili nilipoanza kuhudhuria kanisa la Baptisti pamoja na watu waliyoishi karibu nami. Siku ile nyanyangu alisikwa nilitorokea kwa miti kule makaburini na nikaanguka nikawa natokwa na jasho na kukosa hewa. Gafla Mungu akanishukia – na nikajua ya kwamba Yu hai, nikajua ya kwamba ni mwenye uwezo, na anaogofya, katika utakatifu wake. Lakini sikuwa nimeongoka.

Umewahi pitia hali kama hiyo? Je Mungu wa bibilia Yu hai kwako? Hilo ni jambo la maana sana. Bibilia inasema,

“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao” (Waebrania 11:6).

Kumwamini Mungu kunaitaji kiwango fulani cha imani – lakini siyo ile imani inayookoa. Si uongofu. Mamangu kila mara alisema, “Namwamini Mungu kila wakati.” Na sina shaka yeyote kwa mawazo yangu ya kwamba alifanya hivyo. Alimwamini Mungu tangu utotoni. Lakini hakuwa ameongoka hadi alipotimiza umri wa miaka 80. Ilikuwa muhimu kwamba alimwamini Mungu, likini jambo zaidi ya hilo lazima litendeke ili mtu aongoke kihalisi.

Hivyo, Nina sema, kwamba pengine ulikuja kanisani asubuhi ya leo bila kujua ukweli wa Mungu. Basi, pengine polepole, ama pengine kwa haraka, utaona ya kwamba kuna Mungu. Hiyo ndiyo sehemu ya pili, lakini uongofu badu.

III. Tatu, unafahamu ya kwamba umemkosea na umemkasirisha Mungu kwa dhambi zako.

Bibilia inasema, “waufuatao mwili [k.m. wasio ongoka] hawawezi kumpendeza Mungu.”(Warumi 8:8). Kwa hivyo uaanza kufahamu, kama mtu asiyeongoka, kwamba hakuna jambo lolote unalolifanya linaweza kumpendeza Mungu. Kwa kweli, unaanza kutambua ya kwamba wewe ni mwenye dhambi. Kila siku “Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,” (Warumi 2:5). Bibilia inasema:

“Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu aghadhibikaye kila siku” ( Zaburi 7:11).

Baada ya kugundua ya kwamba kwa hakika kuna Mungu, unaanza kutambua ya kwamba umemkosea Mungu kupitia dhambi zako. Na pia umemkosea Mungu kwa kutompenda. Dhambi ulizozitenda zilikuwa kinyume na Mungu na amri zake. Hivyo itakuwa dhairi kwako ya kwamba huu ni ukweli. Kukosa kwako kumpenda Mungu kutakuletea ufahamu kwamba ni dhambi kuu wakati huu. Lakini zaidi ya hiyo, unaanza kuona ya kwamba asilia yako ni yenye dhambi, ya kwamba hakuna kitu kizuri ndani yako, ya kwamba mwoyo wako una dhambi.

Hatua hii mara nyingi ilijulikana kama “mwamuko” na walioshikilia sana kuishi kwa tabia za dini. Lakini hakuwezi kuwa na mwamuko bila kuhisi kwa undani ile hali ya dhambi na kujihukumu kibinafsi. Utahisi kama John Newton alivyohisi alipoandika:

Ee Bwana, Nina uovu aji, Asiye mtakatifu na mchafu!
Ninaweza aji kukukaribia nikiwa na mzigo kiasi hiki wa dhambi?

Moyo huu ambao umechafuka ni makao yako?
Napiga, Kilele! Katika kila sehemu, Nina yaona maovu gani!
   (“Ee Bwana, Niko mchafu kiasi gani” na John Newton, 1725-1807).

Utaanza kufikiria kwa undani, wakati huu, kuhuzu hali yako ya dhambi katika mawazo na katika moyo. Utafikiria, “Moyo wangu una dhambi sana, na uko mbali na Mungu.” Wazo hilo litakusumbua. Utakuwa mwenye kugadhabishwa na kusumbuliwa na mawazo yako ya dhambi na ukosefu wa upendo kwa Mungu. Hali hii ya kijibaridi cha ukosefu wa uhai katika moyo wako kumwelekea Mungu itakusumbua kwa ndani katika hatua hii. Utaanza kutambua kwamba mtu mwenye moyo wa dhambi kama wako hana tumaini. Utaona ya kwamba inafaa na ni haki kwa Mungu kukupeleka jahanamu – kwa sababu unastahili kwenda jahanamu. Hivi ndivyo utakavyo fikiria utakapokuwa na mwamuko wa kweli na kugundua ya kwamba umemukosea Mungu na kumkasirisha kwa sababu ya dhambi zako. Hatua hii ya mwamuko ni hatua muhimu sana, lakini uongofu bado. Mtu anayeona jinsi alivyo mwenye dhambi amekuwa na mwamuko – lakini bado hajaongoka. Uongofu ni zaidi ya kuhukumika tu ya kwamba una dhambi.

Unaweza gundua gafla ya kwamba umemkosea Mungu, ama hali hii ya mwamuko inaweza kuendelea kutoka kwa mafundisho hadi kwa hali ya kuelewa kwamba Mungu amekosewa na hii haimpendezi. Ni wakati tu utakapopata ule mwamuko ya kwamba una dhambi na wewe si mtakatifu ndipo utakapokuwa tayari kwa hatua ya nne na ya tano “katika hatua hizi” za uongofu.

Charles Spurgeon alitambua ya kwamba ni mwenye dhambi alipokuwa na umri wa miaka 15. Baba yake na babu yake wote wawili walikuwa wahubiri. Waliishi katika nyakati ambazo “uamuzi” ulikuwa bado haujapaka tope uongofu wa kweli. Hivyo, baba yake na babu yake “hawakumusukuma” katika kufanya “uamuzi ambao si wa kweli kwa Yesu.” Badala ya hiyo, walingojea Mungu afanye kazi ya uongofu ndani yake. Nafikiri walifanya jambo la kweli.

Alipokuwa na miaka kumi na tano Spurgeon hatimaye alihisi kuhukumika kwa ndani kuhusu dhambi. Alieleza mwamuko wake kuhusu dhambi zake kwa maneno haya:

Mara hiyo gafla, Nilikutana na Musa, akizibeba mkononi sheria za Mungu, na aliponiaangalia, alionekana mwenye kuniangalia kwa ndani na macho yake ya moto. Yeye [aliniambia nisome] ‘maneno yale kumi ya Mungu’ – zile amri kumi – na nilivyo endelea kusisoma zote zilionekana kunihukumu na kunilaumu mbele ya Mungu mtakatifu.

Na akaona, katika hali hiyo, ya kwamba alikuwa mwenye dhambi mbele za Mungu, na ya kwamba hakuna “dini” au “utuwema” ungemuokoa. Barubaru Spurgeon alipitia kipindi cha dhiki kubwa. Alijaribu njia nyingi za kupata amani na Mungu kwa juhudi zake, lakini alifeli katika majaribio yote yake ya kupata Amani na Mungu. Hii inatupeleka katika hatua ya nne ya uongofu.

IV. Nne, unajaribu kujipatia uokofu, ama unajifundisha jinsi ya kuokolewa.

Mtu aliye na mwamuko atajihisi mwenye dhambi, lakini bado hatamgeukia Yesu. Nabii Isaya alieleza watu walio katika hali hii aliposema, “ Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.” (Isaya53:3). Tuko kama Adamu,aliyejua ya kwamba ni mwenye dhambi, likini alijificha kwa Mwokozi, na akajaribu kufunika dhambi zake na matawi ya mtini (Mwanzo 3:7, 8).

Kama Adamu, mwenye dhambi aliye na mwamuko hujaribu kufanya jambo ili ajiokoe na dhambi. Yeye ujaribu “kujifundisha” jinsi ya kuokolewa. Lakini anagundua “kujifundisha” hakuna manufaa yeyote, na kwamba “wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.” (2 Timotheo 3:7). Ama atatafuta jambo la “kuhisi” badala ya Yesu mwenyewe. Baadhi ya watu wanaotafuta jambo la “kuhisi” huendelea katika hali hii miezi mingi, kwa sababu hakuna mtu yeyote anayeweza kuokolewa kupitia “kuhisi.” Spurgeon alipata mwamuko wa dhambi zake. Lakini hakuamini ya kwamba angeokolewa tu kwa kuamini Yesu. Alisema,

Kabla sijakuja kwa Yesu, Nilijiambia, “Kwa kweli haiwezi kuwa hivyo, ikiwa nitamwamini Yesu, jinsi nilivyo, nitaokolewa? Ni lazima nihisi jambo; Ni lazima nifanye jambo” (ibid.).

Na hii inakupeleka katika hatua ya tano.

V. Tano, mwishowe unakuja tu kwa Yesu, na unamwamini pekee.

Barubaru Spurgeon mwishowe alisikia mhubiri akisema,“Mwangalie Kristo...Hakuma umuhimu wa kujiangalia wewe mwenyewe...Mwangalie Kristo.” Baada ya kusumbuka na kuwa na shida kwa ndani na uchungu – Spurgeon mwishowe alimwangalia Yesu na kumwamini Yeye. Spurgeon akasema, “ Niliokolewa kwa damu[ya Yesu]! Ningecheza danzi njia yote hadi nyumbani.”

Baada ya masumbufu haya yote na mashaka, aliacha kutazamia kuhisi jambo, ama jambo lingine lolote ndani yake. Alimwamini tu Yesu – Na Yesu akamwokoa mara hiyo hiyo. Mara hiyo akatakazwa kutokana na dhambi na damu ya Yesu Kristo! Ni rahisi, na bado ni tukio muhimu kabisa linalotendeka ndani ya mwanadamu. Huo, rafiki yangu, ndiyo uongofu kamili! Bibilia inasema, “Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.” (Matendo ya Mitume 16:31). Joseph Hart alisema,

Mara ile mwenye dhambi anapoamini,
   Na anamwamini Mungu wake aliyesulubishwa,
Anapokea msamaha mara hiyo,
   Ukombozi kamili kupitia damu Yake.
(“Mara ile mwenye dhami anapoamini” na Joseph Hart, 1712-1768).

Hitimisho

Yesu alisema,

“Akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 18:3).

Kama yule mhusika mkuu katika kuendelea kwa msafiri, usitosheke na uamuzi duni “unapofanya uamuzimuzi kwa Kristo.” Hapana! Hapana! Hakikisha kwamba uongofu wako ni halisi, kwa sababu ikiwa kwa hakika haujaongoka, “hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.” (Mathayo 18:3).

Kuwa na uongofu kamili

1.  Lazima huje katika ile hali ya kuamini kwa hakika ya kwamba kuna Mungu – Mungu halisi anayewapeleka wenye dhambi jahanamu wanapokufa.

2.  Lazima ujue, kwa kina ndani yako, ya kwamba wewe ni mwenye dhambi ambaye amemkosea Mungu. Unaweza kuendelea katika hali hii kwa muda mrefu (ama muda mfupi). Dkt. Cagan, Mchungaji wetu mshirikishi, alisema “Nilisumbuka mara nyingi usiku nikikosa usingizi baada ya Mungu kuwa halisi kwangu. Naweza kueleza kipindi hiki katika maisha yangu kama miaka miwili ya uchungu wa kifikira” (C. L. Cagan, Ph.D., Kutoka Darwin hadi kubuni, Whitaker House, 2006, p. 41).

3.  Lazima ujue hauwezi ukafanya jambo lolote nzuri kujipatanisha na Mungu aliyekosewa na aliye na hasira. Hakuna lolote unalolisema, ama kujifundisha, ama kufanya, ama kuhisi linaweza kukusaidia kwa lolote. Hilo lazima liwe dhahiri katika moyo wako.

4.  Lazima huje kwa Yesu, Mwana wa Mungu, na huoshwe kutokana na dhambi zako kwa damu Yake. Dkt. Cagan alisema, “Naweza kumbuka, hata kisekunde, nilipomwamini [Yesu]…Ilionekana kwamba nilikukutana na [Yesu]…Kwa hakika nilikuwa katika uwepo wa Yesu Kristo na kwa hakika alikuwa dhahiri kwangu. Kwa miaka mingi nilimkataa, ingawa kila mara alikuwa pale kwa anjili yangu, kwa upendo akinikaribisha kwa wokovu. Lakini usiku huo nilijua wakati umewadia kwangu ili nimwamini. Nilijua lazima nije kwake ama nimkatae. Wakati huo, kwa sekunde chache, nilikuja kwa Yesu. Sikuwa tena mtu asiye amini na ambaye alijiamini. Nilimwamini Yesu Kristo. Nilikuwa nimemwamini. Ilikuwa rahisi tu hivyo... Nilikuwa nikitoroka maisha yangu yote, lakini usiku huo niligeuka na mara hiyo moja kwa moja nikaja kwa Yesu Kristo” (C. L. Cagan, ibid., p. 19). Huo ndiyo uongofu wa kweli. Hivyo ndivyo unastahili kuhisi ili ubandilishwe kwa Kristo Yesu! Kuja kwa Yesu na umwamini! Atakuokoa na akutakase kutoka kwa dhambi zote na damu aliyomwaga msalabani! Amina.


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Maombi kabla ya mahubiri na Mr. Abel Prudhomme.
Wimbo unaoimbwa kabla ya mahubiri na Mr. Benjamin Kincaid Griffith:
“Neema ya ajabu” (na John Newton, 1725-1807).


MWONGOZO WA

UONGOFU WA KWELI – TOLEO LA 2015

REAL CONVERSION – 2015 EDITION

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

“Akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 18:3).

I.    Kwanza, unakuja kanisani kwa sababu nyingine pasipo ile ya
kuongoka.

II.   Pili, unaanza kujua ya kwamba kuna Mungu, Nehemia 1:5;
Waebrania 11:6.

III.  Tatu, Unatambua ya kwamba umemkosea Mungu na kumkasirisha
kupitia dhambi zako, Warumi 8:8; 2:5; Zaburi 7:11.

IV.  Nne, unajaribu kujipatia uokofu, ama kujifundisha jinsi ya
kuokolewa, Isaya 53:3; Mwanzo3:7, 8; 2 Timotheo 3:7.

V.   Tano, mwishowe unakuja kwa Yesu, na unamwamini Yeye
pekee, Matendo ya Mitume 16:31.